Mali wameweza kujenga daraja hili kwao, hivi kweli Tanzania tunashindwa la Kigamboni?

Magezi

JF-Expert Member
Oct 26, 2008
3,359
692
mali%2Bbridge.jpg
 
Mpaka roho inauma jinsi nchi maskini kama Mali wameweza kujenga daraja hili nchini kwao lakini CCM na siasa zao za kinafiki na wizi wameshindwa kujenga daraja la kwenda kigamboni.

Ukifikiria sana unaweza kujiuliza vipaumbele vya serikali ya CCM huwa ni nini kila mwaka?
 
Ngoja kwanza, wamejenga waMali wenyewe kwa kutumia rasilimali zao (wahandisi, kampuni, hela, vifaa, teknolojia nk) au wamepewa msaada na wafadhili? Maana msije mkaanza kuwasifia kumbe project nzima imefanywa na Wafaransa..
 
Ngojeni la kigamboni linakuja... ni mipango tu na kuangalia contractor gani anapewa kazi
 
Ngoja kwanza, wamejenga waMali wenyewe kwa kutumia rasilimali zao (wahandisi, kampuni, hela, vifaa, teknolojia nk) au wamepewa msaada na wafadhili? Maana msije mkaanza kuwasifia kumbe project nzima imefanywa na Wafaransa..

Kwa priorities za kujenga nyumba ya gavana wa BOT kwa bilioni 2 hatuwezi kulijenga!!!
 
Nasikia la kigamboni NSSF wanapigwa zengwe kuna mtu kalamba ten% ya waarabu ndo anawapigia debe,
Kaaaaaaaaaaaazi kweli kweli kila kitu ni ten % tz bwana
 
Wala msiwe na wasiwasi, litajengwa tena haraka sana, na litakuwa zuri ajabu. Si mnajua kuwa Mmarekani anamiliki kigamboni?

Nadhani wanapoteza muda kidogo kwenye mpango wa nssf ili awamu ya pili ya jk ikija mpango wa US unakuwa wazi na kila rangi inawekwa nuruni!

Tutajiju!
 
Hawa ni MALI: GDP(nominal)2008 estimate - Total$8.774 billion - Per capita $656

Na sisi Tanzania: GDP(nominal)2008 estimate - Total$20.668 billion - per capita $520
Sasa kufikiri eti Mali ni masikini ni upuuzi wa hali ya juu.

Pia Rais wao miaka ya 90 Prof. Alpha Oumar Konaré aliwasaidia saana kuwafikisha hapo walipo. Huyu jamaa ni wale watu ambao wanaenda ULAYA kusoma na kuelimika. Shule aliyoipata huko nje, hasa kimaisha, ilimfanya aliporudi kwao akaanza kufanya mambo kama nchi za nje.

Hizi road Interchange zilizopandana, round about kubwa na SANAMU nasikia amezipanda nyingi tu. Ila hilo daraja ni la zamani saana. Kuna yule Rais alikuwa dictator Moussa Traoré na aliuwa sana sana, hapa kwenye hili daraja kulifanyika kitu kibaya sana. Watu walikuwa wanaandama na jamaa akafunga daraja na kuanza kupiga risasi. Watu wakaanza kurukia majini na huo mto una mamba kibao.

7551d1263493469-a-bamako.jpg
 
Attachments

  • BAMAKO.jpg
    BAMAKO.jpg
    198 KB · Views: 590
Hawa ni MALI: GDP(nominal)2008 estimate - Total$8.774 billion - Per capita $656

Na sisi Tanzania: GDP(nominal)2008 estimate - Total$20.668 billion - per capita $520
Sasa kufikiri eti Mali ni masikini ni upuuzi wa hali ya juu.

Mali siyo maskini? Ok unaweza kuwa mhamiaji huko?
 
Hawa jamaa wako wengi sana Ufaransa. Wengi wakichuma basi wanarudi kwao. Wengi wao wameishi Ufaransa/Western Europe na hivyo ufahamu wao wa mambo ni MKUBWA sana zaidi yetu sisi. Ila kumbuka hadi mwaka 1991, hawa jamaa walikuwa masikini sana chini ya Dikteta huyo nimeandika huko nyuma. Labda ni ajabu kuwa wametupita wapi sisi ambao tangu mwaka 1964 tuko huru? Imekuwaje kipato chao kimekuwa juu kwa haraka sana kutuzidi sisi?

Angalia hata kwenye mpira wa miguu, wana wachezaji wanne mashuhuri sana duniani yaani yaani Keita, Diarra, Kanoute na Sissoko. Wengine waangalie mwenye kwenye Wikipedia.

