Mali za Yusuf Manji hatarini kukamatwa, kuuzwa

Mtarban

JF-Expert Member
Jan 14, 2015
3,818
5,007
1.jpg

Mali za diwani na mwanachama Wa chama cha ccm ziko hatarini kukamatwa na kuuzwa. ikumbukwe kuwa huyu no miongoni mwa matajiri na wafanyabiashara wakubwa hapa nchini. vipi kwa wafanyabiashara wadogo hali itakuwaje?

Uchumi Wa nchi unaimarika, na unakuwa kwa kasi. hapa kazi tu!

======

Siku moja baada ya mfanyabiashara Yusuf Manji kuhama kwenye jengo la Quality Plaza, uongozi wa kampuni ya udalali ya Yono umesema kinachosubiriwa ni mfanyabiashara huyo kulipa deni au kukamatwa kwa mali zake.

Akizungumza jana, Mwenyekiti wa Bodi ya kampuni hiyo, Stanley Kevela alisema Manji alipewa siku 14 zilizoanza kuhesabiwa tangu Jumamosi ili kulipa deni.

Alisema endapo siku hizo zitamalizika bila kulipwa, mali za mfanyabiashara huyo zitakamatwa ili kufidia deni la Dola 6.1 milioni za Marekani (zaidi ya Sh13 bilioni) anazodaiwa.

Kevela alisema fedha hizo ni gharama ya kupanga kwenye jengo hilo ambalo ni mali ya Mfuko wa Pensheni wa Watumishi wa Umma (PSPF).

Alisema baada ya kukamilika kwa mchakato huo, kampuni italikabidhi jengo hilo kwa PSPF kwa ajili ya shughuli nyingine.

Mfanyabiashara huyo alipotafutwa jana ili kuzungumzia suala hilo, simu yake ya mkononi haikupatikana.

Mkurugenzi wa kampuni ya Yono, Skolastika Kevela alisema kazi ya kuondoa mali za mpangaji kwenye jengo hilo ilikamilika juzi.

“Kampuni zote zimeshaondoa vifaa na milango ya jengo hilo imefungwa kwa kufuli za kampuni yetu. Tutalisimamia jengo hadi tutakapowakabidhi PSPF,” alisema.

Uamuzi wa Manji kuhamishwa kwenye jengo hilo ulitolewa na Mahakama kutokana na kushindwa kulipa kodi ya pango ambapo alipewa masaa 24 ya kuondoa vitu vyake

Chanzo: Mpekuzi
 
Na bado wengine . ..dah! MAMA TANZANIA FANYA KAZI
 
Wamuuze na yeye mwenyewe!!!
Kwani Aliko hawezi kufika dau?
 
naliona taifa likididimia, wafanyabiashara wakubwa kama hawa wakiondoa mitaji yao, au kusimamisha biashara zao, na ndio hivyo hela inavyozidi kuadimika mitaani, au mzungukoni
 
Ukishirikiana na mchwa kama ccm lazima wakutafune tu hakuna namna, ccm ni mchwa
 
Back
Top Bottom