Malinyi yapata diwani mpya wa chadema, ubunge ccm iko njia panda..... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Malinyi yapata diwani mpya wa chadema, ubunge ccm iko njia panda.....

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by FDR.Jr, Oct 31, 2010.

 1. FDR.Jr

  FDR.Jr JF-Expert Member

  #1
  Oct 31, 2010
  Joined: Jun 17, 2008
  Messages: 1,335
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 145
  wananchi wa kata ya malinyi wamemchagua ndg said tira kuwa diwani wao, kura zilizo mpa ushindi diwani mteule tira zimetoa taswira na ishara kuwa mgombea ubunge wa chadema prof. Mlambiti anayo nafasi ya kumshinda tabibu haji mponda wa ccm. Mpaka sasa prof. Mlambiti amepata kura 70% ktk tarafa za malinyi na ngoheranga. Wagombea wote wawili wanatokea tarafa ya mtimbira na wote ni wapogoro, kazi hapa iko kwa ccm sasa kuchakachua itete,lupiro na mtimbira kwenyewe maana malinyi wao wameiunga mkono chadema.
   
 2. N

  Njaare JF-Expert Member

  #2
  Oct 31, 2010
  Joined: Sep 26, 2010
  Messages: 1,075
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Mzee Mlambiti tuakuombea Mungu Upate ushindi wa kishindo ili "wasio na uchungu na nchi hii na wanaoona kuwa kuunga mkono upinzani ni dhambi" wajue kuwa watanzania wanakuhitaji. Dr Slaa utakapopata Uraisi mpe Professor uwaziri wa Elimu ya juu au Kilimo.
   
 3. S

  Shiefl Senior Member

  #3
  Oct 31, 2010
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 145
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Thats wonderful:yield:
   
 4. B

  Brandon JF-Expert Member

  #4
  Oct 31, 2010
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 336
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Wow,my prof mlambiti! Mungu msaidie ashinde.

  Nakumbuka lecturez zake jamaa ana uchungu sana wa nchi.

  Viva people's power......
   
 5. c

  chanai JF-Expert Member

  #5
  Oct 31, 2010
  Joined: Oct 9, 2010
  Messages: 279
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hawataweza kuchakachua mwaka huu
   
 6. engmtolera

  engmtolera Verified User

  #6
  Oct 31, 2010
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 5,081
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Mimi nimefanya kazi malinyi,itete ni ngome ya chadema mtimbila ndiko alikozaliwa mlambiti na lupilo ni ngome ya chadema,hivyooo chademaaa juu
  prof mlambiti toka sua anachukuwa ubungeeee mkuuuuu
   
 7. FDR.Jr

  FDR.Jr JF-Expert Member

  #7
  Nov 1, 2010
  Joined: Jun 17, 2008
  Messages: 1,335
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 145
  nimekupata mtolera, chadema wameshinda pia tarafa ya lupiro kwa madiwani, ubunge na urais. Msimamizi wa ulanga magh ameahidi saa sita hii usiku anatoa matokeo yote. Huenda ulanga magh na kilombero itaenda chadema. Congrats to sua students wamemsaidia sana prof this time ktk kamp
   
 8. Ngolinda

  Ngolinda Senior Member

  #8
  Nov 1, 2010
  Joined: Apr 12, 2010
  Messages: 125
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Prof. Mlambiti tunakutakia ushindi wa heshima.
  Sasa kura zitatosha. CCM walizoea kukuibia kwa kupitia jambazi lao Ngasongwa.
   
 9. mudushi

  mudushi Senior Member

  #9
  Nov 1, 2010
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 152
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Bravo Mlambiti. Lazima kieleweke tu.
   
 10. FDR.Jr

  FDR.Jr JF-Expert Member

  #10
  Nov 1, 2010
  Joined: Jun 17, 2008
  Messages: 1,335
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 145
  prof. Mlambiti wa chadema ndie mshindi na kinachosubiriwa ni nec ulanga kumtangaza, tarafa za malinyi na ngoheranga historically ndio ngome thabiti za ccm lakini 2010 wameamua kuchagua mtu na siyo chama, msingi wa taarifa yangu jamvini unategemea fact hizi.

