Mali za CCM vs Zile za Serikali...

jmushi1

JF-Expert Member
Nov 2, 2007
23,943
2,000
Nadhani CCM ikija kuondolewa madarakani kutakuwa na mgogoro kwenye hili suala.Kama kuna wenye insight si vibaya wakatuelemisha kuhusu hili.Kwasababu kuna wakati nasikia "hiki ni cha serikali",halafu hapo hapo unaambiwa ni cha ccm.Kwa mfano TBC,CCM ikiondolewa madarakani,serikali mpya itamiliki chombo hicho ama kitabaki kwa magamba?Mifano ni mingi tu,je utofauti wa mali za chama tawala vs mali za serikali(ambazo wakiondoka madarakani wataziacha kwa serikali mpya) ni upi?@Ritz ndiye alisema TBC ni mali ya ccm,is that true?if so,what else?and what isn't?

quote_icon.png
By jmushi1
Kwani ccm ina gazeti, radio na tv?Ritz said:
Magazeti wanayo Uhuru na Mzalendo na radio wanayo radio Uhuru.

MFUKUZI

JF-Expert Member
Mar 1, 2011
934
1,000
Nadhani CCM ikija kuondolewa madarakani kutakuwa na mgogoro kwenye hili suala.Kama kuna wenye insight si vibaya wakatuelemisha kuhusu hili.Kwasababu kuna wakati nasikia "hiki ni cha serikali",halafu hapo hapo unaambiwa ni cha ccm.Kwa mfano TBC,CCM ikiondolewa madarakani,serikali mpya itamiliki chombo hicho ama kitabaki kwa magamba?Mifano ni mingi tu,je utofauti wa mali za chama tawala vs mali za serikali(ambazo wakiondoka madarakani wataziacha kwa serikali mpya) ni upi?@Ritz ndiye alisema TBC ni mali ya ccm,is that true?if so,what else?and what isn't?

quote_icon.png
By jmushi1
Kwani ccm ina gazeti, radio na tv?
Naunga mkono hoja!!!.... Mimi nalia na viwanja vyetu wa michezo nchi nzima kama kiwanja cha Jamhuri Morogoro na Dodoma, Samora Iringa, Majimaji Ruvuma, Kirumba Mwanza, Sheikh Amri Abeid Arusha, Mkwakwani Tanga na nk. Kwa kweli hivi viwanja CCM imepora viwanja vya umma. Hivi vilijengwa na wananchi kujitolea kwa kusomba mawe na mchanga na nguvu kazi nyingine kipindi cha chama kimoja.... Mimi nadhani CCM watumie busara kwa hivi viwanja wavikabidhi mapema kwa Serikali ili iweze kuendeleza michezo nchini...
 
The Boss

JF-Expert Member
Aug 18, 2009
44,136
2,000
TBC ni mali ya serikali

sawa na Daily News na HabariLEO...

CCM wanamiliki redio Uhuru na magazeti ya Uhuru na Mzalendo...
 
jmushi1

JF-Expert Member
Nov 2, 2007
23,943
2,000
Naunga mkono hoja!!!.... Mimi nalia na viwanja vyetu wa michezo nchi nzima kama kiwanja cha Jamhuri Morogoro na Dodoma, Samora Iringa, Majimaji Ruvuma, Kirumba Mwanza, Sheikh Amri Abeid Arusha, Mkwakwani Tanga na nk. Kwa kweli hivi viwanja CCM imepora viwanja vya umma. Hivi vilijengwa na wananchi kujitolea kwa kusomba mawe na mchanga na nguvu kazi nyingine kipindi cha chama kimoja.... Mimi nadhani CCM watumie busara kwa hivi viwanja wavikabidhi mapema kwa Serikali ili iweze kuendeleza michezo nchini...
Nakubali hili ni lakutupiwa macho.Ni muhimu wakaanza kulifanyia kazi.
 
sukankanwa

Member
Nov 20, 2013
92
0
mkuu umesahau uwanja wa sokoine mbeya nao unamilikiwa na ccm wakati ulijengwa na wananchi,siku wakijaondoka madarakani sijui bado zitakuwa mali zao,kibaya zaidi hivyo viwanja hawavifanyii malekebisho wakati wanaingiza pesa sijui wanatumia kwenye kampeni.
 
