Mali za mmiliki wa hoteli za Naura Spring na Impala kupigwa mnada kufidia madeni ya Wafanyakazi 238 na Benki ya NBC

Deni la NBC halikuwa na bima?

Maana mikopo ya benki siku hizi wanatulazimisha tukatwe hela ya bima wakopaji.. wanasema ikitokea tumefariki ama tumepata kilema bima ilipie deni
Ikitokea hujafa wala kupata kilema hiyo pesa inakwenda wapi
 
Hawa vijana wa Mrema nao viazi , wanashindwaje kutafuta beberu mmoja akawalipia hayo madeni na akaown hizo Kwa mkataba maalumu wa miaka kadhaa kugenerate faida kadhaaa then wakareown Mali Yao tena?

Fundisheni watoto masuala ya pesa , uwekezaji , biashara na jinsi ya kuhandle business negotiations and deals
Mpaka kibo palace imefungwa can imagine. Hali ni mbaya
Ndio na mimi nashangaa, Naura springs peke yake ingeweza kufidia madeni yote hayo na mali nyingine zikabaki, kunaweza kuwa na hujuma kwenye hili
Kabisa mkuu
 
Hapo hamna ushirikina kuna ukubwa jinga tu. Mm mtoto wa kiumeee nasimamia mali za baba angu. Ukweli ukiona baba yako kasema mali asimamie dada yako ujue kaona mbali. Kaona akili kubwa kwa dada yako. Na kwenye kila familia kuna kichwa cha kufanya mambo yawe mepesi.
 
Hatari hii wafanyakazi wanabariki mali zifilisiwe......huku hawajui kesho yao ipoje..
Nani alikwambia kuwa uchungu uliokuwa nao wewe juu ya mali yako ndio uchungu walionao wafanyakazi wako?

Pili watu wana interests tofauti. Mwengine hapo anakwambi anilipeni changu nikajiajiri nimechoka kuajiriwa.
 
Hawa vijana wa Mrema nao viazi , wanashindwaje kutafuta beberu mmoja akawalipia hayo madeni na akaown hizo Kwa mkataba maalumu wa miaka kadhaa kugenerate faida kadhaaa then wakareown Mali Yao tena?

Fundisheni watoto masuala ya pesa , uwekezaji , biashara na jinsi ya kuhandle business negotiations and deals
... tatizo sio wamoja na tumeambiwa "wako wengi" kila mmoja na mama yake. Sio ajabu kati yao humo humo wako wanaofurahia kufilisiwa kwa hizo mali simply "tukose wote". Familia zikishakosa umoja; kukawa na utengano bana yao, kunakuwa na uadui wa hatari kuliko watu baki mliokutana "barabarani".
 
Deni la NBC halikuwa na bima?

Maana mikopo ya benki siku hizi wanatulazimisha tukatwe hela ya bima wakopaji.. wanasema ikitokea tumefariki ama tumepata kilema bima ilipie deni
Nahisi mkopo ulikuwa KWA jina la impala hotels, impala haijafa aliekufa ni mrema
 
Mrema alikua anaingia kazini saa 10 jioni mpka alfajiri ndio anaenda kupumzika,mana anajua pesa nyingi inapatikani jioni asubuhi watu wanacheck out....nlikua naenda kuuza mawe kwa wageni hapo miaka ya 2010
... duh! Jamaa lilikuwa na akili ya hela balaa! Alikuwa anavizia "muda wa hela" baada ya hapo anasepa. Kweli jeshi la mtu mmoja ni hatari kwa afya na usalama wa mali in your absence.
 
Mkuu,kama ni kuzaa nje basi kweli mzee alizaa sana tu,ila naomba nikwambie ukweli kuwa kama kuna wazee wachepukaji wajanja basi mzee mrema alikuwa mjanja hasa,hakuwahi kuwasogeza mahawara wake karibu na mali za kampuni wala za familia,nawajua wanawake kadhaa aliozaa nao mzee,ni kama alikuwa anafanya nao biashara tu! In cash basis,mmoja aliomba tu anunuliwe gari na aongezewe mtaji wa biashara yake ya mtumba,alizaa naye mtoto 1, mwingine amejengewa nyumba ya gharama nafuu tu,wengi walinunuliwa tu vi vitz na ist choka na wakatulia tuli,Neema ndiye aliyekuwa chaguo la mzee kusimamia miradi,tena alimpika mwenyewe na aliujua vyema uwezo wake,randy akashawishiwa na shangazi yake kuwa asikubali dada yake akamate usukani kwani yeye ndiye anayefaa kuongoza kwa kuwa ni mwanaume,wakaenda mahakamani kupinga wosia,na mahakama ikawapa walichotaka,shangazi akaokota alichokitaka na kumwacha jamaa akipambana na mali zake,mali na starehe,mwisho akaelemewa na madeni,siyo tu ya wafanyakazi na nbc,idara ya maji nao wana kesi nae,tra,kuna supplier wadogo wadogo kibao wanadai,siku kila mdeni akienda ku place madai yake pale hela hazitatosha,hata wakiuza na hotel ya impala yote,ila cha kufurahisha ni kuwa dada yake huko aliko anacheka tu,mambo yake yamenyooka kuliko awali!! Karata zake zote dume,ngoja nimalizie kazi nirudi
Dada anaitwa joan. Yeye kapewa ngurdoto na classic. Nae pia Ana case ya staff wa classic,
 
Ikitokea hujafa wala kupata kilema hiyo pesa inakwenda wapi
Inalipia wengine waliokufa au kupata kilema. Bima unalipa kidogo sana hivyo mchanganyiko wa ulicholipa na wengine walicholipa ndicho hufidia janga kwa wachache watakaopata janga.
 
Dada anaitwa joan. Yeye kapewa ngurdoto na classic. Nae pia Ana case ya staff wa classic,
... huyu Mrema alikuwa na hoteli ngapi huyu bepari ? Mara Naura, Impala, Ngurdoto, Classic, jamaa alikuwa vizuri kumbe.
 
masikini siku zote hufurahia tajiri akidondoka mkuu. Acha chuki mkuu
hapana kuna watu wanadai haki zao miaka mingi wanahangaika, nenda rudi mpaka wanakosa nauli ya kufuatilia haki zao, mpaka wanashindwa kuhudumia familia zao kisa kuna kesi, wamechoshwa vya kutosha,
mimi ni mpenda haki sipendi kuona haki ya mnyonge inaburuzwa na tajiri.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom