Jembe Jembe
JF-Expert Member
- Jun 9, 2016
- 749
- 1,797
Mali za Hayati Bilionea Faustine Merau Mrema Mkazi wa jiji la Arusha aliyefariki mwaka 2018, zimeuzwa Kwa amri ya mahakama ili kufidia madai ya wafanyakazi wa hoteli ya Impala na Naura yaliyotokana na malimbikizo ya mishahara kiasi cha zaidi ya shilingi bilioni 1.3.
Amri ya uuzwaji wa Mali hizo ilitolewa na mahakama kuu Kanda ya Arusha Masjala ndogo ya kazi na Msajili wa Mahakama hiyo,Ruth Masama ambapo mahakama hiyo ilimwagiza Dalali wa mahakama kampuni ya Nutmeg Actioneers Property kuuza Mali hizo kabla ya oktoba 15 mwaka huu.
Mali zilizouzwa ni pamoja na kiwanja kitalu namba 16,17,18 19, 20, 21, 22 na 23 vilivyopo eneo la Uzunguni jijini Arusha na kuwezesha kupatikana Kwa kiasi cha Sh. bilioni 2.65.
Akiuza Mali hizo katika mnada wa hadhara Mapema Jana mkurugenzi wa kampuni hiyo ya udalali, Boniface Buberwa alimtangaza mshindi wa mnada huo kuwa ni Edmund Robert Koka ambaye ameweza kufikisha dau la thamani ya Sh. bilioni 2.65 lililoshindwa kufikiwa na washindani wengine wapatao Tisa walioshiriki mnada huo.
Alisema kuwa mnada huo umefanyika Kwa kufuata taratibu zote za kisheria kupitia ushindani wa Bei na Mshindi aliweza kufikia kiasi hicho Cha fedha kiasi ambacho hakikufikiwa na mshindani yoyote katika mnada huo.
Mkurugenzi wa kampuni ya udalali, Bonface Buberwa alisema kuwa ushindani katika mnada huo ulikuwa ni mkubwa kwani mshindi wa pili alifikisha dau la sh, bilioni 2.6 na Mshindi wa tatu alifikisha dau la sh bilioni 2.5
"Mshindi wetu ni Edmund Koka ambaye amefikishwa kiasi cha sh, bilioni 2.65 hivyo atapaswa kulipa asilimia 25 Leo na baada ya siku 14 anatakiwa awe amelipa fedha yote naniwapo ataahindwa atapewa mshindi wa pili naye akishindwa atapewa mshindi wa tatu na yeye akishindwa mnada utarudiwa" alisema Buberwa
Kwa upande wake mnunuzi wa Mali hizo Edmund Koka alishukuru kupata bahati hiyo kwani ushindani ulikuwa mkali na yeye ndio aliiibuka mshindi Kwa kutoa dau la sh, Bilioni 2.65 na atapaswa kulipa asilimia 25 leo na kiasi kitakachobaki atakitoa baada ya wiki mbili kama sheria ya mnada inavyopaswa
"Kwa kweli namshukuru mungu Kwa kupata bahati ya ushindi, ushindani ulikuwa mkubwa kilichopo Mbele yetu Kwa Sasa ni kwenda kuingiza fedha hizo benki ili mambo mengine yaweze kuendelea" alisema Koka
Zoezi la uuzwaji wa Mali hizo lilishuhudiwa pia na familia ya Marehemu akiwemo Mtoto wa marehemu Randy Mrema ambaye alikuwa mkurugenzi wa hotel za Impala na Naura springs dada wa marehemu, Peragia Mrema ambaye alionekana kutokwa machozi asiamini kinachoendelea.
Kuuzwa Kwa Mali hizo ni wazi kwamba wafanyakazi zaidi ya 200 wanaodai malimbikizo Yao wanakwenda kuogelea mamilioni ya fedha na hivyo kuondoka na shida ndogo ndogo Iliyokuwa zikiwakabili baada ya kusotea malipo yao kwa muda mrefu.
Kesi hiyo ilifunguliwa katika mahakama hiyo na afisa kazi mfawidhi Mkoa wa Arusha Emmanuel Mweta baada ya wafanyakazi hao kulalamika katika ofisi hiyo kutoliowa mishahara tao Kwa muda mrefu huku jitihada mbalimbali zilifanyika juu ya madai hai bila mafanikio Hadi suala hilo lilipofikishwa mahakamani.
Kwa upande wake mwenyekiti wa wafanyakazi hao, Jacob Joel alisema kwamba wanaishukuru Serikali kupitia mahakama Kwa kuhakikisha wanapata haki zao
Baadhi ya wafanyakazi hao Queen Naftari na Magreth Ayo Kwa upande wao waliishukuru Serikali kupitia mahakama Kwa kusimamia haki zao kwa kuwa wameteseka Kwa muda mrefu kupigania haki zao na Wana Imani kubwa na Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan.
Mwisho.
Picha Baadhi ya majengo yaliyokuwa ya Bilionea Hayati Mrema baada ya kuuzwa Jana, familia yatokwa na machozi, mwakilishi wa Tajiri aliyenunua aongea.