bendaki

JF-Expert Member
Feb 5, 2013
952
250
Itakuwepo haja ya kwenda mbali zaidi kisheria. Mali nyingine kama viwanja vya majengo na mejengo walivipata enzi za chama kimoja mgongoni mwa serikali, ambapo chama kilikaa kama taasisi ya umma. Hii ikiimanisha kuwa zilikuwa ni Mali za watanzania wote. Kwa sheria ya vyama vingi kunatakiwa kuwepo sheria ya utaratibu wa mali hizo kuendelea kuwa za watanzania wote mil. 45 na si wanaCCM tu mil. 2.
 
Mlayjr

JF-Expert Member
May 7, 2013
399
250
Mwisho wa haya wote ni 2O15, tutafilisi wezi wote, kuanzia wenye viti wao wa serikali za mitaa mpaka raisi wao
 
jmushi1

JF-Expert Member
Nov 2, 2007
23,943
2,000
Itakuwepo haja ya kwenda mbali zaidi kisheria. Mali nyingine kama viwanja vya majengo na mejengo walivipata enzi za chama kimoja mgongoni mwa serikali, ambapo chama kilikaa kama taasisi ya umma. Hii ikiimanisha kuwa zilikuwa ni Mali za watanzania wote. Kwa sheria ya vyama vingi kunatakiwa kuwepo sheria ya utaratibu wa mali hizo kuendelea kuwa za watanzania wote mil. 45 na si wanaCCM tu mil. 2.
Good point,inatakiwa liwekwe wazi na lifayiwe kazi.Mali za umma zitenganishwe n ccm.
 
vutakamba

JF-Expert Member
Apr 2, 2012
201
250
Naunga mkono hoja!!!.... Mimi nalia na viwanja vyetu wa michezo nchi nzima kama kiwanja cha Jamhuri Morogoro na Dodoma, Samora Iringa, Majimaji Ruvuma, Kirumba Mwanza, Sheikh Amri Abeid Arusha, Mkwakwani Tanga na nk. Kwa kweli hivi viwanja CCM imepora viwanja vya umma. Hivi vilijengwa na wananchi kujitolea kwa kusomba mawe na mchanga na nguvu kazi nyingine kipindi cha chama kimoja.... Mimi nadhani CCM watumie busara kwa hivi viwanja wavikabidhi mapema kwa Serikali ili iweze kuendeleza michezo nchini...
Nashauri kuwe na mjadala mpana kuhusu mali zilizopatikana wakati wa chama kimoja, ambazo zilitokana na nguvu za wananchi wote hata ambao hawakuwa wanachama wa TANU au CCM.
Wananchi walijitolea na kujenga miradi mbali mbali ambayo ni pamoja na viwanja vya michezo, kwa njia ya kujitolea na CCM haikugharamia kiasi chochote.
Mwanzoni viwanja hivi vya michezo vilikuwa chini ya Halmashauri za miji husika mahali ambapo ni neutral na kila mtanzania alifaidika, bila kujali ni wa itikadi gani. Lakini CCM kwa ubabe baadaye walivichukua viwanja hivi na kuwa chini ya miliki yao.
Viwanja hivi havifanyiwi ukarabati wowote, viko ktk hali mbaya sana kimazingira, na kila mwaka wanapandisha kodi, kwa kujilinganisha na nyumba za watu binafsi ambao wengi wao wamekopa ktk mabenki, ambapo wanatakiwa kurudisha mikopo pamoja na riba. Tofauti na CCM ambao walichukua bure viwanja vya michezo na wanaendelea kukusanya kodi kwa faida yao.
Naunga mkono kuwa kwa kuwa tuko ktk mfumo wa vyama vingi, ambapo hakuna ajuae kwa uhakika kwamba ktk miaka ijayo ni chama gani kitakuwa madarakani, ni busara kwa CCM kuanza kuzoea mazingira ya kutathmini ni miradi gani ambayowao kama chama cha siasa hawakugharamia moja kwa moja, na waaanze kurudisha miradi hii kwenye usimamizi wa idara za serikali, ambazo ndizo zenye mamlaka ya kusimamaia maslahi ya kila mwananchi.
Ni suala la kujitambua tu, kuwa Tanzania haitaendelea kuwa chini ya CCM milele, na kuwa kuna siku mabadiliko tunayoyatamani yatafika na mali zilizochukuliwa kinyemela na kwa ubabe wa CCM zitarudishwa ktk mikono ya chombo cha serikali. Kama ilivyotokea Kenya. Baada ya KANU kuondolewa madarakani jengo kubwa na refu la Kenyatta conference Centre lilirudishwa serikalini.
Nashauri CCM tusiwe wapofu wa kuona dunia inayozunguka na kubadilika. Hakika hakuna jiwe lililosimama daima.
 
