Malezi ya wenetu yanapokuwa ya laana….!

Mtambuzi

Platinum Member
Oct 29, 2008
8,806
15,335
804027871.jpg

Wataalamu wamethibitisha hivi sasa kwamba, familia ambazo wazazi ni walevi kwa mfano, au ni wavuta bangi, ni rahisi sana kwao kuwarithisha watoto wao kuliko watu wanavyofikiria. Jambo ambalo halipendezi katika matokeo ya tafiti nyingi kuhusu hali hii ni ule ukweli kwamba, badhi ya tabia mbaya hujitokeza wakati watoto wa familia yenye ‘laana’ fulani wakiwa barubaru, (miaka 13 hadi 19) au huweza kujitokeza ukubwani. Kwa nini nimesema halipendezi? Subiri nitakwambia.

Tabia walizozitaja wataalamu hao ambazo ni kama laana kwa familia kwa sababu hurithiwa kirahisi na watu wa familia husika ni pamoja na kupigana, kuiba, kukosa uzingativu au utulivu wa mahali pamoja au kukosa uwezo wa kuheshimu sheria au kuheshimu watu walioko madarakani.

Katika jarida la Abnormal Child Psychology la hivi karibuni limebainisha kwamba, ni mara chache kukuta mtoto hajaathiriwa na tabia za wazazi wake ambazo hujitokeza sana katika familia. Kwa mfano kati a watoto watano wa wazazi walevi, anaweza kupona mtoto mmoja tu. Labda tu kama mzazi mmoja anapinga ulevi na ndiye mwenye nguvu kwa watoto. Kwa nini nilisema pale awali kwamba, yale ni matokeo yasiyopendeza? Nadhani unakumbuka. Basi nilikuwa na maana hii:

20th+Annual+Soul+Train+Music+Awards+Arrivals+0l9qCwKPocUl-404x450.jpg

Mwanamke: Hebu fikiria kwamba, umepata mchumba, handsome boy, ana fedha zake na amesoma madarasa ya kutosha. Anataka kuwa na uhusiano nawe, tena pengine uhusiano wa kudumu yaani kuoana. Je utaangalia tu uzuri, elimu na fedha zake au utakwenda mbali zaidi?
post.png

Mwanaume: hebu chukulia kwamba, umekutana na msichana, jicho-jicho, guu-guu, kalio-kalio na anajua mahaba, halafu amekubali kuwa mpenzi wako, nawe umebabaika unataka haraka sana muitwe mke na mume. Je unajitendea haki kuishia kwenye guu-guu tu au unapaswa kwenda mbali zaidi?

Kwa kawaida familia anayotoka mtu ina mchango mkubwa sana kuhusiana na tabia za mtu huyo. Anaweza asioneshe tabia hizo wazi na hata akizionesha kwa kiasi fulani unaweza kushindwa kujua kwamba, ni tabia ambazo hawezi kujiepusha nazo, kwani ni za familia kwa sababu hujui familia yake. Kwa hiyo badala ya kuishia kwenye guu-guu au jicho-jicho na kuishia kwenye u-handsome, elimu au fedha, inabidi uende mbali zaidi. Kama kweli unataka kuwa na familia bora na imara, inabidi uende mbali zaidi pale unaposema umempenda fulani.
de8c9_black-couple-arguing-pf.png

Usipoenda mbali utampata handsome ambaye amerithi kupiga mke, amerithi ulevi, amerithi ghubu na mengine yanayofanana na hayo. Kwa kuwa umempenda utakaa kwenye ndoa ya mateso na vipigo, ambapo watoto wenu nao watakuwa ni wa kupiga wake au kupigwa na waume zao na kuwavumilia. Hapo mtakuwa mnaendeleza familia ya laana. Mila na desturi zetu zilikuwa zinahimiza kwamba, kabla ya vijana hawajaamua kuwa pamoja, ilikuwa ni lazima wazazi kujua kuhusu familia ya mwingine. Hata kama haina maana kuwa mmoja akijua mwenzake familia yake ina laana ya kupiga, aachane naye, hapana. Kwa kujua, anaweza kuwa kwenye nafasi ya kujua namna anavyoweza kumsaidia mwenzake kuchana na tabia hiyo au kujisaidia kuepuka vipigo kwa maana ya kuchukua tahadhari.
Corbis-42-28379829.jpeg

Wazazi wetu zamani hawakuwa wajinga walipokuwa wanachunguza familia ya mahali binti yao anapotaka kuolewa au kijana wao anapotaka kuoa. Walikuwa hawajui somo linaloitwa saikolojia, lakini walikuwa wakijua kwamba, tabia mbaya au nzuri zinawezsa kuwa zinatembea katika familia. Ni jambo la kusikitisha kukuta binti anajua vizuri familia ya mpenzi wake kwamba, baba wa mpenzi wake huwa anampiga sana mkewe, mbaya zaidi, inawezekana ameshaanza kuona dalili za mkono mwepesi wa kupiga kwa huyu mpenzi wake. Lakini bado anang’ang’ania kuingia kwenye ndoa na mpenzi huyu mkorofi. Huu ni ujinga….

Ukweli ni kwamba ukienda kuoa kwa wapewa na watoa talaka, jiandae kwa kutoa au kupewa talaka. Huna haja ya kujidanganya kwamba, utaweza kubadili tabia hii kirahisi kama unayeoana naye anayo kutoka katika familia yake………..
 

Mtambuzi

Platinum Member
Oct 29, 2008
8,806
15,335
Tabia huwa inaambukiza na inaambukiza kwa njia ambayo ni sawa na mtu kupita mahali ambapo pana rangi mbichi ambayo humuingia kwenye mwili au nguo,halafu tayari anakuwa na rangi hiyo bila hiyari yake. Hakutaka kujipaka rangi, lakini rangi iko pale na ameigusa, hawezi kuepuka kujipaka. Kwa hiyo mzazi au wazazi wanapokuwa na tabia mbaya, watoto hudaka tabia hizo kwa njia hiyo.

Awali wanaweza kuzichukia, lakini baadaye ukubwani wakazitumia kwa sababu ndizo njia pekee wanazozijua katika kukabiliana na matatizo ya kimaisha.
 

King'asti

JF-Expert Member
Nov 26, 2009
27,801
24,510
Kuzmbe hata sio kosa langu kuvuta bhange?
Seriously, nakubaliana na wewe sawia mshua. Kuna wototo wa binamu yangu nawahurumia kweli manake wanaishi exactly ya wazazi wao. Nimejaribu kuwasaidia nimekwama. Manake binti amepewa mimba na kijana mwenzie ila amemshikisha mume wa mtu pia aliekuwaanatembea nae. Na hii habari nasimuliwa na mama yao mzazi huku anamsifia binti mdogo kuwa mjanja kuliko mkubwa.
 

snowhite

JF-Expert Member
Aug 2, 2012
17,377
22,819
bahati mbaya sana sasa hivi watu wengi au ndoa nyingi zinafungwa kwa sababu moja tu
GUU GUU,KALIO KALIO
HANDSOME,ANA JIMUDU KIMAISHA!
mkiingia ndani kila mtu anajiona mzuri zaidi ya mwenzie!
mkichangnya na malezi mliyolelewa amabapo baba kurudi usiku wa manane akiwa amelewa ni kawaida na binti kutumwa kwa the so called uncle au kijana kutambulishwa kwa nyumba ndogo ya mzee!
walahi hao watoto watakaopatikana kwenye hiyo familia ni balaa!
aina ya maisha tunayoishi na wenzi wetu huchangia sana sana mahusiano ya watoto wetu na jamii.
mtoto akikua kwenye familia anayoshuhudia baba na mama yake ni marafiki hujifunza kupenda na kupendwa pia!
anayeishi kwenye familia kinyume chake hujikuta kwenye akisi hiyo kwenye mahusiano yake na jamii!
 

Blaine

JF-Expert Member
Jan 11, 2012
2,276
1,652


Mwanamke: Hebu fikiria kwamba, umepata mchumba, handsome boy, ana fedha zake na amesoma madarasa ya kutosha....

Mwanaume: hebu chukulia kwamba, umekutana na msichana, jicho-jicho, guu-guu, kalio-kalio na anajua mahaba, halafu amekubali kuwa mpenzi wako, nawe umebabaika unataka haraka sana muitwe mke na mume.
...
huu ni uzuri wa mkakasi. mke/mume bora sio appearance peke yake, appearance itakufanya uvutiwe naye na kujaribu mahusiano. tabia yake ndio itakujulisha kama yeye ni "Mr/Mrs Right" au ni "Mr/Mrs Right Now"

..... Kuna wototo wa binamu yangu nawahurumia kweli manake wanaishi exactly ya wazazi wao. Nimejaribu kuwasaidia nimekwama. Manake binti amepewa mimba na kijana mwenzie ila amemshikisha mume wa mtu pia aliekuwaanatembea nae. Na hii habari nasimuliwa na mama yao mzazi huku anamsifia binti mdogo kuwa mjanja kuliko mkubwa.
mhh! sounds liike riwaya nilizokuwa nasoma nikiwa shule, kumbe duniani kuna mambo.
 