  tarafa za ngoheranga na malinyi zina kata tano katika hizo tano ccm wameshinda 4 na chadema 1 hiyo ni udiwani, kwenye ubunge kura 75 % zote zimeenda chadema, maana prof ameshinda almost 99 polling station za tarafa hizi isipokuwa vijiji vya ihowanja na mbalinyi. Hapa ameshinda sana kwa sababu ya majeraha ya kura za maoni hususani vijana waliojitokeza kumuangusha dkt.ngasongwa baada ya wao nao kuchakachuliwa na tabibu mponda kwa nguvu ya celina kombani na ccm wilaya wakaiasi ccm na kumpigia debe prof. Mlambiti, kosa lingine ni kitendo cha mgombea wa ccm tabibu hadji mponda ni kuitenga na kuidharirisha kambi ya ngasongwa ktk kampeni zake kwa imani kuwa yassin njayagha na simon ngonyani watamsaidia hali ikawa ni tofauti sana maana hao aliowategemea ndio waliotuma majeshi ya kummaliza. Alisituka kuitafuta shuka alfajiri kuwa jamaa wanammaliza tena baada ya ujio wa kingunge jimboni aliyeagiza wagombea wote ktk kura za maoni warudi jimboni na kumtaka dkt ngasongwa akaokoe jahazi, bahati mbaya dkt ngasongwa akiwa ktk safari ya kuitikia wito akapata ajali njiani na kumfanya kukosa sehemu kubwa ya kampeni za lala salama ingawaje ndio aliwaokoa madiwani wa ngoheranga, biro na ihowanja. Dakika za lala salama ccm waliliona tatizo na kuwataka njaygha na ngonyani wakasafishe sumu walioipanda jimboni kama wasemavyo waswahili siku ya kufa nyani vijana hao wakiwa ktk gari moja walipata ajali sehemu ileile ambayo dkt ngasongwa alipatwa na ajali na kujikuta wanarudi mjini ifakara kwa matibabu na kumuacha tabibi hadji mponda akipata sapoti toka kwa alhaj ngasongwa ili kuirejesha malinyi ccm.

  tarafa ya mtimbira takwimu zaonyesha kuna kata 6 katika hizo chadema ameshinda mbili lakini kura za ubunge zimegawanyika 55% ccm na 45 chadema, hii imetokana na uzawa wa wagombea wote wawili, wote wanatoka tarafa hiyo na ni wapogoro vidabagha tabibu hadji mponda kwa mtimbira yeye ni mhamiaji lakini prof ni mzawa halisi wa mtimbira, kinachosumbua hapa ni wanamtimbira kuwekwa njia panda ila advantage imekwenda kwa prof.mlambiti na chadema, tarafa ya lupiro kuna kata tano chadema wamezinyakua 2, katika ubunge kura zimegawanyika kwa 55 chadema na ccm 45, hii imetokana na majeruhi wa kura za maoni ccm ndg njayagha ambaye ni mzaliwa wa lupiro kumuunga mkono prof.mlambiti .

  mtaji mkubwa hapa ni kura za maoni ndani ya ccm, uongozi wa ccm mkoa na wilaya ulielekeza nguvu ya kumng'oa hasimu wao mkuu dkt ngasongwa wakiamini kuwa tatizo lao ulanga magh ni ngasongwa wakasahau kura jimboni humo ni za mtu si chama. Katibu wa ccm alikula 5m toka mgombea wa ccm anayeshindwa uchaguzi sasa na kijana ngonyani na mkiti alikula mzigo kwa wagombea wa udiwani karibu wote ++yassin njayagha.
  kwa msingi huo prof.mlambiti ndio chaguo la ulanga magharibi 201-15.

  ktk hali hii ccm ulanga 2012 inatakiwa ifanyiwe overhaul halisi kuelekea 2015,ccm tujipange upya 2015.
   
 11. FDR.Jr

  FDR.Jr JF-Expert Member

  #11
  Nov 1, 2010
  Joined: Jun 17, 2008
  Messages: 1,335
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 145
  Habari za punde ulanga magharibi kuna mchezo unataka kufanywa kumpoka ushindi prof mlambiti, tarafa ya mtimbira ambako wagombea wote wawili wanaopambana wanatokea matokea hayajawekwa hadharani mpaka daki 5 zilizopita, kuna kada mmoja wa chama cha mapinduzi ameatawanya habari kuwa ccm imeshinda kwa kura 12 dhidi ya elfu nane za prof mlambiti.

  Tume yenyewe ahaijasema lolote mpaka sasa licha ya kuwa jana iliahidiwa kuwa leo saa sita usiku matokeo yangelikuwa hadharani.