Mafwi Munda

JF-Expert Member
Nov 30, 2017
1,752
2,000
Kwani CCM wanampango wa kuondoka madarakani?!
Sidhani kama mnajadili kitu sahihi. Au ndio tumeambiwa ni ndoto hizi.
 
jmushi1

JF-Expert Member
Nov 2, 2007
23,943
2,000
Kwani CCM wanampango wa kuondoka madarakani?!
Sidhani kama mnajadili kitu sahihi. Au ndio tumeambiwa ni ndoto hizi.
Haya mkuu, hata kama si ndoto, wewe unadhani ni sahihi? Kwamfano sasa hivi kuna tume ya ccm imeanzishwa na mwenyekiti wao kufuatilia mali za ccm.

Kumbuka utofauti uliopo!

  • Mali za chama siyo za serikali and vice versa
  • Mali za serikali ni mali za wananchi
  • Mali za ccm ambazo zilikuwa ni mali za serikali, pia siyo mali za wananchi, bali wanachama wa ccm.
 
Mafwi Munda

JF-Expert Member
Nov 30, 2017
1,752
2,000
Haya mkuu, hata kama si ndoto, wewe unadhani ni sahihi? Kwamfano sasa hivi kuna tume ya ccm imeanzishwa na mwenyekiti wao kufuatilia mali za ccm.

Kumbuka utofauti uliopo!

  • Mali za chama siyo za serikali and vice versa
  • Mali za serikali ni mali za wananchi
  • Mali za ccm ambazo zilikuwa ni mali za serikali, pia siyo mali za wananchi, bali wanachama wa ccm.
Usijali sana wanasema tushukuru tu kwa hali yoyote iwayo mkuu. Hata vya serikali humilikiwa na ccm. Sasa jiulize ukishavifahamu vya serikali ni vipi na vya ccm ni vipi, wakati CCM ndio watawala na wanamiliki kila kitu, utampa nani mali ya serikali aitizame au akutunzie?! CCM ndio wamiliki wa vyote, na kwa kukumbusha tu. HAWANA mpango wa kuondoka kabisa. Hivyo zoea hivi. Mali ya serikali ni mali ya ccm, na mali ya ccm ni mali ya ccm.
Heri mimi sijasema.
 
Maneno yako yanatia hasira lakini ndo ukweli uliopo. Ndo maana nasema haya mambo ya upinzani ni kiini macho tu, and in the process, tunapoteza pesa nyingi sana, muda, nguvu kazi na akili kwenye ujenzi wa Taifa. Something is seriously wrong.

Sasa Mwenyekiti wa CCM anaposema zikahakikiwe, yeye anadhani zinaweza kuwa mali za nani? Au anahisi watu binafsi wamekwapua mali hizo?

Mimi bado nina imani kuwa mali nyingi tu za ccm ni za wananchi wote. Miaka ya nyuma, kila mtu alichangia chama, whether kwa hiari au kulazimishwa, watu walilipa karo za uanachama na michango mingine mingi tu.

Sasa tukisema mali za ccm ni mali za serikali and vice versa, ni kosa kubwa kabisa.
 
Hahaha pole kwa hasira. Hao ccm wana entitlement ya mali za serikali na huwezi kuzitenganisha hivyo zoea tu. Hakuna demarcation kati ya ccm na serikali kwa sasa. Serikali ni ccm na ccm ni serikali. Hii ndiyo Tanzania ndugu yangu jitahidi kupunguza hasira usije ukajiumiza bure na hayo mambo.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom