Mali na makazi ya wanakijiji wapatao 200 kimbiji - kigamboni zimeharibiwa na wanajeshi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mali na makazi ya wanakijiji wapatao 200 kimbiji - kigamboni zimeharibiwa na wanajeshi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by nngu007, Aug 31, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Aug 31, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145


  NANI ALEYATOA AMRI YA KUWAVUNJIA MAKAZI NA KUWAHARIBIA MAZAO
  WANAKIJIJI KIMBIJI ??

  SOURCE:
  http://fundirkombo.blogspot.com/


  [​IMG]

  Wanakijiji wa kimbiji bado wamebaki na mshangao ! hakuna afisa yoyote wa serikali, kuanzia wilaya, mkoa hadi serikali kuu aliyekwenda kuangalia uharibifu! wala kutoa tamko lolote la kuwalinda wanakijiji !

  Uvamizi wa wanajeshi dhidi ya wanakijiji Kimbiji ! Polisi hawajakubali kupokea malalamiko ya wanakijiji ! nani ? wa kumfunga simba kengele?

  Uvamizi uliofanyika 16.08.2011 jumanne saa 4.00 hasubui wakazi kijiji cha Kimbiji,nje kidogo ya jiji la Dar, wamekuwa na mashaka ya maisha baada ya makazi na mazao yao kuharibiwa vibaya na wanajeshi (JWTZ) ambao walivamia kijiji hiko na kuvunja vunja makazi ya raia..kinyume cha sheria.

  Hata hivyo baadhi ya wanakijiji walipeleka taarifa katika vya vituo vya polisi vya Kigamboni na mji mwema, havijakubali kupokea malalamiko ya wanachi walioharibiwa mali zao na kutishiwa usalama wao, hadi sasa inaonekana kuwa wanachi wa Kimbiji hawana wa kuwalinda wao na mali zao, kama inavyoeleza katiba ya nchi kuwa kila raia ana haki ya kupewa ulinzi wa maisha yake na mali zake!

  Katika Sakata hili la wanajeshi (JWTZ) kuvamia makazi ya raia na kuharibu mali za raia bado lina utata wa nani ? kumfunga kengengele simba?

  Pamoja na ujangili huo uliofanywa na wanajeshi hao dhidi ya wanakijiji cha kimbiji hakuna uongozi wowote wa ngazi ya wilaya au taifa kutembelea eneo la wanakijiji hao ambao wamekuwa "punching bag" la kujipimia nguvu wanajeshi !

  Serikali ya kijiji na wanakijiji wa Kimbiji wamebaki midomo wazi na kupatwa na mshangao mkubwa kutokana na ukimya wa serikali na vyombo vya dola kugeuka bubu kwa kutoingilia kati sakata hilo, wala kutotoa karipio kali dhidi ya wanajeshi wenye tabia za kuwanyanyasa wanakijiji wa Kimbiji na sehemu zingine ambazo zimeshafanyiwa vitendo vya kinyama na wanajeshi wa JWTZ

  jaribu kuwasiliana na mwenyekiti wa kijiji Kimbiji
  Simu 0713846688 hili kupata mkasa wenyewe ulivyokua.
   
Loading...