Mali za marehemu sharo milionea zapatikana, watuhumiwa mbaroni

R.B

JF-Expert Member
May 10, 2012
6,296
2,564
[h=3][/h]


[h=3][/h]
[h=1][/h]


Baadhi ya vitu vya marehemu Sharo milionea vilivyokamatwa baada ya msako mkali baina ya Polisi na wananchi wa Kijiji Songa Kibaoni.
Na Mashaka Mhando,Tanga
WATU wanaosadikiwa kuiba vitu vya marehemu Hussein Mkiety maarufu kwa jina la 'Sharo Milionea' aliyefariki kwa ajali ya gari katika kijiji cha Songa Kibaoni wilayani Muheza Novemba 26 mwaka huu, wamesalimisha baadhi ya vitu hivyo kwa mwenyekiti wa Kijiji hicho huku wakiendelea kuishi mafichoni kuogopa kutiwa mbaroni.
Watu hao wamesalimisha vitu hivyo baada ya Mkuu wa wilaya ya Muheza Subira Mgalu ambaye ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama kuwatangazia kwamba wale wote waliomwibia marehemu watasakwa na kuchukuliwa hatua za kisheria kufutia kitendo walichokifanya kutokuwa cha kiungwana.
Mkuu huyo pamoja na jeshi la polisi wilayani humo waliendesha msako juzi usiku lakini hawakuweza kuwakuta watu baada ya kuzihama nyumba zao kuogopa kutiwa mbaroni na mkuu huyo kuwalazimsha baadhi ya familia walizozikuta kuendesha zoezi la kuwataja watu wanaohofiwa kwamba huenda watakuwa wamchukua vitu hivyo.
Kamanda wa polisi mkoani Tanga ACP Constatine Masawe, aliwaeleza waandishi wa habari ofisini kwake kuwa, usiku wa kuamkia juzi mwenyekiti wa kijiji hicho Abdi Zawadi alipelekewa vifaa mbalimbali ikiwemo nguo ambazo marehemu alikuwa amezivaa pamoja na spea tairi ambalo waliling'oa na kutokomea porini.

Kamanda huyo alitaja vitu vilivyokabidhiwa kwa mwenyekiti huyo kuwa ni pamoja na begi lake lililokuwa na 'viwaro' nguo zake, betri ya gari hilo lililokuwa na namba T 478 BVR aina ya Toyota Harrier, saa yake ya mkononi, simu yake aina ya Blackberry na redio ya gari iliyokuwa pia imeng'olewa na wezi hao.
Kamanda huyo alisema vitu hivyo vilipelekwa na mtu mmoja ambaye kwasasa jeshi hilo linashindwa kumtaja jina lake kwa vile alijitambulisha kwamba ana undugu na wezi hao ambao walimpa vitu hivyo avipeleke kwa uongozi wa kijiji hicho hatua ambayo alidai kwamba wanafanya uchunguzi ili kuwatia nguvuni wale wote waliohusika na tukio hilo.
Alisema waliweka mtego baada ya kusikia kwamba kuna mwizi mmoja wapo anaitafutia mteja simu ya mkononi ya marehemu lakini wakati wameweka mtego huo kijana huyo alipokuwa akijadiliana bei na mtu waliyemweka, alibaini na alipompa mkononi alikimbia vichakani kuogopa kukamatwa.
Kamanda huyo aliwashukuru baadhi ya wananchi wa kijiji hicho pamoja na Mkuu wa wilaya kuhakikisha wanashirikiana na jeshi hilo ili kuwabaini na kuwakamata wote waliohusika katika tukio hilo ambalo limetokea huku wananchi kadhaa wakiomboleza kifo cha msanii huyo ambaye alizikwa kijijini kwao Lusanga wilayani Muheza juzi.
Katika hatua nyingine kamanda huyo alisema katika matukio ya ajali yaliyotokea mwezi huu wa Novemba jumla ya ajali 10 zilitokea ambazo zimesababisha vifo ni 7 na zilizosababisha watu kujeruhiwa ni tatu, kati ya hizo watu 12 walipoteza maisha na wengine wanane walijeruhiwa.
Kamanda Masawe alisema jumla ya makosa 2,365 yalitendeka na kupigwa faini iliyosababisha serikali kujiingiza kiasi cha sh. 70,950,000 hatua ambayo kamnada huyo alisema haioneshi kwamba watumiaji barabara wamekuwa wakifuata wakitii sheria za usalama barabarani.
 

Chiya Chibi

JF-Expert Member
Jul 6, 2011
484
110
Hiv hao wez walimkuta marehem nje au ndan ya gar, isije ikawa walimmalizia ili kuchukua vitu vyake kirahisi?! Uchunguz uendelee zaidi!!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom