Malipo ya korosho yatawaliwa na dhuluma, Serikali yaombwa kumtuma CAG akague

britanicca

JF-Expert Member
May 20, 2015
15,634
29,997
Mbunge wa Mtama Nape Nnauye (CCM), amesema hali ya wakulima wa Korosho hivi sasa ni mbaya licha ya nia njema ya Rais kutaka wakulima wa zao hilo kulipwa, na badala yake zoezi hilo limetawaliwa na dhuluma pamoja rushwa, huku akibainisha kuwa zaidi ya wakulima 1181 bado mpaka sasa katika jimbo la Mtama hawajalipwa pesa zao.

Aidha Nape ameishauri Serikali kumruhusu Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, kwenda kufanya ukaguzi katika zoezi hilo ili kuubaini ukweli, huku akitaka wale wote waliohusika katika mchakato wa uuzaji Korosho wawajibishwe kutokana na dhuluma wanaodaiwa kuifanya kwa wananchi wa mkoani Mtwara.

Wakati Nape akiyasema hayo Mbunge wa Rombo (Chadema), Joseph Selasini, amemshauri Spika wa Bunge Job Ndugai kuunda kamati ya wabunge wachache, kukagua maghala ya kuhifadhi Korosho, lengo likiwa ni kubaini Kororsho nzima na zilizooza.

Katika hoja yake mbunge huyo ambaye pia ni Kaimu Mnadhimu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, amesema zaidi ya asilimia 30 ya Korosho zimeoza.

Raisi ndiye aliyewatuma.

Na kama kuna wakati wowote walitenda bila kufuata maagizo na maelekezo yake alipaswa kuwawajibisha na siyo kusubiri Wabunge na wananchi walalamike.

Rais alitamba kuwa korosho zitabanguliwa kwa MENO. Na alimtisha hata Waziri Mkuu kuwa atawapiga shangazi zake, wakinamama wa mikoa ya kusini.
 
Ile siku PM alimletea JPM wanunuzi waliojiandikisha kwake kua wako tayari kununua. JPM kwa jeuri akasema serikali itanunua na jeshi litabeba mzigo wote. Leo watu wanamung'unya maneno, JPM screwed up, this is on him and him alone!
 
Mbunge wa Mtama Nape Nnauye (CCM), amesema hali ya wakulima wa Korosho hivi sasa ni mbaya licha ya nia njema ya Rais kutaka wakulima wa zao hilo kulipwa, na badala yake zoezi hilo limetawaliwa na dhuluma pamoja rushwa, huku akibainisha kuwa zaidi ya wakulima 1181 bado mpaka sasa katika jimbo la Mtama hawajalipwa pesa zao.

Aidha Nape ameishauri Serikali kumruhusu Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, kwenda kufanya ukaguzi katika zoezi hilo ili kuubaini ukweli, huku akitaka wale wote waliohusika katika mchakato wa uuzaji Korosho wawajibishwe kutokana na dhuluma wanaodaiwa kuifanya kwa wananchi wa mkoani Mtwara.

Wakati Nape akiyasema hayo Mbunge wa Rombo (Chadema), Joseph Selasini, amemshauri Spika wa Bunge Job Ndugai kuunda kamati ya wabunge wachache, kukagua maghala ya kuhifadhi Korosho, lengo likiwa ni kubaini Kororsho nzima na zilizooza.

Katika hoja yake mbunge huyo ambaye pia ni Kaimu Mnadhimu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, amesema zaidi ya asilimia 30 ya Korosho zimeoza.
 
"Wameenda kuua na kukoroga lengo la Rais..."

Nani hao, amewataja?

Nape Nauye ...hivi hawezi akajikita katika kuwapigania wananchi wake jimboni bila ya kujitia aibu kwa namna hii anayotumia sasa?
 
Hata pwani yote hawajalipwa na korosho zinaoza magarani. Na ramadhani hii watu wananjaa kweli. Wanamhukumia Mungu. Magufuli kawanyoosha wanyonge wa korosho na wakanyooka kabisa kabisa.
 
Back
Top Bottom