nsanzu
JF-Expert Member
- Jul 29, 2015
- 4,389
- 4,816
Hivi vidada vinakera mno dadaangu. Nakumbuka tulipofika darasa la nne mama akaanza kutufundisha kupika, kufua, kupiga deki na kuosha vyombo mimi na kaka zangu watatu. Tulinyooka mbona, mzee yeye zake zilikuwa ni safari tu za kikazi, akiwa home wote tunajua baba yupo ila stering ni mama. Hatukuwahi kuona mama akimdharau baba na mpaka leo mimi kazi za ndani huniambii kitu.Hahahahahahaha boss sio kwa hasira hizi taratibu
Ilikuwa tushapangiwa ratiba ya kila siku na mama, tukitoka shule ni twisheni, tukitoka twisheni ni kanisani mafundisho, tukimaliza mafundisho kurudi nyumbani mapemaa, hapo kama ni zamu yako kupika unakaa jikoni, haina nini wala nini labda siku hiyo unaumwa.
Nakumbuka kuna siku tumetoka shule tukawa tunakula, sasa bro aliyekuwa ana zamu ya kutoa vyombo akawa kamaliza kula kaenda kuoga ili awahi twit, mimi na mshikaji wangu siku hiyo kapita hom tumemaliza si nikaacha vyombo mezani bro hajamaliza kuoga, mama kuingia ndani akakuta vyombo mezani akauliza, nani kamaliza kula vyombo kaviacha hapa!? Nikamjibu ni zamu ya fulani kutoa, nikamtaja broo
Bi mkubwa akaja ananiuliza, unasemaje!? Nikamjibu tena, akanambia njoo utoe vyombo pumbavu we, yaani mwenzio akamalize kuoga ndio aje atoe vyombo na nyinyi mlikuwa mezani!? Adabu ya wapi hiyo!? Nikajifanya kama kugoma hivi, weeeeeeeee! Kilifuata kipigo heavy acha kabisa, hiyo tupo darasa la sita. Nilivitoa na kipigo sitosahau, tangu siku hiyo hata kama ni zamu ya mtu au mtu anatakiwa alifanye lile jambo na halina madhara nikifanya mimi, sisubiri aje mhusika nitalifanya tu, as long as halitaathiri utaratibu.