Phillipo Bukililo
JF-Expert Member
- Dec 29, 2015
- 18,487
- 13,612
Neno analolisema mzee aliyekuzidi umri siku zote ni la kusikilizwa kwa umakini. Nimewahi kumsikia mzee mmoja akisema kuwa mali ya dhuluma huwa haimfikii mjukuu. Alimaanisha kuwa kisicho haki kinapochumwa na mtu ni sawa na yule mtu kuwashikia wenye mali, anaweza kukaa na hiyo riziki isiyokuwa yake kwa miaka mingi lakini ipo siku mali hiyo itawarudia wale wenye haki ya kuimiliki.
Huwa nawaangalia matajiri ambao wanaibuka kadri ambavyo awamu za uongozi zinavyokuja na kuondoka. Waliibuka matajiri wa awamu ya kwanza, ilipoondoka na kuja ile ya pili wale walioshi kwa dhuluma katika awamu ya kwanza wakafilisika. Ikaibuka awamu ya pili, na wale walioshi kwa kuwadhulumu na kuwaona walio wengi katika awamu ya kwanza, ikawa ni zamu yao kufilisika. Ikaja awamu ya tatu na matajiri wake, wale waliotesa katika awamu ya pili wakaanza kuingia katika maisha ya dhiki tofauti na ile miaka kumi ya starehe waliyoizoea. Awamu ya nne ikaja, wakaibuka matajiri "wazee wa vimemo", wakati wale matajiri wa awamu ya tatu wakizidi kufilisika. Sasa tunayo awamu ya tano, ambayo na yenyewe itakuwa na matajiri wake wa miaka kumi.
Lakini wapo wale matajiri ambao wanaishi kwa amani katika awamu zote bila ya kuhofia mamlaka za kiserikali kuja kutaifisha mali zao. Utajiri wao unawafikia wajukuu zao, ambao wanakua wakifurahia mali iliyopatikana kwa amani. Mali ya dhuluma hufurahiwa na watoto, huwa haiwezi kumfikia mjukuu kwa sababu aliyedhulumu ni kama vile amevaa nguo ya kuazima, kuna siku mwenye mali atakuja kuifuata.
Na haya ndio maisha ya kiafrika. Wapambe wa serikali zinazokuwa madarakani wanafurahia maisha wakifahamu fika kuwa uongozi unaofuatia sio mzuri kwao. Wapo matajiri wachache wenye kutokea jasho walichonacho, hawa mali zao zinarithiwa mpaka na vitukuu lakini wapo wengi ambao utajiri wao hauwafikii wajukuu zao kwa sababu walichonacho ni dhuluma, kimepatikana huku wanyonge wakitoa machozi, wanyonge wakiwa na vinyongo mioyoni. Maneno ya watu wazima kwa maana ya Baba zetu na Mama zetu yamejaa busara sana. Mali ya dhuluma haimfikii mjukuu.