Mali za CCM vs Zile za Serikali...

Maneno yako yanatia hasira lakini ndo ukweli uliopo. Ndo maana nasema haya mambo ya upinzani ni kiini macho tu, and in the process, tunapoteza pesa nyingi sana, muda, nguvu kazi na akili kwenye ujenzi wa Taifa. Something is seriously wrong.

Sasa Mwenyekiti wa CCM anaposema zikahakikiwe, yeye anadhani zinaweza kuwa mali za nani? Au anahisi watu binafsi wamekwapua mali hizo?

Mimi bado nina imani kuwa mali nyingi tu za ccm ni za wananchi wote. Miaka ya nyuma, kila mtu alichangia chama, whether kwa hiari au kulazimishwa, watu walilipa karo za uanachama na michango mingine mingi tu.

Sasa tukisema mali za ccm ni mali za serikali and vice versa, ni kosa kubwa kabisa.
Lakini wapinzani unawaonea tu, wale pia wanatafuta kama mtu yeyote awaye. Mfumo ulitoa fulsa kwa wasio ndani ya mfumo au waliosahaulika sio kukosoa kama katiba inavyosema. Serikali wenyewe hawataki kukosolewa hivyo utaona kwanini wapinzani wanaonekana ni wahaini. Hivyo haya mambo yazoee tu otherwise utajiumiza bure. Kama unapata mkate wako mshukuru mungu. Hakuna njia nyingine, kumbuka majeshi hulinda watawala na wanakinga dhidi ya mahakama, wameziba huku na kule katikati vacuum na hapo ndo tulipo. Usipotaka kukubali haya utavunjika maguu.
Heri mimi sijasema.
 
Back
Top Bottom