Mali iliyoko Singida ni utajiri kwa watu wake na Taifa

Intelligence Justice

JF-Expert Member
Oct 23, 2020
3,036
3,479
Wakuu,

Mjadala unawekwa mezani kuhusu fursa za kiuchumi kutokana na rasilimali asili zilizoko Singida

1. Safu za mlima Sekenke hadi Makutupora ina mkanda wa madini ya Dhahabu. Wajerumani walivuna sana madini hayo na jinsi ya usafirishaji wake ilikuwa wanatumia mitaro ya zege.

2. Zao la Vitunguu ni moja la mazao la aina ya viungo kwenye chakula

3. Zao la korosho kwa kulingana na mazingira ya ustawi wake ni fursa ya kiuchumi kwa kuwa matumizi yake ni mtambuka (mafuta, kitafunwa, kimiminika cha alikoholi)

4. Miti asili ya Mihama inayofanana na minazi ambayo inaishi sio chini ya miaka 300

5. Maziwa yenye uhusiano wa kiasili (Singida na Kindai) moja lina maji chumvi jingine lina maji mchanyiko baridi na magadi yanafaa sana kwa uwekezaji wa kitalii, mapumziko na utafiti;

6. Miamba ya mawe iliyobebana kwa nguvu za asili bila kuanguka yanafaa kwa uwekezaji wa utalii

7. Zao la Alizeti ambapo mazao hayo yanawakilisha upendo na kudumisha uzao wenye furaha-mazao yake yanatumika utengenezaji wa mafuta, makapi/mashudu yake yanatumika kwa ajili ya kulisha mifugo

8. Upatikanaji wa ndege asili wa Kware na Kanga kwa wingi

9. Nyuki, asali na nta

10. Mazao ya karanga, njugu mawe, kunde, na ubuyu (kwa juisi, mafuta na sabuni)

Rasilimali nilizoainisha hapo juu ambazo zinapatikana kwa wingi huko Singida ni fursa pekee kwa watu na serikali kiuchumi na maendeleo
 
Lakini bado ni moja ya Mikoa ambayo wakazi wake ni maskini wa kutupwa sasa mali zote Izo mmezilalia tu mbona hampo serious nyie wakazi?
Tutakuja kuvuna tuwaache kama mlivyo
 
.... ongezea:-
11. Asali (nyuki wakubwa na wadogo).
12. Mbao - MNINGA
13. Tundu Lissu - product ya Singida hii; libarikiwe tumbo lililomzaa.
14. Mifugo
15. Humble people - generally ni watu wasio na tabia za ajabu ajabu.
16. n.k.
 
Back
Top Bottom