Ndahani

Platinum Member
Jun 3, 2008
17,872
8,686

de8c9_black-couple-arguing-pf.png

Usipoenda mbali utampata handsome ambaye amerithi kupiga mke, amerithi ulevi, amerithi ghubu na mengine yanayofanana na hayo. Kwa kuwa umempenda utakaa kwenye ndoa ya mateso na vipigo, ambapo watoto wenu nao watakuwa ni wa kupiga wake au kupigwa na waume zao na kuwavumilia. Hapo mtakuwa mnaendeleza familia ya laana. Mila na desturi zetu zilikuwa zinahimiza kwamba, kabla ya vijana hawajaamua kuwa pamoja, ilikuwa ni lazima wazazi kujua


Kusuka nywele kina kaka, mhhh!

Wazazi wetu zamani hawakuwa wajinga walipokuwa wanachunguza familia ya mahali binti yao anapotaka kuolewa au kijana wao anapotaka kuoa. Walikuwa hawajui somo linaloitwa saikolojia, lakini walikuwa wakijua kwamba, tabia mbaya au nzuri zinawezsa kuwa zinatembea katika familia. Ni jambo la kusikitisha kukuta binti anajua vizuri familia ya mpenzi wake kwamba, baba wa mpenzi wake huwa anampiga sana mkewe, mbaya zaidi, inawezekana ameshaanza kuona dalili za mkono mwepesi wa kupiga kwa huyu mpenzi wake. Lakini bado anang'ang'ania kuingia kwenye ndoa na mpenzi huyu mkorofi. Huu ni ujinga….

Ukweli ni kwamba ukienda kuoa kwa wapewa na watoa talaka, jiandae kwa kutoa au kupewa talaka. Huna haja ya kujidanganya kwamba, utaweza kubadili tabia hii kirahisi kama unayeoana naye anayo kutoka katika familia yake………..

[/QUOTE]

Hilo nalo neno.....
 

Gunda66

JF-Expert Member
Mar 8, 2012
518
312
Naomba niepuke kikombe hiki cha ukoo wetu,,, naomba kuongeza sio familia tu bali ni ukoo mzima take it from me ukoo ukiwa ni watu wakuwa na wake au wanaume wengi kesheni kuomba kubadilisha laana hiyo lazvyo my dears kikombe hicho mtakinywa tu:smiling:
 

Mtambuzi

Platinum Member
Oct 29, 2008
8,806
15,335
Kuzmbe hata sio kosa langu kuvuta bhange?
Seriously, nakubaliana na wewe sawia mshua. Kuna wototo wa binamu yangu nawahurumia kweli manake wanaishi exactly ya wazazi wao. Nimejaribu kuwasaidia nimekwama. Manake binti amepewa mimba na kijana mwenzie ila amemshikisha mume wa mtu pia aliekuwaanatembea nae. Na hii habari nasimuliwa na mama yao mzazi huku anamsifia binti mdogo kuwa mjanja kuliko mkubwa.
King'asti na ushukuru Mungu nimekufunza kuvuta Bangi, la sivyo ungekuwa unabakwa kila siku..........! LOL
 
Last edited by a moderator:

Lisa

JF-Expert Member
Aug 13, 2009
1,549
1,073
Ni kweli Mtambuzi, Unalosema, Mm upande wa wakwe zangu kuzaa nje ya ndoa ni kawaida kabisa, na Hata mume wangu ni mtoto wa nje ya ndoa. Nimekuja kustukia hiyo laana wakati nimeshaingia.Ninawaasa ambao hawajaolewa/kuoa wapende kuchunguza familia wanazotaka kuoa au kuolewa maana unaweza kuingia kwenye familia ambayo ni ya ajabu ukaja ukajuta.
 

prianka

JF-Expert Member
Aug 29, 2012
684
168
Ni kweli Mtambuzi, Unalosema, Mm upande wa wakwe zangu kuzaa nje ya ndoa ni kawaida kabisa, na Hata mume wangu ni mtoto wa nje ya ndoa. Nimekuja kustukia hiyo laana wakati nimeshaingia.Ninawaasa ambao hawajaolewa/kuoa wapende kuchunguza familia wanazotaka kuoa au kuolewa maana unaweza kuingia kwenye familia ambayo ni ya ajabu ukaja ukajuta.
hapo umenena wangu
 

Ndahani

Platinum Member
Jun 3, 2008
17,872
8,686
Cognitive Theory na si laana.

