Malezi yapi sahihi? Watoto wengi wa matajiri pesa zinawaharibu sana!!

Machozi ya Simba

JF-Expert Member
Feb 23, 2012
3,219
2,000
1582469173819.png

Nakumbuka viroja na vituko vya watoto wa matajiri jinsi walivyoathiriwa na pesa nyingi za wazazi.

Chuoni nakumbuka nimesoma Arusha basi kuna kipindi chuo cha Ifm kilijaa ikabidi wanafunzi wengine waje huku chuo cha uhasibu arusha, Walikuja vijana kama wanne hivi napokaa wakitafuta hostel mi nikawaunganisha na mwenye hostel wakalipa, Aisee!!! kile kikundi kilikuwa cha kishua si mchezo, kulikuwa na hadi mtoto wa mtu mzito sana serikalini, Nakumbuka moja wao mama yake alikuwa anatumia milioni kila mwezi na kila chuo kikifungwa anatumiwa laki 5 ya ndege,Matumizi yalikuwa ya ajabu sana moja wao alikuwa anapenda sana madem na aligombaniwa pia na madem wengi kwasababu alikuwa na pesa ya mzazi, alikuwa anakodisha lodge 3 tofauti analipia wiki 2 zote, lodge ya mianzini kwajili ya kusex na madem wake wa mianzini, Lodge ya kisongo kwajili ya kusex na mabinti wa huko na lodge ya njiro kwajili ya kusex na mabinti wa huko maeneo ya njiro.

Pia nakumbuka kulikuwa na mtoto wa mzito flani hapa mkoani, alivyomaliza form 4 alipewa range rover awe anatembelea, Aisee!!! Kila akipita full kushobokewa, Dogo alikuwa miaka 17 aligombaniwa sana hadi na dada zake waliomzidi kiumri akaishia kupata gono, Pia alipata marafiki wengi mno ambao hawakuwa na urafiki wa kweli wakaishia kumuingiza kwenye ulevi na matumizi ya bangi.

Je ni malezi yapi sahihi?
 

Baba Joseph17

JF-Expert Member
Jul 15, 2013
8,342
2,000
Machozi ya Simba,
Miaka ile ya tisini nilisoma na baadhi ya watoto wa vigogo shule Fulani ya serikali nikichogundua ni kuwa mama zao hao watoto hawakuwa na malezi mazuri maana baba zao muda mwingi wako bize mtoto akitaka pesa anampigia mama kwa simu ya mezani ya TTCL utashangaa baada ya siku 2 Ems ya pesa mingi inatumwa na wengi wao waliishia pabaya
 

mangatara

JF-Expert Member
Jul 6, 2012
14,342
2,000
Hakuna malezi sahihi ya hao watoto wa vigogo. Malezi sahihi ni hao hao wazazi wao waweze kushuka na kukaa pamoja na wanyonge wawasaidie kidogo watoto wao kimaisha.
Huwezi kunielewa lakini most of them ni wahujumu uchumi hivyo fedha yao haina jasho hivyo huliwa kwa fujo. Utawezaje kumpa mtoto mmoja 1m fedha ya matumizi kwa mwezi. Je kama una watoto 4 nao wapo vyumo au wengine ndo wanaanza maisha utawapa nini?? Utakuwa unazipata wapi??
Mali ikipatikana kwa pupa huliwa kwa pupa. That is the theory of mali
 

Machozi ya Simba

JF-Expert Member
Feb 23, 2012
3,219
2,000
Miaka ile ya tisini nilisoma na baadhi ya watoto wa vigogo shule Fulani ya serikali nikichogundua ni kuwa mama zao hao watoto hawakuwa na malezi mazuri maana baba zao muda mwingi wako bize mtoto akitaka pesa anampigia mama kwa simu ya mezani ya TTCL utashangaa baada ya siku 2 Ems ya pesa mingi inatumwa na wengi wao waliishia pabaya
Pana ukweli hapa mama zao kuwapa kila wanachohitaji
 

Baba Joseph17

JF-Expert Member
Jul 15, 2013
8,342
2,000
Pana ukweli hapa mama zao kuwapa kila wanachohitaji
Mama/wake zetu hawajui malezi bora kwa watoto, dingi unaweza ukawa ni mkali na vijana wako wanakuogopa lakini kama mkeo hakupi taarifa (maana yeye ndo anakaa nao muda mrefu na hata ishu zao anazifahamu) we jua wakiharibikiwa mkabe mama yao kwanza
 

Machozi ya Simba

JF-Expert Member
Feb 23, 2012
3,219
2,000
Ukinitajia mtoto mmoja tajiri mwenye tabia chafu, nitakutajia watoto watano wa masikini wenye tabia chafu.
Ishu ni ngao ya wazazi, Watoto wa matajiri hata wakifanya upuuzi kesi zinaisha juu kwa juu na kiburi na jeuri inaongezeka, Watoto wa masikini wakiufanya huo upuuzi wanaishia segerea.
 

david steve

JF-Expert Member
May 17, 2015
830
1,000
Mfano halisi ni mimi yameniathiri kiasi kikubwa sana now nafanya kazi ambazo hata sikuwahi kuwaza kama ntazifanya naona aibu kukutana hata na marafiki zangu...
 

Nkwe2RG

JF-Expert Member
Nov 11, 2014
233
250
Mfano halisi ni mimi yameniathiri kiasi kikubwa sana now nafanya kazi ambazo hata sikuwahi kuwaza kama ntazifanya naona aibu kukutana hata na marafiki zangu...
Samahan mkuu... kwa upande wako unaona shida ilianzia wapi hasa kiasi ukaathirika na mapesa ya wazee wako? Tuna la kujifunza kwako, mkuu
 

david steve

JF-Expert Member
May 17, 2015
830
1,000
CC:Nkwe2RG malezi ya kuzoeshwa kupewa kila unachohitaji yaan kwako wewe hujui maana ya shida
 

MLEVi Mmoja

JF-Expert Member
Jun 29, 2019
6,032
2,000
Kuna wakishua darasani anagonga A kama zote

Kwenye mpira sasa ni kama ronaldo hata timu ya mkoa inamtegemea


Kwenye kusali na kuongoza ibada semina na maupupu ya kila aina ndo usiseme


Mademu wanamgombania kama vile pesa zinazorushwa kwenye mkusanyiko wa watuNguvu na karatika ,judo taikondo anazijua sio legelege na anakidunda kabisa


Hanaga show off


Na licha ya kuwa wakishua kwao ukute kamaliza chuo tayari kapata na ajira kabisa bila msaada wa mzee

Na hana tabia mbaya


Haya sasa tuje kwa wewe mtoto wa mbwa ndo balaa ...

Hapo ndo utajua life is not fair

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Top Bottom