Malipo ni hapa Duniani Ndege ya Antonov 225 Vs Moskva Warship

bryan2

JF-Expert Member
Jun 8, 2016
3,323
4,667
Wahenga hawakukosea waliposema malipo ni hapa hapa duniani.

Mwanzoni kabisa wakati Russia ya Putin inafanya mashambulizi dhidi ya nchi ya kidemokrasia iliyokua imetulia kabisa Ukraine alishambulia ndege ya kawaida kabisa ya kubeba mizigo iliyohusika kutoa misaada ya kibinadamu Antonov 225 ndege kubwa kabisa duniani mfano kusafirisha chanjo za Covid 19 kwenye mataifa mbalimbali kama vile Canada hapa ilikua inafanya kazi ya kuokoa maisha ya watu na sio kutoa uhai.

Ila kwa vitendo vyake vya kiharamia majeshi ya Urusi yaliidondoshea makombora ndege ya Antonov iliyokua imepaki uwanja wa Hostomel Ukraine hakupiga kelele kabisa bali alishukuru kwa yote mpaka leo ukiniuliza kwanini Urusi alishambulia hiyo ndege ntakujibu ni ubabe wake tu Ukraine na Wivu.

Ila hapa juzi meli ya kivita ya kirusi imeshambulia na makombora ya Neptune ya Ukraine Urusi ameanza vitisho vyake mara Ntatumia Nyuklia, Mara Kyiv yote itakua flat, mara mataifa yote yanayoisaidia Ukraine watapata tabu...nk

Hivi Urusi ndiye mwenye mamlaka ya Kuishambulia Ukraine tu?
 
Hii vita ya urusi na ukrein ni vita ya piga ni kupige. Bwana mdogo kaamua kumdindishia mzee mzima na mzee mzima anaona akiishia njiani ataonekana kumbe ni yeye.

Ni mdebwedo sasa ni kutoana makamasi mwazo mwisho .Lakini ninacho kiiona hapa mahesabu ya mzee baba yalikuwa sio kupigana kwa mda mrefu hivi maana vita ni gharama lakini ndiyo hivyo tena maji ukiyavulia nguo sharti uyaooge unajua ukiwa ni bausa na watu wanakuamini mtaani kwamba unajua kuuchapa mkono alafu unapigana na kajamaa kakawaida alafu kamedindisha ile mbaya anabidi utumie hata mawe isije kuwa nishai ndio urusi anacho fanya ukrein that is not convetional war .

Urusi atafanya kila namna ashinde hii vita maana bila hivyo ni aibu kubwa kwake na ikijulikana kwamba yeye ni mfanya biashara wa silaha duniani iwe baridi jua mvua lazima kiileweke ingawa inacost
 
Hamna habari kuwa jamaa yenu ameshanyoosha mikono na kuamkia mkubwa ili asife?
1650226361-picsay.jpg
 
Ajabu sana kwa binadamu wa kawaida kushangilia upuuzi na hii nonsense war aliyoitaka Putin kwa hiyo hizo hapo ni Kambi za Jeshi au makazi ya watu kwa hiyo kilichompeleka Ukraine ni Kupiga mabomu makazi ya watu.

Ukienda mbali sana Putin sio binadamu wa kawaida either anahitaji sala sana na maombi haiwezekani binadamu wa kawaida unashuhudia watoto&wajawazito&bucha massacres halafu bado unacheka.

Mbona wengine hata kuchinja kuku tunaogopa.
 
Ajabu sana kwa binadamu wa kawaida kushangilia upuuzi na hii nonsense war aliyoitaka Putin kwa hiyo hizo hapo ni Kambi za Jeshi au makazi ya watu kwa hiyo kilichompeleka Ukraine ni Kupiga mabomu makazi ya watu.

Ukienda mbali sana Putin sio binadamu wa kawaida either anahitaji sala sana na maombi haiwezekani binadamu wa kawaida unashuhudia watoto&wajawazito&bucha massacres halafu bado unacheka.

Mbona wengine hata kuchinja kuku tunaogopa.
Bora putin ,Bush alipo ivamia Irak na Afghanistan mpaka vita inaisha zaidi ya watu million 2 walikuwa wamesha uawa, sasa ww hata watu 4000 hawajafika mnapiga kelele?

Utakuwa mpuuzi kiamini ya kwamba mwana siasa anajari maisha ya watu mbele ya maslahi yake.

Ukitaka kiamini ninayo yasema sasa hivi jaribuni kuingia mitaani kuiondoa CCM Madarakani muone kama hamjauawa kama sisimizi.
 
Back
Top Bottom