Pia wana matajiri wakubwa sana kulinganisha na wetu na wanarudi kwao kuwekeza. Mfano ni huyu hapa mwenye kampuni ya AIRNESS.

Airness is a footwear trademark founded in 1999 in Saint-Denis (France) by Malamine Koné (December 21, 1971 in Niena, Mali) who is a Malian and French entrepreneur

Hawa jamaa wana suply jezi za timu ya Mali, Guinea, Gabon, DR Congo na Bennin. Pia wanasuply AJ Auxerre, Havre Athletic na Toulouse na pia wanam-suply Nikolay Davydenko (Tennis).
housse-couette-airness-22056_m.jpg
 
chini ya daraja hilo inaweza pita meli? au linapitisha vidau vya wavuvi tu

Hilo linawezekana. Ila sema watabidi wachimbe sana na aneo refu tu. Hapa nafikiri wameongezea tu upana ili kutunza maji yanayotumika Bamako. Ila mbele na nyuma ya mto ni mwembamba sana na au kugawanyika sehemu mbili.
 
chini ya daraja hilo inaweza pita meli? au linapitisha vidau vya wavuvi tu

Tangu lini meli zikapita kwenye mito ya Ukanda wa Tropical na Sahara.....
Mali ni land locked country hilo daraja lina cross mto mmoja hapo Mali. mashua na vivuko vinapita....
 
Hawa jamaa wako wengi sana Ufaransa. Wengi wakichuma basi wanarudi kwao. Wengi wao wameishi Ufaransa/Western Europe na hivyo ufahamu wao wa mambo ni MKUBWA sana zaidi yetu sisi.

Say what? Unahusisha kuishi Ulaya na ufahamu mkubwa? Kwa hiyo huwezi kuishi Afrika na kuwa na ufahamu mkubwa? Na kwa nini ukiishi Ulaya unakuwa na ufahamu mkubwa? Waulaya wameutoa wapi huo ufahamu mkubwa?
 
Hawa jamaa wako wengi sana Ufaransa. Wengi wakichuma basi wanarudi kwao. Wengi wao wameishi Ufaransa/Western Europe na hivyo ufahamu wao wa mambo ni MKUBWA sana zaidi yetu sisi. Ila kumbuka hadi mwaka 1991, hawa jamaa walikuwa masikini sana chini ya Dikteta huyo nimeandika huko nyuma. Labda ni ajabu kuwa wametupita wapi sisi ambao tangu mwaka 1964 tuko huru? Imekuwaje kipato chao kimekuwa juu kwa haraka sana kutuzidi sisi?

Angalia hata kwenye mpira wa miguu, wana wachezaji wanne mashuhuri sana duniani yaani yaani Keita, Diarra, Kanoute na Sissoko. Wengine waangalie mwenye kwenye Wikipedia.

Pia wana matajiri wakubwa sana kulinganisha na wetu na wanarudi kwao kuwekeza. Mfano ni huyu hapa mwenye kampuni ya AIRNESS.

Airness is a footwear trademark founded in 1999 in Saint-Denis (France) by Malamine Koné (December 21, 1971 in Niena, Mali) who is a Malian and French entrepreneur

Hawa jamaa wana suply jezi za timu ya Mali, Guinea, Gabon, DR Congo na Bennin. Pia wanasuply AJ Auxerre, Havre Athletic na Toulouse na pia wanam-suply Nikolay Davydenko (Tennis).
housse-couette-airness-22056_m.jpg

Sikonge unayosema ni kweli kabisa, I have been to Mali kwenye migodi yao ya dhahabu sometimes in 2000/ 2001. The country is so poor by whateva standards na kiujumla nadhani ilikuwa zaidi hata ya Tanzania by then. One thing they are the happiest pple I have ever met.

Can you imagine hawa jamaa wanafaidika mno kwa dhahabu yao kuliko sisi? And the same co. AnglogoldAshanti ambayo ipo hata Tz inaoperate tofauti kabisa in Mali.

1. Serikali ni shareholder mkubwa tu wa migodi yote ya dhahabu (I think it is around 25% kama kumbukumbu zangu ziko vizuri.

2. Wananchi wa Mali ni waadilifu sana na ni watu wa dini sana and therefore naamini kabisa hakuna ufisadi au kama upo ni kidogo sana.

3. Migodi yao ni kati ya best producing with highest gold grade in the world.

4. Wananchi wanaoishi maeneo ilipo migodi ni wadau wakubwa na wanafaidika moja kwa moja kwa kupewa fursa za supplies kwenye migodi.

