Mali ya bil. 2/- yauzwa kwa mil. 800/-

Mugishagwe

JF-Expert Member
Apr 28, 2006
300
58
na Mwandishi Wetu


UUZAJI wa mali za umma unazidi kuzua maswali, ambapo sasa imebainika kuwapo mali iliyouzwa kwa thamani ndogo, licha ya kuwapo mnunuzi aliyekuwa tayari kutoa fedha nyingi.


Mali hiyo ya umma, ni kilichokuwa Kitengo cha Uchapaji Kijitonyama (KPU), chini ya Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL). Mali hiyo, pamoja na nyingine kadhaa, ilikuwa imewekwa chini ya Kampuni ya Simu 2000 Limited, kwa ajili ya mauzo.


Rekodi za umma zinaonyesha kwamba, thamani halisi ya KPU ni sh bilioni 1.954, kati ya hizo, thamani ya ardhi na majengo bila vifaa, ilikuwa sh bilioni 1.6, lakini ajabu ni kwamba, pamoja na mashine zilizopo, vyote viliuzwa kwa sh milioni 800 tu.


Ziliuzwa kwa thamani hiyo, baada ya uongozi wa Simu 2000 Limited, nalo shirika la umma, kuomba kibali Wizara ya Fedha, kuuza mali hiyo chini ya thamani yake.


"Thamani ya mali hiyo ya umma ni kubwa, karibu sh bilioni 2, iweje sasa mali hiyo iuzwe kwa sh milioni 800 tu? Na ni kwa nini hakuna mkataba rasmi wa mauziano ya mali hiyo ya umma?


"Ni vigumu kupata jibu la maswali haya. Kuna upungufu mkubwa, tena wa makusudi katika uuzaji wa mali za umma nchini. Haiingii akilini, kwa nini mkurugenzi mtendaji wa shirika la umma ameuza mali ya umma nje ya taratibu wazi na zinazokubalika," kilihoji chanzo chetu cha habari.


KPU sasa imeuzwa kwa ZEK Group, baada ya mazungumzo yaliyofanyika ofisini ZEK, kati ya uongozi wake na ule wa Simu 2000 Limited, na mawasiliano ya barua kwa mara kadhaa, ikakubaliwa kwamba, ZEK walipe kwanza sh milioni 150, halafu sh milioni 250, zote ndani ya mwezi mmoja.


Ilikuwa pia kwamba, baada ya kulipa kiasi hicho cha fedha, ambacho ni nusu ya bei waliyokubaliana, ZEK wakabidhiwe mali kwa ajili ya mipango ya awali ya kuiendeleza, kisha kiasi kingine kilipwe Desemba 2004.


Hata hivyo, mnunuzi huyo hakulipa salio katika muda uliokubaliwa, kwani malipo ya mwisho alifanya Aprili mwaka huu, yaani kipindi cha miaka miwili tangu akabidhiwe mali yenyewe.


Mauzo hayo yalifanyika kwa jinsi hiyo, licha ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, katika barua yake ya Januari 16, 2003, kwenda kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Simu 2000 Limited, iliomba iuziwe majengo hayo yaliyopo kitalu namba 717/3, mali ya umma, na wizara ikiwa inashughulikia zaidi masilahi ya umma.


Ikiwa imesainiwa na Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, W.N. Magoi, ilisema iko tayari kununua eneo na majengo hayo, na ikaomba ipewe nafasi, ili ibadilishe eneo hilo litumike kwa ajili ya kuwa Makao Makuu ya Kikosi cha Zimamoto na Uokoaji.


Kadhalika, Katibu Mkuu alieleza kwamba amewasilisha barua hiyo kutokana na tangazo/notisi ambayo Simu 2000 Limited ilichapisha kwenye gazeti la serikali la Daily News, toleo la Januari 15, 2003, ikimaanisha wizara iliandika barua hiyo siku moja tu tangu notisi hiyo itolewe.
Wizara iliieleza Simu 2000 Limited kwamba, iko tayari kutoa sh 1,957,705,000 kwa ajili ya kununua vitu vyote hivyo. Barua hiyo ilipokewa Simu 2000 Limited Januari 17, 2003, lakini hakuna maelezo zaidi juu ya kilichoendelea, wala sababu za kukataa kuiuzia wizara, inayotumikia umma, kwa kiasi kikubwa cha fedha, iliyokuwa tayari kutoa.


Kumekuwa na malalamiko mbalimbali kuhusu mauzo ya mali za umma, ikiwa ni pamoja na kubinafsisha mashirika nyeti kama yanayotoa huduma ya maji. Serikali ilikuja kufuta mkataba wa kubinafsisha huduma ya maji jijini Dar es Salaam, ambao uliingiwa huku wananchi wakilalamika na kuonya. Mashirika nyeti kama Bandari na Reli nayo yamekuwa yakipigiwa kelele yasiuzwe wala kubinafsishwa.


Aidha, mauzo mengine yamekuwa yakifanywa kwa bei ndogo, tofauti na ile ya soko. Mengine yamefanywa kwa kuzipa kampuni kubwa na kuacha walalahoi, kati ya hizo ni mashamba makubwa ya mpunga ya Mbarali na Kapunga, ambapo wananchi zaidi ya 5,000 wanaendelea kuyalilia.
 
Huu ndiyo wakati mwafaka wa vyama vya upinzani(kama vingekuwepo) kuonyesha nguvu yake. Vijifunze kutoka Georgia, Ukrain, Serbia, n.k.
Hakuna nguvu inayoizidi nguvu ya umma. Wananchi wakipata viongozi wazuri
wa vyama vya upinzani(vyenye nia njema na TZ) wanaweza wakabadilisha hata mikataba iliyoshindikana kama ya IPTL, SONGAS na mingineyo kama hiyo.
Vyama vya upinzani unganeni muiokoe nchi kutoka kwenye mikono ya Chukua Chako Mapema(CCM). Msipofanyahivyo kaburi zenu na za CCM zitapigwa viboko na vizazi vijavyo.
WAKATI WA VYAMA VYA UPINZANI KUUNGANA NA KUUZIKA UKOLONI NA UNYAMA WA CCM NI HUU.
 
Na huyu Basil yiko kwenye Serikali ya kasi hii .Iko kazi sana . Wabunge sasa wako wapi , ndugu Mzawa kwa hali hata Wabunge wa Upinzani wakisema hawatakuwa na lao maama kama Serikali imenyimwa jengo akapewa mtu binafsi utafanya nini ? Hili ni swala JK kuamuaru uchunguzi wa haraka na kulitolea maamuzi maana hii ni rushwa ya wazi na Seeikali iko macho inaona .Sasa kama mali ya Mke wa MKapa na mtoto wa Mramba na yeye ni Waziri sasa tutasema nini ? CCM safiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii

Maana CCM wao Chama mbele na maslahi ya Tanzania baadaye ama hata yasipokuwepo they have nothinhg to loose .Wanapata ruzuku 1bn na Bungeni wanatesa sasa nini ?
 
JK ameweka pamba masikioni na hamna hata mmoja anayethubutu kuzitoa hizo pamba. Itabidi tusubiri mujiza.
 
Mugishagwe,
Karibu tena. Kama ni akina Mkapa hawa wameshazoea kuchukua vya bure. Angalia ile nyumba ya pale Seaview
 
Back
Top Bottom