Sesten Zakazaka
JF-Expert Member
- Sep 10, 2017
- 10,561
- 19,054
Jumapili iliyopita nilihudhuria kwenye msiba wa ndugu wa rafiki yangu, Miongoni mwa waombolezaji alikua dada mmoja mwenye miaka kama 26-30, alikuwa na mwanae wa kama miaka minne hivi
Sijui ilikuaje lakini mara yule dogo akaanza kulia na kisha kumvurumishia ngumi na mateke mama yake. Mama mtu akabakia kusema tu " Brian stooop banaa". Mpaka mama mmoja alipokuja akamwambia hiyo ni aibu mwanao hata kama ni mdogo unamuachia akupige hivyo hebu ingieni kule chumbani mkabembelezane
Watoto wote wadogo sio ajabu kuwa na utundu lakini utundu mwingine nahisi kama ni wa kukosa adabu na unaendekezwa na wazazi hasa wakike.
Nimewahi kushuhudia mtoto wa chini ya miaka mitano akiipasua simu ya mama yake kwa makusudi kwa kuibamiza chini na mama mtu anasema "mmmh leo sijui kakasirika nini huyu!" halafu akaanza kumbembeleza!
Kuna mtoto wa shangazi yangu aliwahi kumtupia usoni mfuko wa chips mama yake baada ya kugundua alicholetewa sio alichomuagiza wakati anaenda kazini!
Hapo kwenye msiba baada ya tukio la huyo mama na mtoto watu walisema mengi sana kuhusu dosari za kimalezi za wazazi wa kike wa siku hizi. Kuna mzee mmoja akawa anasema dunia inavokwenda huko baadae hayo mapenzi ya mama na mwana yanaweza kufikia hatua ya aibu zaidi hata mama "kumuonjesha" mwanae atakapo balehe
Sina hakika kama haya mambo ya kudekeza watoto kiasi hiki yalikuwepo zamani ila nahisi mengine ni kuwapotosha watoto kwa kuwapa malezi yasiyofaa.