Mali za Bilionea Mrema zauzwa bilioni 2.6 kulipa madeni, yamo mahekalu, familia yadondosha chozi

Nadhani sisi waafrika tujifunze jambo. Tuandae mfumo wa kuendeleza biashara hata baada ya waanzilishi kufariki. Kwanini makampuni ya wazungu, waarabu, wahindi yanasonga mbele baada ya mmiliki kufa lakini kwetu imekuwa mtihani?
Yaani mmiliki akufariki ni ugomvi mwanzo mwisho wakigombea kugawana mali na sio kuendeleza.
Hili deni iwapo wangeamua kutulia na kuwa na mpango wa kulilipa wangeweza ila ndio hivyo wote walikuwa wanawaza kuchuma tu na kuweka kwenye mifuko binafsi. Sisi ni wabinafsi sana.
Hili lilitaka kutokea kwa Mengi pia.
Ugomvi unakuja sababu ya mgongano wa maslahi😂!!!

Unakuta marehemu alikuwa hana ubaguzi wa ndugu ila kuna kundi la ndugu lilikuwa linaumia wenzao flani kunufaika na mali za huyo ndugu Don!

Hivyo akifa wanataka kuleta utata kuwa flani na flani hamuhusiki
 
Wanadai billion 1.3

Wanauza viwanja 16,17,18 19,20,21,22 na 23 na kupata billion 2.65

Kwa nini wasitafute viwanja kadhaa vitakavyo leta pesa billion 1.6 wakalipa madeni Mali zingine wakawaachiwa wana Family.
Inaelekea hii familia pasua sana

Ova
 
Bado familia ina mali nyingi wanalia lia nini? Wangefilisiwa kabisa wasibaki hata na baiskeli si wangekufa.
Kwa hyo ukiwa na milion mia tatu ukapoteza milion Kumi hautaumia ndugu. Chako ni chako wanahak ya Kulia na kusikitika Kwan wanepoteza sehemu ya Mal yao
 
Kwa hyo ukiwa na milion mia tatu ukapoteza milion Kumi hautaumia ndugu. Chako ni chako wanahak ya Kulia na kusikitika Kwan wanepoteza sehemu ya Mal yao
Mkuu kumbuka hawadhulumiwi bali wanalipa stahiki za wafanyakazi ambao hawakulipwa muda mrefu.

So they are paying what is due.
 
Bora mtu uwekeze kwenye fixed diposit au bond za serikali maana kuendesha kampuni kikwetu kwetu bado sana.JPM alimponda sana abood kwa kufanya godonw kiwanda lakini kiukweli kuendesha kampuni si lele mama.
Mh! Haujaongea kinyume kweli!
"Kufanya godown kuwa kiwanda" au kufanya kiwanda kuwa godown?
 
Marehemu anaondoka na mali zake! Bora hawa madogo wauze hizo hoteli ili wapate fedha wafanye biashara wanayoiweza. Watakuja kufilisika washindwe kununua hata ndala wakiendelea kuzifuga hizo hoteli.
 
Kwa kuangalia mkaa wa hizi Mali za Mrema utagundua kuwa pamoja na watoto kuwa na makosa lakini kimsingi marehemu alianza kuboronga yeye.

Kumekuwa na desturi ya matajiri wengi wa kiswahili kutowaamini watoto wao hivyo kushindwa kuwaachia miradi mapema waiendeshe.
Inakuwa maradufu zaidi inapofika Kwa Wazee wa kichaga,anakomaa na miradi yake mpaka akiwa ICU.
Hicho ndio haswa kilichotokea Kwa huyu mzee, kona kona zote za kuendesha mahotel yake alizijua mwenyewe
 
8 Reactions
Reply
Back
Top Bottom