Malezi ya wazazi wa siku hizi na dosari zake!

Well said
Kuna community zingine kama wahindi na hata wazungu huwa hawawapigi watoto lakini the way wanavyokwenda nao mtoto anafata vile mzazi anavyotaka kutokana na culture yao, watoto wa kizungu tunavyo waona mienendo yao ni kutokana na utamaduni wa jamii nzima, tatizo ni sisi waswahili tunaotaka kuiga, na mchanganyiko wa uzungu na uswahili unatoa tabia ya ajabu
 
Wanawake wenzio wameiona hii. ..I bet watanuna
Wazazi wa kike wanachangia sana malezi mabovu kwa watoto. Tutamlaumu baba mtu ila kuna kipindi akiingilia kati ataambulia kauli "leba nilikua mwenyewe na manesi usinitesee mtoto" "haukunisaidia kupush" "huujui uchungu na maumivu ya kujifungua"

Akina mama wa siku hizi wanadekeza vibaya. Na zile kiss za mdomo uchafu mtupu
 
Duu! mleta uzi umenigusa.
Kwanza niseme uwazi mimi ni muumini wa kanisa katoliki. tuna utaratibu wa kusali jumuiya. kwa maana ya kusali nyumba kwa nyumba za wakatoliki kulingana na utaratibu wa kanisa.
Kuna siku tulienda kusali kwa dada mmoja ni Dr. wa hospitali ya BMC, uwiiiiii jamani wale watoto walinikera!!
Yaani sala zinaendelea mara wanakwenda pale mbele kwenye "altare" wanaanza kuvuta vitambaa, mishumaa, bibilia n.k" mara vinaanza kuimba nyimbo za shuleni, mara vinatuambia tunyanyuke kwenye viti vya nyumbani kwao, mama yao sasa ambaye ni Dr. yuko tu "yuuu, yuuuu plisi, plisi...)
Nimeapa siku nyingine wakipanga kusali jumuiya kwa Dr. siendi maana nitawafinya wale watoto wake
:mad::mad::mad::mad::mad::mad::mad:
Hahaha haaa hahaa. .Aibu kubwa sana hii kwa wazazi wanao jitambua
 
Wazazi wetu walikua very proud mtoto wao anaposifiwa kua na adabu na heshima mbele ya watu wengine ikiwemo wageni kama wametembelea nyumbani kwao. Siku hizi mtoto kua na adabu sio priority ya mzazi.. Hawaelewi kua mtoto aki behave ni sifa kubwa sana kwake mwenyewe na kwa mzazi pia
Hii ndio sababu moja wapo iliyo changia 'Jamii kuwa na watu kama kina amber rutty. Mariam birian. Juma okelo. Na vijana wengine wanaoshinda mitandaoni na kutukana watu matusi mazito mazito na kashfa juu Wema sepetu akiwa ni moja ya product ya malezi ya aina hiyo "

Jamii inapokuwa na majority kubwa ya watu wenye Tabia hizo. ..Taifa linaingia kwenye dosari kubwa na hatimae Lita onekana kuwa ni Taifa la watu wa hovyo ..wasiojua mantiki ya ustaarabu
 
Nikikumbuka kipigo alichokuwa ananipa mama yangu mpaka leo nacheka na kumshukuru sana kama kaka mkubwa kipigo kile kilinisaidia kufuata njia inayofaa na wadogo zangu wakaniiga. Kosa lolote liwe dogo au kubwa nilitandikwa sana na mama, kuchapwa malapa ya usoni kama yote, baba yeye alikuwa hapigi mara kwa mara ila akifikishiwa kesi na mama jiandae kufa. Alikuwa na waya huo wa umeme acha kabisa.
Maranyingi watu hukumbuka pale walipolelewa vizuri kwa kufundishwa adabu , heshima na ubinadamu kuliko kule walipodekezwa na kuharibiwa tabia

Wanakumbuka hata ikiwa ni kwa shangazi, mama mdogo, bibi au ndugu japo wakati huo wakiwa wanafunzwa adabu walikua wanadhani wanaonewa au wanateswa
 
Hii ndio sababu moja wapo iliyo changia 'Jamii kuwa na watu kama kina amber rutty. Mariam birian. Juma okelo. Na vijana wengine wanaoshinda mitandaoni na kutukana watu matusi mazito mazito na kashfa juu Wema sepetu akiwa ni moja ya product ya malezi ya aina hiyo "

Jamii inapokuwa na majority kubwa ya watu wenye Tabia hizo. ..Taifa linaingia kwenye dosari kubwa na hatimae Lita onekana kuwa ni Taifa la watu wa hovyo ..wasiojua mantiki ya ustaarabu
Ni kweli kabisa usemayo mkuu
 
Wewe acha tu mkuu ' tanzania ni Jahazi lililo Toboka. .kama halitofanyiwa service basi tusishangae tutakapoona linazama
Bahati mbaya sana wanaopigania maadili kwa watoto wanaonekana wamepitwa na wakati kwa hiyo kama ni jahazi la maadili limeachwa tu lifuate upepo utapolipeleka

Miaka kadhaa ijayo zitakuja sheria kama za nchi za magharibi, kwamba mtoto akiadhibiwa na mzazi anaenda kushtaki ustawi wa jamii na mzazi anaadhibiwa😃
 
Daaah! Inasikitisha sana na yote hayo vyanzo ni sisi wazazi wa kidigitali kwani tunawalea watoto kimadekezo kuliko kawaida.

Na ndio sababu mtoto anaweza mkosea mzazi akachapwa na ikitokea mtoto kakasirika basi mzazi atakwenda kumbembeleza yaishe wakati zamani hayakuwepo haya.
 
Hivi Shadeeya ushawahi kumuomba radhi mwanao kisa kanuna baada ya kumuadhibu? Au wewe mtoto kwako hakanywi?
 
Wazazi wa kiume wanakuwa wapi katika malezi?
mtoto anapokuwa mdogo ni wa mama, kwa maana ya kwamba 80% ya malezi yake ya udogoni yanabebwa na mama. Na ndio maana hata sheria inatuambia kwa wazazi wanaoishi mbali mbali baba anaruhisiwa kuishi na mtoto akiwa tayari ana umri wa 6+.

Hivyo mtoto yeyote akiwa na mitabia ya ajabu obvious lawama nyingi zinaenda kwa mama kwa kushindwa kutekeleza wajibu wake vizuri.
 
Wazazi wetu walikua very proud mtoto wao anaposifiwa kua na adabu na heshima mbele ya watu wengine ikiwemo wageni kama wametembelea nyumbani kwao. Siku hizi mtoto kua na adabu sio priority ya mzazi.. Hawaelewi kua mtoto aki behave ni sifa kubwa sana kwake mwenyewe na kwa mzazi pia
wazazi wa siku hizi priority kwao ni kuona mtoto anakua huku akiongea kingereza kwa ufasaha, suala la nidhamu kwao sio issue kabisa.

Kwenye hizi day care centers matoto mengi yana vichwa vigumu kweli hayasikii ukiyakataza kitu, halafu yakiguswa tu na kiboko kesho yake mama mtu huyu hapa anakuja kulalamika.
 
Back
Top Bottom