mwengeso
JF-Expert Member
- Nov 27, 2014
- 9,227
- 6,666
Soka ni mchezo mkubwa kati ya michezo pendwa nchini na duniani, kwa kuwa hutoa ajira, shughuli za kibiashara na afya ya kimwili kwa wachezaji katika ngazi zote.
Katika ngazi ya msingi, zaidi ni ushiriki. Hivyo soka hukuza maendeleo ya mshiriki na kuimarisha uwezo wa moyo na mishipa na mifumo yake ya fahamu. Hii humsaidia mshiriki kuwa imara wakati wote. Katika ngazi ya juu, soka ni biashara na hutoa ajira na kulitangaza Taifa.
Lakini kinachotokea kwa sasa ni ubabaishaji wa uendeshaji soka Tanzania. Ligi inasimamishwa bila mpangilio. Juzi juzi TFF akaunti zake za benki zimezuiliwa na TRA kwa kutokulipa kodi, japo serikali imekuwa ikigharamia mishahara yao. Kwa nini Rais Malinzi asiwajibike mwenyewe kabla jipu alijatumbuliwa!
TAFAKARI CHUKUA HATUA