  Chadema makao makuu wanapaswa kuilifuatilia jambo hili kwa speed ya umeme vinginveyo ccm watampora kura prof.mlambiti
   
 12. FDR.Jr

  FDR.Jr JF-Expert Member

  #12
  Nov 1, 2010
  Joined: Jun 17, 2008
  Messages: 1,335
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 145
  Kada huyu anaitwa kanduru ni mwenyeji wa lupiro pale
   
 13. TUKUTUKU

  TUKUTUKU JF-Expert Member

  #13
  Nov 1, 2010
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 11,852
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Hongera sana prof mlambiti,nakutakia kila la kheri!!
   
 14. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #14
  Nov 1, 2010
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160

  Kazi ipo! Mungu saidia hilo lenye kuleta utata lipotee kama upepo
   
 15. FDR.Jr

  FDR.Jr JF-Expert Member

  #15
  Nov 1, 2010
  Joined: Jun 17, 2008
  Messages: 1,335
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 145
  Taarifa nilizo nazo ni mchezo uleule waliomfanyia dkt. Ngasongwa pale mtimbira, kura zinazoingizwa sasa toka mtimbira ni zile za kupikwa ili kumpa margin mgombea wa ccm. Kuna taarifa wazi kuwa mawakala wa chadema pale mtimbira wamenunuliwa kwa fedha ili kuruhusu mchezo huo ufanywe na kuzibariki kura hizo, sasa sijajua upande wa chadema wao wanasemaje juu ya hili. Maana takwimu hazituonyeshi kuwa kuna wapiga kura wa kiasi hicho mtimbira.

  Chadema makao makuu kama wamo humu wawashe helicopter waende huko kumnusuru prof mlambiti
   
 16. i

  igoji Member

  #16
  Nov 1, 2010
  Joined: Sep 5, 2010
  Messages: 65
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Wasuaso tunakutakia kila lakheri prof. Mlambiti, kwa chaguzi mbili zilizopita( 2000, 2005) ngasongwa alikuibia kura. tunafahamu uchungu ulionao kwa nchi hii. sasa ni wakati wako kuongoza mapambano ya kuibadili nchi hii.
   
 17. FDR.Jr

  FDR.Jr JF-Expert Member

  #17
  Nov 1, 2010
  Joined: Jun 17, 2008
  Messages: 1,335
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 145
  Matokeo yatakayotangazwa ulanga magh. Ni ushindi kwa tabibu hadji hussein mponda dhidi ya profesa mlambiti. Ni matokeo yasiyo na ridhaa ya wana ulanga magharibi lakini inatubidi sote kama wanafunzi wa demokrasia turudi ktk mstari wa kukubali na kuheshimu matokeo hayo.

  Udiwani umekaa hivi kule ulanga magharibi. Ni kweli kuna wards 15 au 16 ila nina hakika na hizi zifuatazo.
  kata za ulanga magharibi ni hizi hapa
  1. kivukoni-chadema
  2. mavimba/minepa-ccm
  3. lupiro-chadema
  4. kichangani-ccm
  5. iragua-ccm
  6. itete-chadema
  7. njiwa-chadema
  8. mtimbira/madira-ccm
  9. mtimbira-usangule-ccm
  10. sofi-tlp
  11. malinyi-chadema
  12. igawa-ccm
  13. biro-ccm
  14. ngoheranga-ccm
  15. kilosa kwa mpepo-ccm
  ukweli ndio huo na ni mtindo uliomuondoa dkt ngasongwa ktk kura za maoni chini ya uratibu wa celina kombani,ccm wilaya na mkoa ndio umetumika kumtoa roho profesa mlambiti.

  amini usiamini mtimbira hawana vote za kumshindisha mgombea yeyote katika hali ya namna hiyo. Tafakarini wana ulanga na tupatieni majibu 2015.

  mbunge mpya apewe ushirikiano ktk agenda hizi na siyo vinginevyo
  • wilaya mpya ya malinyi pasipo kuporwa mipaka ya sasa ya ulanga magharib
  • umeme
  • songea road
  • elimubora
  • elimu ya uraia kwa kila mwananchi
  • afya na huduma zingine za jamii
  ikiwa mgombea anatumia milioni 50-100 kupata ubunge kwanini basi mtu huyu akishaapishwa akwepe jukumu la kuwa kinara wa maendeleo kwa hali na mali, daima utu haununuliwi.
  ninawapongeza kwa kuthubutu kuleta mabadiliko, daima safari ni hatua nanyi mko safarini.........

  ninawasilisha
   
 18. S

  Solomon David JF-Expert Member

  #18
  Nov 1, 2010
  Joined: Mar 1, 2009
  Messages: 1,148
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  hongera wana malinyi kwa kazi nzuri
   
Loading...