Malighafi zinazotumika Tanzania kutengeneza barakoa zinatoka nje au zinazalishwa na rasilimali zetu?

kifupi kirefu

JF-Expert Member
Oct 29, 2018
539
3,507
Naona MSD wanahamasisha tununue barakoa za ndani lakini kimwonekano zinafanana na zile za majuu kuanzia size,rangi na kila kitu.

Najiuliza hizi barakoa zinazalishwa kwa malighafi za ndani au tunaagiza? Kama zinazalishwa ndani wamiliki wa kiwanda ni wazalendo wenzetu au ni ndugu zetu wa magaharibi?

Lakini kwa hizi nyingine za vitenge, je barakoa hizi zinaviwango? Nani anapima ubora wakati zinazalishwa kila penye cherehani? Je, malighafi zinatoka wapi?

Kwanin barakoa za ndani zilizothibitishwa na TBS zisiwe nembo maalumu konyesha ni Mali yetu?

Tuwalinde Watanzania kwa elimu na bidhaa zifaazo Kama ALIVYOELEKEZA baba
 
Kauli nyingine za Jiwe zinapaswa kupuuzwa.

Kwa mfano, kuna wakati alisema lazima uniform za magereza, wanajeshi, zishonwe hapa Tz kwasababu zikishonwa nje zinaweza kuwekwa upupu halafu askari wetu wakashindwa kupigana vita.

Wakati anayasema hayo, majeshi yetu yanapokea silaha na vifaa vya kijeshi toka nchi za nje.
 
Kuna mshauri mmoja kasema ukiona mtu ana zuia wenzake kuvaa barakoa ni ishara kwamba hata kondom haja wahi kuvaa. Hivyo ana umwa. Sijui kama ni kweli!!!!
 
Nyie wenzangu, naomba mnitajie taifa moja tu ambalo lina nia mbaya na Tanzania ili tujiepushe nalo kuliko kutishana tu kwamba kuna watu wanatupiga vita wakati Kabudi yuko huko huko akiwasujudu wanaoitwa mabeberu. Sikuwahi kuwaza kwamba Bashiru ni mtupu kiasi hicho kichwani.
 
..kauli nyingine za Jiwe zinapaswa kupuuzwa.

..kwa mfano, kuna wakati alisema lazima uniform za magereza, wanajeshi, zishonwe hapa Tz kwasababu zikishonwa nje zinaweza kuwekwa upupu halafu askari wetu wakashindwa kupigana vita.

..wakati anayasema hayo, majeshi yetu yanapokea silaha na vifaa vya kijeshi toka nchi za nje.
kaka hii kauli aliisema wapi na lini? natamani nijue.
he cant be serious anaongea trash kiasi hiko.
 
Back
Top Bottom