Malipo gerezani

kamonga

Senior Member
Feb 13, 2008
170
33
Baada ya kusikia mitaani kua eti wafungwa wanatakiwa kulipwa pesa kadhaa kwa ajili ya shughuli za uzalishaji wanazofanya pindi wawapo gerezani, ikanibidi niulize locally na kugundua ni shilingi mmoja kwa siku moja( tafadhali nisahihisheni kama nimekosea) hivyo wakifanya kazi mwaka yaani siku 365 na robo ni sh 365 tsh ndo wanazolipwa........

swali ni:- je fedha hii ya ujira ni halali ukilinganisha na pato linalotokana na jasho lao?
Je ni kweli wanalipwa hata hizo senti?
Je kama walipwi hebu fikiria wafungwa wapo wangapi, wamekaa miaka mingapi?
na Je ambae amebana pesa hizo ni kiasi gani over the years?
na ninani haswa?
chemsha bongo jamani.......wana JF
 
Serikali inashiriki ktk unyonyaji na ubaguzi against humanity.
hebu fikiria majengo yoote yanayojengwa na magereza wanatumia leba na utaalam wa wafungwa wao magereza input yao ni ndogo kulinganisha na kazi kubwa inayofanywa na inmates. Halafu mijisenti yoote inaishia kwa wajanja wachache ktk safu za uongozi wa magereza....

Mie nikisema tubadili katiba ili kurekebisha utoaji na usimamizi wa haki za wananchi.... tatizo wengine wanataka kubadili katiba ili iwasaidie kuingia madarakani...
 
kabla hawajakimbilia kufanya usanii (kama kawaida yao) waboreshe kwanza huduma muhimu za msingi kwa wafungwa. Wafungwa hawana maji, vibakuli vya kulia, madawa n.k. hivyo huu ni usanii kama walivyozoea kufanya usanii.
 
In principle, mtu ukifungwa unapoteza haki nyingi za kimsingi, ikiwa pamoja na haki ya kujiendeshea maisha.

Kulikuwa na kesi moja San Fransisco ya mwanasheria mmoja aliyefungwa kwa kutolipa kodi.mwanasheria huyu aliyezoea kulipwa mamia ya dola kwa saa, alijikuta anapata kazi ya kumwagilia bustani za jela kwa senti 19 za kimarekani kwa saa, hela ambayo ukilinganisha na mshahara wake wa uanasheria ilikuwa ni kama utani.

Serikali inaweza kusema mengi.Mfungwa anakosa baadhi ya haki zake za kiraia, ikiwamo ya kujiendeshea maisha, inaweza pia kusema uzalishaji unaotokana na kazi za wafungwa unatumika katika kuendeshea magereza na mambo mengine mengi.

Ukitoa mshahara mnono kwa wafungwa siajabu uswahilini kwetu watu wasio na kazi watafanya zali ili mradi waende kupata kazi za gerezani. Tena huko wala huna shida ya kufanya savings, hamna vishawishi vingi vya kutumia pesa na serikali inakutunzia mshiko wako mpaka unapotoka.

Ukishakubali wafungwa wafanye kazi tu, inakuwa vigumu kuwaombea mshahara wa maana.Ndiyo maana watu wanaopigania haki za wafungwa wanataka kupiga marufuku kabisa wafungwa kufanya kazi. Kwa mtu anayeangalia upande wa argument ya kwamba kazi za wafungwa zinaweza kusaidia kuendesha magereza kiuchumi, na hivyo kupunguza mzigo kwa walipakodi, hili swala la wafungwa kuacha kufanya kazi inakuwa haiyumkiniki.

Pia kuna wengine wanaoona kazi kama sehemu ya rehabilitation, kwa hiyo inabidi wafungwa wakubali the rehabilitative payment of work kuwa muhimu zaidi kuliko the economic aspect.

Wachina wanaongoza kwa kutumia prison labor, bidhaa nyingi zenye label ya "made in China" zimetengenezwa jela, kitu ambacho watu wa magharibi wanakilalamikia sana siku hizi.
 
Je wale wanawake waliofungwa kwa makosa ya waume zao, inakuwaje hiyo? Hapo kuna haki kweli? JK si aliahidi kulishughulikia hili alipoonana na yule mwanamke? Mbona kimya?
 
Mfungwa nielewavyo mimi ni kunyimwa Uhuru wako binafsi wa kutokuwa na jamii yako inayokuzunguka na Magereza ni chuo cha kurekebisha tabia.
But kumfanyisha kazi bila malipo hii sio haki kwani wafungwa wangelipwa japo wakawekewa ktk account zao za benki ili iweze kuwasaidia pindi anapotoka jela, wengi wa wafungwa waingiapo magereza wanafundishwa kazi nyingi like ufundi cherehani,magari na useremala, ufugaji hata kilimo. Mfano mzuri upo kwenye maonyesho ya sabasaba ukiingia ktk banda la magereza utaona jinsi walivyokuw ana fanicha nzuri,bustani nzuri,shughuli za ufugaji ziko njema hii yote ni nguvu ya wafungwa.
Je mfungwa mmoja kwa mwaka anaingizia jeshi la magereza kiasi gani na yeye anafaidika vipi?
1. Tuelewe mtu anapokuwa mfungwa kama alikuwa anafanya kazi halali basi ile kazi imekwisha potea.
2. Familia aliokuwa nayo kama yeye alikuwa ndie muhimili wa basi ile familia imeathirika.
3. Punde anapotoka magereza au amemaliza kifungo ni kwamba anaanza maisha yake upya au moja.
swali linakuwa Je! Tunawezaje kumsaidia mfungwa kujimudu kimaisha mara amalizapo kutumikia kifung?
1. Tukiweza kuwawezesha sidhani kama kuna mfungwa atarudia kufanya makosa ili arudishwe tena kifungoni. Ikiwa watakuwa wanalipwa na pesa zinawekwa ktk account zao na kupewe wanapomaliza kifungo hii itawasaidia kwa namna moja ama nyingine kujikimu.
2. wanapotoka gerezani wapewe vyeti vinavyo onyesha wamefuzu mafunzo ambayo vitatambulika kisheria ili viweze kuwasaidia kujiajiri au kuajiriwa ktk taasisi mbalimbali ziwe za kiserikali ama binafsi
 
Its so unfair.Atleast wangefanya some changes angalau even the little wnacho produce wapate even a 20% commission na hata wawafungulie acounts ili pale wanapotoka gerezani wasirudie kwenye makosa ila wawe na capital ya kurun their own lives.Hii itapunguza dependence ratio hata kuongeza rate ya economic growth.Lets not underestimate things.South Korea grew kwa sababu ya technical schools ambazo hapa Tanzania wale wanaofell kabisa ndio wanaenda huko.
This minor things could move mountains.
 
Siku zote ukisha itwa mfungwa basi haki yako imekwisha na maisha yako yapo rehani na unakabidhi roho yako mikononi mwa serikali,unakuwa kama mtoto wa serikali ulipwe usilipwe serikali ndo inayo amua.
Ila navyo jua mfungwa akimaliza kifungo anapewa nauli ya kurudi kwao hata kama unakaa mbali kiasi gani watakupigia hesabu ya nauli inayo simama kwa wakati huo.
Lakini inaonyesha kule kutakuwa na starehe mbona vibaka wanakaa mwaka kisha wanarudia tena makosa yale yale na wanarudi tena gerezani na mchezo unaendelea wanadai kule msosi ni bure tofauti na uraiani ni mpaka utumie akili nyingi sana kujipatia chakula cha kila siku kule ni bure.
 
Inawezekana serikali kupitia magereza hawajakaa chini na kufanya utafit wa kina kuhusu faida ya mfungwa kumlipa kwa kazi anazofanya za uzalishaji anapokuwa kifungoni....Mtazamo wao ni kumuadhibu mfungwa wakiamini ndio njia sahihi ya kumfundisha asifanye uharifu kitu ambacho mimi binafsi siamini sana..

Nakumbuka mwanzoni mwa mwezi Mei mwaka huu Kamanda wa Polisi wa mkoa wa kilimanjaro au Arusha aliwahi kusema kuwa matukio mengi ya uhalifu yaliyotokea katika mwezi huo yamechangiwa na wafungwa waliopata msamaha wa Raisi..ilinishangaza...
Lakini nikapata jibu kuwa yawezekana kabisa huyu mfungwa aliyetoka gerezani aidha kwa msamaha au kumaliza kifungo chake ni binadamu mwenye mahitaji yote ya kibinadamu na anapokuja uraiani akiwa hana chochote cha kumuendeshea maisha lazima utarajie arudie uhalifu huenda akiamini ni ndio njia rahisi ya kujipatia kipato...

So nakubaliana kabisa na wazo la wafungwa kulipwa angalau kima cha chini cha mshahara nina imani kwa mtu aliyekaa gerezani miaka 5 akitoka anakuwa amenufaika sana; kwanza atakuwa ameongeza ujuzi kwa shughuli alizokuwa akifanya gerezani, Pili anaweza kuja kuwa mjasiriamali mzuri huku uraiani anapotoka na mtaji na pia atakuwa amejifundisha kuwa maisha ni kazi halali na si uhalifu kwa hiyo uwezekano wa yeye kurudia uhalifu hautakuwepo...
 
Shida kubwa ni kwamba sheria zetu za magereza ni za tangu enzi za ukoloni. Wenzetu waliziweka kutukomoa sisi. Sasa tulipojitawala bado viongozi wetu kwa mtizamo finyu hawakufikir kuzifanyia marekebisho mazuri, wakati kule zilikotoka walishazibadili na kuziboresha.
Ni kweli ukifungwa unapoteza haki zako za kuwa nje uraiani. Nidiyo sababu viongozi wetu ambao kimsingi walitakiwa wengi kwa sababu ya ufisadi wawe wameshatangulia huko. Lakini kwa sababu wanajua hakuna haki za kibinadamu katika magereza yetu, wamepafanya magereza kama sehemu ya kupeleka wana wetu huko vijijini.
Simulizi zinaonyesha huko ni jehanamu ndogo lakini pia ni mahali pa kutoa digrii za uhalifu na si kurekebisha tabia kama wanavyotaka tuamini. Kama nasema uongo wale waliokwisha pita huko watatupa simulizi zinazoni support ninachosema.
Magereza pakiendelea kufanywa torturing camps badala ya mahali pa kuwasaidia watu kubadlika tabia mentaly, physicaly and spritualy tutaendela kuwa na magereza zilizosheheni watu kibao. Maana mateso pekee hayajawahi kusaidia kupunguza uharifu. Maisha yao pia ni bora yaboreshwe.
Mimi nitaendelea kuamini kwamba Magereza Tanzania ni kwa ajili ya watoto wetu wakulima kijijini, wapinzani wa kisiasa wa serikali ya chama cha mafisadi na watu wachache wa kada ya chini. Nitaamini kuwa ipo kurekebisha Tabia mafisadi wakishaanza kufungwa huko, tukianzia na wakina Lowasa, Karamagi, Msabaha na wengine wengi wanaochezea resources zetu.
Si mnakumbuka jinsi viongozi wetu waalifu wasivyokaa magerezani? Si mnakumbuka kisa cha Dito? na mnakumbuka hata visa vya watoto wa viongozi ambao wamekuwa convicted na wako nje kwa sababu magereza hazikujengwa kwa ajili yao?
Tafakari.
 
Swali langu ni moja tu kwa mtoa mada, Jiulize kwanini waliopo jela wengi ni maskini???? ukishafahamu hilo jibu unalo.
 
Mfungwa ni Mali ya Serikali wanaweza hata kukuua hukohuko gerezani na usishitaki kokote, mfungwa kwa Serikali ni kama punda wako wa kubebea mizigo
 
Back
Top Bottom