Malinzi na Mwesigwa waendelea kuzoeshwa maisha ya kuishi Segerea

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,385
108,441
Muda mchache uliopita Viongozi wa TFF Rais Jamal Emil Malinzi na Katibu Mkuu wake Celestine Mwesigwa wamerudishwa tena Segerea hadi tarehe 31 mwezi huu ambapo Kesi yao itatajwa tena baada ya upande wa Washtaki kukataa ombi la Mawakili wa hawa Viongozi.

Nawasilisha.
 
dah uchaguzi ule na zengwe la mikoani alofanya akishirikiana na yule mkurugenzi wa ufundi ambaye hajui figisufigisu ila kuzifanya anajua
 
Mahakama ya Kisutu imewarudisha rumande Rais wa TFF, Jamal Malinzi na maofisa wawili wa shirikisho hilo, kufikishwa tena kortini Julai 31.

DE65HPVXYAAlV-2.jpg
 
"Upelelezi haujakamilika" na ukikamilika itaanza safari ya "mahakama hii haina uwezo wa kusikiliza kesi hii"
 
MALINZI AGONGA TENA MWAMBA KISUTU ,AREJESHWA RUMANDE MPAKA JULAI 31


Dar Es Salaam,Tanzania.

KESI inayomkabiri Rais wa shirikisho la soka Tanzania (TFF),Jamal Malinzi,Katibu wake Celestine Mwesigwa na Mtunza Fedha,Nsiande Mwanga imesoma tena leo asubuhi kwenye mahakama ya Kisutu,Dar Es Salaam.

Imeamuliwa kuwa Malinzi pamoja na wenzake warejeshwe tena rumande kwa madai kuwa upelelezi wa kesi yao bado haujakamilika na watarejeshwa tena mahakamani hapo Julai 31 mwaka huu.

Malinzi anakabiriwa na mashitaka 28 ya kughushi nyaraka na kutakatisha fedha wakati Mwesigwa na Mwanga wanakabiriwa na mashitaka matatu kila mmoja.

Malinzi na wenzake walifikishwa kwenye mahakama ya Kisutu kwa mara ya kwanza Juni 29 kabla ya kupandishwa tena kizimbani Julai 3 mwaka huu.
 
Back
Top Bottom