MALIASILI UPDATES: Makinda Aipangua hoja ya dharura ya Wenje kuhusu umeme

GHOST RYDER

JF-Expert Member
Jun 10, 2011
1,025
475
Muda mfupi uliopita Mbunge wa Nyamagana CDM Mh. Ezekiah Wenje amenukuu kifungu kinachoruhusu kujadiliwa kwa jambo la dharula katika Nchi na kumtaka Spika kuuahirisha Mjadala wa Wizara ya Maliasili na Utalii na Badala yake kuruhusu Mjadala wa Suala la Dharula la Umeme.

Umeme umekuwa kadhia kubwa kwa sasa na shuguli nyingine zinazotegemea Umeme zimekwama jumla kama usukumaji wa Pampu za maji, uzalishaji viwandani, usagishaji wa nafaka na masuala maengine mengi ya kiuchumi.

Katika Hali isiyokuwa ya kawaida Spika anaitaka serikali kuja na Majibu ya Uhakika...Yaaaapi hayo????????????
 
Jana nilipata Bahati ya kusikiliza Radio Kiss FM inayotangaza kutoka Mwz mjadala ulikuwa kuhusu hali ya Umeme na maji huko Mwanza. Jiji limekuwa zizi Ndoo na mabeseni yanabebwa kila pahala huko kwa sasa.

Nimechek na mdau huo Rocky City ananiambia baadaya Kelele za Kiss Maji yametoka saa 4 usiku na mpaka sasa yapo...Sasa Idara ya Maji walikuwa wapi mpaka kelele hizo na News ya jana Star TV usiku hii ni aibu

NGUVU ya UMMA Mbele kwa mbele
 
GR Maji hakuna, huku maeneo ya Bwiru, Ilemela, Pasiansi, kirumba, kitangiri....inshort wilaya nzima ya Ilemela na Jiji zima siku ya tatu leo hakuna kitu kinaitwa Umeme, maji ya bomba wala saloon zinazofanya kazi! Tunashukuru Mungu hali ya ubaridi kwa muda wote huo kuoga tumesahau!
 
hebu fanyab raking vema utupe yayojiri huko... A TOWN tunategemea feedback soon
 
Hii ni aibu ya hali ya juu, ndo serikali tuliyo nayo hii
Siku tatu jiji kama la Mwanza halina maji, harafu serikali inahubiri kuwa Maji ni uhai???
Is this not a sense os stupidity?
 
Viongozi wabovu sana ila wanabebana tu,upuuzi huu watu siku tatu hakuna maji?wanafanya nini ofisini hao idara ya maji?posho tu!
 
Hakuna mashaka mara nyingi hoja za dharura za wapinzani zinaonekana hazina mashiko. Nakumbuka mabomu ya gongo la mboto yalipolipuka Tundu Lissu aliomba bunge lijadili issue hiyo kama hoja ya dharura lakini spika makinda aliitolea nnje akidai hajaridhika kama jambo hilo lilikuwa la dharura. Pengine hoja ingetolewa na mbunge wa ccm ingekubaliwa.
 
Jamani kwa hili mnamuonea spika.Hajatupilia mbali hoja ya Wenje bali amemtaka waziri mhusika aje na majibu ya kueleweka baadaye kuhusu tataizo hilo la umeme.Na ndio maana wapinzani wote walimpigia makofi spika baada ya kutoa uamuzi huo.Nadhani mtoa mada hajamuelewa vizuri spika.
 
GR Maji hakuna, huku maeneo ya Bwiru, Ilemela, Pasiansi, kirumba, kitangiri....inshort wilaya nzima ya Ilemela na Jiji zima siku ya tatu leo hakuna kitu kinaitwa Umeme, maji ya bomba wala saloon zinazofanya kazi! Tunashukuru Mungu hali ya ubaridi kwa muda wote huo kuoga tumesahau!

Makosa makubwa sana wabunge wetu walifanya kile kupitisha tu Budget mzee na mgao ukaanza the next day sasa sielewi hapo serikali hili halija ona au huko Dodoma wao kila kitu kipo???
 
Kama wamekataa kuijadili bungeni, basi sisi tuingie mitaani.

Me nawaaambieni pale bungeni kuna watu wanajiona wao ndio wao kwenye hivyo vyeo ili hali hawajui uwajibikaji wao tatizo kubwa hapa ni serikali kutowajibika kwa kipindi kirefu mkapa nchi ikumbwe na tatizo ndipo itajitokeza na kujifanya ina mikakati imala huku hakuna kitu

Dawa sisi ni Magogoni au Ikulu ya Dodoma period nchi ilisha washinda hawa wana CCM kabisa
 
Hawa wabunge wengine kama huyu Wenje naona wanajitafutia umaarufu wa kijinga. Swala la umeme wa dharura limeshajadiliwa na mitambo imepigwa picha inafungwa Ubungo na Waziri husika kisha sema mpaka December ndio ukali wa mgao utakwisha! Sasa huyu Wenje anataka blah blah za nini?
 
MH MAMA MAKINDA PUNGUZA UCCM!

Mama mjengoni punguza UCCM, unakumaliza kisiasa, unazidi kukuongezea Ujuha katika kazi yako mjengoni.
Maana ungeruhusu ule mjadala wa dharura imani yangi Govt legelege ingekuja na Taarifa ya Maana kama walivyofanya ktk sakata la nishati last tym..., but wasipojadiliwa hawa jamaa siyo WASIKIVU ni WALEGEVU TOSHA,
hata yale mavazi ya wasanii Mlegezo ni afadhali kuliko huu Ulegevu wa Govt ya JK...!

Mama Makinda ukae ukujua ya kwamba ni Watanzania wote wanaouumia na haya matatizo ya kukosekana kwa Umeme na Maji kwa baadhi ya mikoa hapa Tanzania.
Next tym ni muhimu kuwa balanced ktk kuruhusu mijadala kujadiliwa Mjengoni kwa manufaa na maslahi ya Taifa., cyo kwa CCM tuu.

Mh Wenja kaza buti umaarufu wa CDM upo palepale na utaongezeka! mama alikuonea wivu ww na CDM kwa ujumla.
 
Jamani kwa hili mnamuonea spika.Hajatupilia mbali hoja ya Wenje bali amemtaka waziri mhusika aje na majibu ya kueleweka baadaye kuhusu tataizo hilo la umeme.Na ndio maana wapinzani wote walimpigia makofi spika baada ya kutoa uamuzi huo.Nadhani mtoa mada hajamuelewa vizuri spika.

Non-sense!! Waziri anapaswa kuwa na majibu yanayoeleweka wakati wote. Tunamlipa mshahara kwa kodi yetu ili afanye kazi na si vinginevyo.
Angetoa majibu kwanza halafu kama hayatoshelezi ndo options zingine zingeangaliwa... Watu hatuna umeme wala maji kwa siku tatu mfululizo halafu tunaambiwa ngoja ngoja?
 
Hawa wabunge wengine kama huyu Wenje naona wanajitafutia umaarufu wa kijinga. Swala la umeme wa dharura limeshajadiliwa na mitambo imepigwa picha inafungwa Ubungo na Waziri husika kisha sema mpaka December ndio ukali wa mgao utakwisha! Sasa huyu Wenje anataka blah blah za nini?

Wenje hatafuti umaarufu hapa. LAZIMA awasemee wapiga kura wake, period.
Jiji kukosa umeme na maji kwa siku tatu mfululizo sio suala la ukali wa mgao. Hili ni janga. Hatua za kushughulikia janga hili ndo zinazotakiwa sasa... Ukali wa mgano is out of point.
Hongera WENJE KOMAA MWANANGU.
 
Baada ya Mbunge wa Nyamagana kulieleza na kuomba Serikali ieleze mgao huu wa umeme ambao umeyakumba Mijiji ya Mwanza, Arusha, Mbeya na ....kwa kukosa umeme cku 4 na Spika Mama Anna kuwambia serikali walete majibu. Serikali imeleta majibu kwa hapa Mwanza umeme upo, Vipi huko Arusha, Mbeya na .......?
 
Hawa wabunge wengine kama huyu Wenje naona wanajitafutia umaarufu wa kijinga. Swala la umeme wa dharura limeshajadiliwa na mitambo imepigwa picha inafungwa Ubungo na Waziri husika kisha sema mpaka December ndio ukali wa mgao utakwisha! Sasa huyu Wenje anataka blah blah za nini?

Kama hata hicho kiasi kidogo cha umeme kilichokuwapo hakipatikani tena kwanini asiulize na kutaka kupewa majibu kulikoni? Picha za mitambo Ubungo hazizalishi umeme!!! Anyway, waziri atatoa majibu saa kumi jioni.
 
Me nawaaambieni pale bungeni kuna watu wanajiona wao ndio wao kwenye hivyo vyeo ili hali hawajui uwajibikaji wao tatizo kubwa hapa ni serikali kutowajibika kwa kipindi kirefu mkapa nchi ikumbwe na tatizo ndipo itajitokeza na kujifanya ina mikakati imala huku hakuna kitu

Dawa sisi ni Magogoni au Ikulu ya Dodoma period nchi ilisha washinda hawa wana CCM kabisa

Kwani hukumsikia Spika wiki iliyopita aliposema kuwa wabunge wanaumezea uwaziri,
kila mbunge wa CCM anajiona ni waziri mtarajiwa ndo' maana haya yote yanafanyika!
 
Back
Top Bottom