5. As we speak migodi mingi sasa hivi inendeshwa na wazawa, some mines hata General managers, CEO's ni wazawa (Hizo hizo Barrick zenu, Anglo etc.). Tofauti kabisa na Tz. And mind you we almost started serious mining with them around 2000.
 
Tatizo ni uchaguzi wa vipaumbele. Kama Maghufuli angekuwa miundo mbinu hadi leo huenda wimbo ya kujenga daraja ingekuwa hadithi zau zilipendwa.

Leka
 
Say what? Unahusisha kuishi Ulaya na ufahamu mkubwa? Kwa hiyo huwezi kuishi Afrika na kuwa na ufahamu mkubwa? Na kwa nini ukiishi Ulaya unakuwa na ufahamu mkubwa? Waulaya wameutoa wapi huo ufahamu mkubwa?

Hamna haja ya kufikiri sana kifanyike nini wakati unaweza kucopy na kupaste toka Asia, Ulaya ama Marekani. Expoture is a window of hope to us.
 
Say what? Unahusisha kuishi Ulaya na ufahamu mkubwa? Kwa hiyo huwezi kuishi Afrika na kuwa na ufahamu mkubwa? Na kwa nini ukiishi Ulaya unakuwa na ufahamu mkubwa? Waulaya wameutoa wapi huo ufahamu mkubwa?

Omega,

Kama hujawahi kuishi nchi za nje, huwezi kufahamu nina maanisha nini. Angalia tu wenzetu hata kwenye Mpira, jinsi walivyowakali. Pia wameanza kuwa na Wazungu kwa miaka mingi sana hasa enzi za Falme za Mali.

Ukisoma maelezo ya Nyambala, utaelewa maana yake nini. Rais wao ambaye si tu aliishi nje ila pia alisomea nchi za nje alifanya kazi nzuri sana na sasa ni rais wa umoja wa Africa. Huyu jamaa ndiye alifanya mabadiliko mengi sana Mali na kama sikosei kiuchumi wao umesimama na hadi kutuzidi kwa ajili ya huyu jamaa. Na kama wataendelea basi watatuzidi kwa haraka sana sana.
 
Sikonge unayosema ni kweli kabisa, I have been to Mali kwenye migodi yao ya dhahabu sometimes in 2000/ 2001. The country is so poor by whateva standards na kiujumla nadhani ilikuwa zaidi hata ya Tanzania by then. One thing they are the happiest pple I have ever met.

Can you imagine hawa jamaa wanafaidika mno kwa dhahabu yao kuliko sisi? And the same co. AnglogoldAshanti ambayo ipo hata Tz inaoperate tofauti kabisa in Mali.

1. Serikali ni shareholder mkubwa tu wa migodi yote ya dhahabu (I think it is around 25% kama kumbukumbu zangu ziko vizuri.

2. Wananchi wa Mali ni waadilifu sana na ni watu wa dini sana and therefore naamini kabisa hakuna ufisadi au kama upo ni kidogo sana.

3. Migodi yao ni kati ya best producing with highest gold grade in the world.

4. Wananchi wanaoishi maeneo ilipo migodi ni wadau wakubwa na wanafaidika moja kwa moja kwa kupewa fursa za supplies kwenye migodi.

5. As we speak migodi mingi sasa hivi inendeshwa na wazawa, some mines hata General managers, CEO's ni wazawa (Hizo hizo Barrick zenu, Anglo etc.). Tofauti kabisa na Tz. And mind you we almost started serious mining with them around 2000.

Nyambala,

ni kweli kuwa hawa jamaa walikuwa masikini sana. Kwani hiki kipindi ilikuwa ni miaka 10 tangu waishi chini ya Dikteta mmoja aliyedumu kwa muda mrefu sana hadi wakachoka na kumuondoa madarakani. Jamaa aliyefanya mapinduzi akajitoa na kuachia serikali ya kiraia na ndipo akaja Rais Alfa. Huyu jamaa alileta ndoto zake za alivyoona Ufaransa na kuanza kuviweka hapo kwao Mali. Ukiangalia wenzetu Bamako, wanabarabara hadi zilizopandana (konokono). Pia walishaandaa mashindano ya Afrika, jambo ambalo sisi hatuliwezi.

Kuna kabila moja nimesahau jina, nasikia ni wafanyabiashara wakubwa sana na wako wengi Ufaransa. Hawa jamaa wanapeleka hela nyingi sana kwao. Pia wana wacheza mpira ambao nimesema na wanamuziki wakubwa sana duniani kama Serif Keita (Albino), Amadou and Mariam (vipofu) na Marehemu Ali Farka Toure (RIP) ambaye alipata Grammy Award.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom