Malinzi tuachie TFF, Umeshindwa kuwalipa wafanyakazi mishahara tangu Machi 2016

Mwanagandila

Senior Member
Oct 9, 2011
182
100
Hali si shwari katika Shirikisho la Soka Tanzania TFF kufuatia kuwepo kwa hali mbaya, baada ya wafanyakazi wake kuendelea kufanya kazi kwa mwezi wa nne sasa bila ya kulipwa mishahara yao wala marupurupu ya aina yoyote.

Habari za ndani zinasema, ukata huo unatokana na ufujwaji mbaya wa pesa kutoka kwa Rais wake Jamal Malinzi ambaye amekua na matumizi mengi na safari za hapa na pal zisizo na tija pamoja na wapambe wake.

Katika hali ya kawaida Malinzi haonekani kujali wafanyakazi wake kutolipwa mishahara tangu Februari - Juni 206, zaidi anafika ofisini hapo na kutoka bila kufikiria wafanyakazi hao wanaishije.

TFF ya Tenga haikuwahi kufikia huku, na hii inaonyesha ni anguko jingine katika mpira wa miguu Tanzania.

Wachezaji wa Taifa Stars waligoma kuwavaa Misri wiki iliyopita mpaka walipolipwa posho za tokea mchezo dhidi ya Chad na Bonus zake siku moja kabla ya mchezo husika.

Kwa uongozi huu wa Malinzi maendeleo ya mpira wa miguu nchini yanazidi kurudi nyuma badala ya kwenda mbele alipoachiwa na aliyemtangulia.
 
Back
Top Bottom