Singida ndio home
JF-Expert Member
- Feb 23, 2012
- 3,192
- 3,353
Nakumbuka viroja na vituko vya watoto wa matajiri jinsi walivyoathiriwa na pesa nyingi za wazazi.
Chuoni nakumbuka nimesoma Arusha basi kuna kipindi chuo cha Ifm kilijaa ikabidi wanafunzi wengine waje huku chuo cha uhasibu arusha, Walikuja vijana kama wanne hivi napokaa wakitafuta hostel mi nikawaunganisha na mwenye hostel wakalipa, Aisee!!! kile kikundi kilikuwa cha kishua si mchezo, kulikuwa na hadi mtoto wa mtu mzito sana serikalini, Nakumbuka moja wao mama yake alikuwa anatumia milioni kila mwezi na kila chuo kikifungwa anatumiwa laki 5 ya ndege,Matumizi yalikuwa ya ajabu sana moja wao alikuwa anapenda sana madem na aligombaniwa pia na madem wengi kwasababu alikuwa na pesa ya mzazi, alikuwa anakodisha lodge 3 tofauti analipia wiki 2 zote, lodge ya mianzini kwajili ya kusex na madem wake wa mianzini, Lodge ya kisongo kwajili ya kusex na mabinti wa huko na lodge ya njiro kwajili ya kusex na mabinti wa huko maeneo ya njiro.
Pia nakumbuka kulikuwa na mtoto wa mzito flani hapa mkoani, alivyomaliza form 4 alipewa range rover awe anatembelea, Aisee!!! Kila akipita full kushobokewa, Dogo alikuwa miaka 17 aligombaniwa sana hadi na dada zake waliomzidi kiumri akaishia kupata gono, Pia alipata marafiki wengi mno ambao hawakuwa na urafiki wa kweli wakaishia kumuingiza kwenye ulevi na matumizi ya bangi.
Je ni malezi yapi sahihi?