Mali za Yusuf Manji hatarini kukamatwa, kuuzwa

ngoja tusubili kama kawaida ya mtanzania kujivunia future ukishindwa leo utasikia subili 2020 mara 2025
 
Bil 16 ndo zimfilisi mtu mwenye private jet , ?? Mtu anayeendesha kampuni zake kwa zaidi ya bil 1 kwa mwezi umfilisi kwa bil 16?? .. Tuache siasa kuna kitu zaidi ya hicho
Unaongea kinadharia zaidi na si kiuchumi. Kama huamini kuwa mtu akipokwa billion 16 kuwa hatateteleka kiuchumi basi wewe ni mchumi wa upper class.
Punguza Uyanga, mali za Yusuph wewe hazikuhusu.
 
naliona taifa likididimia, wafanyabiashara wakubwa kama hawa wakiondoa mitaji yao, au kusimamisha biashara zao, na ndio hivyo hela inavyozidi kuadimika mitaani, au mzungukoni
Duuh, huyu naye eti akiondoa mtaji wake na na biashara zake mambo yatasimama, hawa sio type ya watu wakuwaonea huruma kabisa, akichuma hapa anawekeza nje , hiyo TZ kwake ni kama shamba tuu.
 
Watu Wa simba kwa tunavyomjua Manji haituingii akili hii habar ya huyu bilionea kufilisiwa kwa hyo pesa madafu.
 
Unaongea kinadharia zaidi na si kiuchumi. Kama huamini kuwa mtu akipokwa billion 16 kuwa hatateteleka kiuchumi basi wewe ni mchumi wa upper class.
Punguza Uyanga, mali za Yusuph wewe hazikuhusu.
N zikipelea itabd wakamatwe mashabiki maan n wao wamechangia kumfilic mzee w watu, kwend taifa bureeee
 
Acheni porojo
Sifurahii yeye kukamatiwa mali zake bali najiuliza kwanini ile misaada anayojidia kuwapa Yanga asilipe madeni yake? Ina maaana kutoa misaada ilhali hujajitosheleza ni kutafuta misifa ama kuna kitu anawinda huko nako?? wacha waisome namba vyema si diwani huyu naam!
 
Huyo kada wao ni tapeli tu hela zake zote kapata kma ndama mutoto wa ngombe tofauti yeye alikua anapiga za serikali
 
kama wadaiwa wa HESLB wanakatwa!!! na yeye alipe , dawa ya deni kulipa
 
Za mwizi ni arobaini!Hawa ndio walio-collude na viongozi wasiowaaminifu wa nchi hii kuifilisi nchi yetu,nadhani sasa siku yake ya arobaini imefika.Unaweza kudanganya mara moja lakini huwezi kudanganya siku zote.

Wakifilisi mali zake wasisahau kiwanda cha kukobolea mpunga alichotupora kilichopo Wami Dakawa, Morogoro.

Kufuru za kuonyesha uwezo wa kifedha zilizofanyika kwenye kiwanda hicho zinatisha.
1.jpg

Mali za diwani na mwanachama Wa chama cha maccm ziko hatarini kukamatwa na kuuzwa. ikumbukwe kuwa huyu no miongoni mwa matajiri na wafanyabiashara wakubwa hapa nchini. vipi kwa wafanyabiashara wadogo hali itakuwaje?

Uchumi Wa nchi unaimarika, na unakuwa kwa kasi. hapa kazi tu!

======

Siku moja baada ya mfanyabiashara Yusuf Manji kuhama kwenye jengo la Quality Plaza, uongozi wa kampuni ya udalali ya Yono umesema kinachosubiriwa ni mfanyabiashara huyo kulipa deni au kukamatwa kwa mali zake.

Akizungumza jana, Mwenyekiti wa Bodi ya kampuni hiyo, Stanley Kevela alisema Manji alipewa siku 14 zilizoanza kuhesabiwa tangu Jumamosi ili kulipa deni.

Alisema endapo siku hizo zitamalizika bila kulipwa, mali za mfanyabiashara huyo zitakamatwa ili kufidia deni la Dola 6.1 milioni za Marekani (zaidi ya Sh13 bilioni) anazodaiwa.

Kevela alisema fedha hizo ni gharama ya kupanga kwenye jengo hilo ambalo ni mali ya Mfuko wa Pensheni wa Watumishi wa Umma (PSPF).

Alisema baada ya kukamilika kwa mchakato huo, kampuni italikabidhi jengo hilo kwa PSPF kwa ajili ya shughuli nyingine.

Mfanyabiashara huyo alipotafutwa jana ili kuzungumzia suala hilo, simu yake ya mkononi haikupatikana.

Mkurugenzi wa kampuni ya Yono, Skolastika Kevela alisema kazi ya kuondoa mali za mpangaji kwenye jengo hilo ilikamilika juzi.

“Kampuni zote zimeshaondoa vifaa na milango ya jengo hilo imefungwa kwa kufuli za kampuni yetu. Tutalisimamia jengo hadi tutakapowakabidhi PSPF,” alisema.

Uamuzi wa Manji kuhamishwa kwenye jengo hilo ulitolewa na Mahakama kutokana na kushindwa kulipa kodi ya pango ambapo alipewa masaa 24 ya kuondoa vitu vyake

Chanzo: Mpekuzi
 
Unaongea kinadharia zaidi na si kiuchumi. Kama huamini kuwa mtu akipokwa billion 16 kuwa hatateteleka kiuchumi basi wewe ni mchumi wa upper class.
Punguza Uyanga, mali za Yusuph wewe hazikuhusu.
Kwa hiyo unaamini jamaa atafilisika kisa kodi ya jengo ? Mtu aliyeajiri wafanyakazi zaidi ya elfu moja , Manji keshapata utajiri mkubwa mno hizo ni hela za kawaida kwake. Ana kampuni nyingi sana imezi diversify mno , ogopa mtu mwenye exclusive right ya kuuza Honda kwa tanzania , kuanzia kuuza mchele ,nenda dakawa Moro wakupe story zake , mwanza ana kiwanda cha samaki (tanperch) vifaa vya kilimo mpaka caterpillars .. jamaa ana biashara kubwa mno sema hazijulikani maana kila kampuni ina jina lake ,,Kwa Hesabu ya kawaida unahisi yanga kaidhamini kwa hela ngapi ? Na mpaka sasa quality group ndo inalipa wachezaji na makocha wa yanga.. Ndo maana mpaka sasa naamini issue siyo kodi tu
 
Billion 16 ni pesa nyingi kwa kushtukizwa tena sana na ujue Manji alianza kupoteza kuanzia kwenye ofukwe wa Coco beach na huko bandarini kufutwa kwa Hati za Kigamboni viwanja alivyonunua kwa bei chee na kutegemea kuja kuipiga serikali kwa mabillioni ya shilingi kutolewa nje na serikali.

Usijethani kile kiwanja kule geza ulole Kigamboni alichokigawa yanga ni kwa kupenda ni kwamba vimemdodea baada ya serikali kutonunua refer statement ya Lukuvi hivyo kwa hasara zote hizi zinavyomuandama ndio anafukarishwa hivyo taratibu.
 
Ukifika uchaguzi wa 2020, JPM atabaki peke yake.

Kawaumiza wengi sana upande wake. Hata wale watu wa karibu na chama.
 
Eti zile milioni 700 zilizokamatwa Dodoma kipindi cha uchaguzi Mkuu wa CCM zilikuwa za Manji ili kumsaidia mgombea ambaye hakuwa Uncle Magu? Yawezekana makovu ya Uchaguzi uliopita bado yanasumbua.
 
Back
Top Bottom