Malipo ya King'amuzi cha DSTV na thamani ya shilingi ni changamoto

AFCON dstv unaweza kuona ukiwa na kifurishi hata kile kidogo cha Tsh 19975 per monthly pia na ligi ya hispania laliga
 
mimi natumia star times....jamaa hawa ni wababaishaji tu...hawana channel yoyote inayoonesha AFCON.. ndo maana inabidi niende kibanda umiza kucheki gem...

kuna wakati najutia kununua hiki king'amuzi chao....kiukweli hawatutendei haki wateja wao
Hauna channel inaitwa ABOOD mi naangalia hiyo katika king'amuz cha startime wanaonyesha mechi na ligi nyingi mfano EPL, SERIA A, LEAGUE 1,UEFA, NA EROUPA LEAGUE. nainjoy sana nipo Morogoro
 
Kifulushi cha bomba 19500 kinapatiaka DSTV au azam wanaoneha kupitia zbc2 game mwanzo mwisho kwa sh15000 tu kazi kwako mkuu
 
Mwakatopeter5 nimeipata hiyo mobdro channel ya Mpira inapatikana Vipi ni update please


Mkuu Ukishaidownload Unapofungua inafunguka Kama Hivi ↓↓
Then ingia Hapo Penye alama ya Jamaa anaeendesha Bicycle Ambapo Pameandikwa SPORTS utaziona Dozens Za Channel Za Soka.....




2017-01-18_16.13.52.jpg
 
Nashukuru nimefanikiwa kuidownload ila unaweza kupata tv station nyingine zaidi ya hizi walizonazo wao? Mfano mi nataka liverpool tv ila sijaiona kwenye list


Mkuu Jaribu Kuangalia Kwa Makini! Liverpool TV , Manu TV, Chelsea TV zote Zimo...
 
kwenye ulimwengu huu wa live streaming unahangaika nn na dstv?mie epl kila wiki naangalia live kwa streaming natumia goatd.net
 
Ni kipindi ambacho kwa sasa watanzania wengi nyakati za jioni wamekuwa wakitawanyika katika majumba ya starehe ikiwemo baa na vibandani kushuhudia mashindano ya Afcon yanayoendelea pale nchini Gabon.
Pamoja na hilo, naendelea na utafiti mfupi huku nikiwa na hoja ya msingi kuwa: je watanzania wengi hawana uwezo wa kulipia Dstv kama ambavyo wanaweza kufanya kwa ving'amuzi vya ndani ya nchi?!
Unaweza ukawa na hija nzuri kuhusiana na gharama za juu za dstv ila mfano ulioutumia una walakini kidogo, mashindano ya afcon unaweza pia kuyaona kupitia king'amuzi cha Azam kwa gharama ya 15,000 tu au hata bila ya kulipia kupitia channel ambazo zinaonekana kwenye other channels. Labda ungetolea mfano ligi kuu ya uingeleza nk, ila nakubaliana na weww kuwa dstv wana gharama za juu na kulingana na hali ya sasa ya kiuchumi, ni kweli imepelekea watanzania wwngi kuwa selwctive kwenye kwenye matumizi hususan kwenye mambo ya msingi.
 
mimi natumia star times....jamaa hawa ni wababaishaji tu...hawana channel yoyote inayoonesha AFCON.. ndo maana inabidi niende kibanda umiza kucheki gem...

kuna wakati najutia kununua hiki king'amuzi chao....kiukweli hawatutendei haki wateja wao
Kuondoka kwa Tido startimes na TBC hazina tofauti na channel za uchochoroni..inakuwaje wanashindwa kuonesha AFCON

VIONGOZI WANAFANYA NINI hasa akina Nnape..au kazi yao kubwa ni kuangalia habari chochezi..
 
Jamani hali ni ngumu. Mimi vifurush vya DSTv vya chini ya elfu 80,000 havina maana kwangu maana mimi ni mpenzi wa movies na musiki. Sasa kimeisha hii siku ya tatu. Najibania ili nipate tena iyo 80. Ila kusema kweli dstv ni very expensive. Mi naona waanza kuwa wanatukata kwa muda tunaoangalia tv. Mi tv naangalia nikitoka kazini saa 12 had saa 4 ila. Na nimeshakuwa adicted. Bila dstv sikai home
 
Back
Top Bottom