Ndio maana wanasema waafrika, environment and beliefs, which sometimes are even misleading us, play a crucial role in our conditioning to the extent that we set ourselves in traps. We limit our potential to think outside the box believing that a curse or something unusual will happen
 

lara 1

JF-Expert Member
Jun 10, 2012
15,710
29,049
Mtambuzi mtambizi na theory zako za FALLACY kila kukicha!!!!!!!!!!! Mpaka nachoka kutoa CRITICS!!!!!

1. Theory yako imeignore the SI unit ya oblongata ya mtoto! IQ ya mtoto mwenyewe ina nafasi kubwa sanaaa katika behaviour ya mtoto no matter wazazi wapoje! Ndo maana unaweza kuwa mtoto wa mchungaji ila unagawa kila kona!

2.Mob psychology! Hata uwe mzazi mzuri aje kaka mwanao akijiunga na Mobb kwisha kazi!

3.Sentimental reasons! Ujue baba yako akiwa mlevi afu akija anawapa nakoz za uhakika, maza nyang'ang'a yale matukio hayatoki kichwani kirahisi so unaweza usinywe pombe maishani wala uasiweze kumpiga mwanamke kamwee! Au maza wako akiwa malaya akawaacheni mkiwa wadogo mkateseka huwezi kuja kugawa gawa kirahisi.

conclusion!!!!!!!!!!
Wazazi wabaya sana ni hawa liberal, si moto wala si baridi! They are so worried on being the best parents to their kids until they forget the basics!!!!!!!!! Its good though Like me, I enjoyed doing whatever the hell i wanted all my life and my mum will always back me up in anything! (Not quite a sucker mum!!!) I turned out fine didn't i? I wounder what kind of mother will i ever be!? (Not quite a sucker mum tooo!)
 

Kongosho

JF-Expert Member
Mar 21, 2011
36,006
23,863
Neno sana hili

Ndio maana wanasema waafrika, environment and beliefs, which sometimes are even misleading us, play a crucial role in our conditioning to the extent that we set ourselves in traps. We limit our potential to think outside the box believing that a curse or something unusual will happen
 

Ndahani

Platinum Member
Jun 3, 2008
17,872
8,686
Neno sana hili

Laiti kama tungelijua jinsi brain/mind inavyofanya kazi, waafrika tungebadilisha mambo haraka sana...ila mambo tunayoamini mengi sio sahihi...mizimu, biashara za kuroga, kutoamini kwamba tuna uwezo wa kufanya lolote kubwa...yote haya na mengine yanakuwa ndio limitations zetu when it comes to thinking....
 

yatima

JF-Expert Member
Mar 2, 2011
354
128
Si kwa uwezo wala kwa nguvu BALI KWA ROHO YANGU - asema Bwana wa Majeshi
 

Kongosho

JF-Expert Member
Mar 21, 2011
36,006
23,863
Hasa mizimu, ulozi, limbwata, kikombe cha babu

Jamani, shule hazijatufungua kabisa

Laiti kama tungelijua jinsi brain/mind inavyofanya kazi, waafrika tungebadilisha mambo haraka sana...ila mambo tunayoamini mengi sio sahihi...mizimu, biashara za kuroga, kutoamini kwamba tuna uwezo wa kufanya lolote kubwa...yote haya na mengine yanakuwa ndio limitations zetu when it comes to thinking....
 

nyumba kubwa

JF-Expert Member
Oct 8, 2010
10,312
8,344
Ndio maana waswahili walisema 'huwezi (ni ngumu) kuokota embe chini ya mfenesi'

Fikiria ukute embe chini ya mfenesi...sidhani hata kama utasthubutu kula...limetoka muembe gani na hapa kuna mfenesi. Lol
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

9 Reactions
Reply
Top Bottom