FDR.Jr
JF-Expert Member
- Jun 17, 2008
- 1,359
- 353
Wiki hii kumetokea mgogoro kati ya wafugaji(Wasukuma) na wananchi wa Igawa-Malinyi; chanzo cha mgogoro huu mpya ni watumishi wetu wa vyombo vya ulinzi na usalama kukiuka maadili ya kutunza identity ya mtoa taarifa/chanzo cha habari.
Tangu mwaka jana kule Ulanga Magharib kulikuwa na zoezi la kuwaondoa wafugaji na kuhakikisha kilakaya inabaki na mifugo yenye idadi ndogo na isiyo na madhara ktk kilimo; eneo la Ulanga Magharibi si eneo la ufugaji bali kilimo....
Kuna mwananchi alitoa taarifa kwa vyombo vya ulinzi na usalama kuwa licha ya zoezi hili la kuondoa mifugo kuonekana limekamilika lakini bado kuna wafugaji wamehodhi mifugo mingi mno ktk eneo lao....jamaa wa usalama wakarejesha habari kwa wafugaji...
Ijumaa kuamkia Jmosi usiku wafugaji wakamvamia mtoa taarifa na kumuua .....kitendo hicho kikaamsha hasira ya wakulima na wananchi wa Igawa wakawasaka waliohusika na kumpata mmoja wao ambae alikiri kuhusika na jinsi walivyoarifiwa juu ya mtoa habari...kwa bahati mbaya sana wana Igawa kwa uzembe wakamchoma moto Mfugaji yule baada ya kukiri...
Juzi Mkuu wa Wilaya ya Ulanga amabaye naye anatuhumiwa kuwa ni chanzo na msingi wa tatizo hili alikwenda Malinyi Igawa na kuongea na wafugajikwa faragha kisha akaja kuongea na wana Malinyi akikemea hulka za kujichukulia sheria mikononi mwao...akawaambia midhali kila upande umejitwalia sheria mkononi basi anaomba hali hiyoiishe na isijirudie....
Jana akaleta askari na kuwakamata wananchi wanaohisiwa kumchoma moto mfugaji na kuwatupa selo jambo liliowaudhi wananchi wa Igawa ambao tangu jana walimtaka awaachie huru kama alivyowaacha wafugaji....
Leo asubuhi wamevamia kituo cha polisi tarafa ya Malinyi wamekipiga moto, wamewatoa mahabusu wote lakini kuna madhara yamejitokeza ktk vurugu hizo...risasi za moto toka polisi zimetumika na kuna watu takribani watatu wanahisiwa kufa au kujeruhiwa hapo polisi Malinyi....
Tunatoa wito kwa serikali na viongozi wa jamii kulimaliza tatizo hili haraka ili kuepusha umwagaji mkubwa wa damu.
Media houses tusaidieni kuweka wazi undani wa sakata hili ambao tangu 2011 umekuwa ukichukua uhai wa wananchi, jiridhisheni kwa taarifa kwa kuwasiliana na Mh. Mbunge Hajj Mponda na diwani wa Malinyi Mh.Tira 0755397467
Mungu Ibariki Tanzania
Mungu Iponye Malinyi....