Malezi ya watoto

Aiba

JF-Expert Member
Oct 4, 2018
1,730
3,009
Ibada njema huanzia nyumbani vivyo ivyo katika malezi japokuwa mtaa unaweza mlea mtu na kumkuza vizuri inategemea watu gani anajichanganya nawo
 
Distant Relatives

JF-Expert Member
Nov 21, 2020
415
720
Kulea mtoto ni kazi ngumu sana. Inahitaji kujitoa, commitment, busara, udadisi, ufuatiliaji mapenzi na uvumilivu wa hali ya juu. Jambo unaloliona ni dogo sana, ila lina impact kubwa sana kwa malezi ya mtoto.

Wazazi wengi wa sasa tunaharibu kizazi sababu hatutoi muda wetu mwingi kwa watoto wetu, tunaachia shule. Shule hawana hayo hapo, Wao wanatafuta mshahara tu. Malezi ni nyumbani. Huo ndio msingi. Kulea mtoto ni project ngumu na ya muda mrefu sana.
 
Caroline Danzi

JF-Expert Member
Dec 19, 2008
3,711
1,249
Kulea mtoto ni kazi ngumu sana. Inahitaji kujitoa, commitment, busara, udadisi, ufuatiliaji mapenzi na uvumilivu wa hali ya juu. Jambo unaloliona ni dogo sana, ila lina impact kubwa sana kwa malezi ya mtoto. Wazazi wengi wa sasa tunaharibu kizazi sababu hatutoi muda wetu mwingi kwa watoto wetu, tunaachia shule. Shule hawana hayo hapo, Wao wanatafuta mshahara tu. Malezi ni nyumbani. Huo ndio msingi. Kulea mtoto ni project ngumu na ya muda mrefu sana.
Umenena vyema. Hapo kwenye commitment ni muhimu sana. Point taken.
 
Distant Relatives

JF-Expert Member
Nov 21, 2020
415
720
Umenena vyema. Hapo kwenye commitment ni muhimu sana. Point taken.
commitment muhimu sana kaka. Kuna time kinywaji kimekolea inabidi uache urudi home mapema ujue mtoto amekula, na ule nae. Huwezi lala kabla mtoto hajalala. Asubuhi inabidi uamke mapema uhakikishe anaenda shule yuko smart. Inabidi ujenge urafiki nae ili awe huru kufunguka kwako, hapo utajua yanayomkuta shule, watu anaokutana nao, marafiki zake wakoje, fikra na mitazamo yake ikoje ili umshape. Needs a high commitment!
 
Flashfifty

Senior Member
Feb 10, 2021
156
387

Well saidlazima wazazi tujitoe yan full participation ktk malezi ya watoto
 
Shimba ya Buyenze

JF-Expert Member
Dec 22, 2014
158,311
926,872
commitment muhimu sana kaka. Kuna time kinywaji kimekolea inabidi uache urudi home mapema ujue mtoto amekula, na ule nae. Huwezi lala kabla mtoto hajalala. Asubuhi inabidi uamke mapema uhakikishe anaenda shule yuko smart. Inabidi ujenge urafiki nae ili awe huru kufunguka kwako, hapo utajua yanayomkuta shule, watu anaokutana nao, marafiki zake wakoje, fikra na mitazamo yake ikoje ili umshape. Needs a high commitment!
Umemaliza kila kitu mkuu. Na mtoto anachohitaji zaidi ni wewe kuwa karibu naye. Ajue kuwa anapendwa, anajaliwa na kwamba yuko salama.

Ukimfanya kuwa rafiki yake na mkaaminiana basi kazi yako itakuwa rahisi sana kwa sababu atakuwa anakusikiliza, si kwa sababu ya hofu bali ile heshima, uaminifu pamoja na urafiki wenu.

Na ukiweza msogeze kwa Mungu. Sali naye. Nenda naye kanisani. Soma naye Neno na mruhusu ajihusishe na kuchangamana na marafiki zake wa huko kanisani; hasa wale wenye interests kama zake.

As a single father of a 13 yrs old girl, hii fomyula imenisaidia sana mpaka malezi yameonekana kuwa rahisi...
 
Caroline Danzi

JF-Expert Member
Dec 19, 2008
3,711
1,249
commitment muhimu sana kaka. Kuna time kinywaji kimekolea inabidi uache urudi home mapema ujue mtoto amekula, na ule nae. Huwezi lala kabla mtoto hajalala. Asubuhi inabidi uamke mapema uhakikishe anaenda shule yuko smart. Inabidi ujenge urafiki nae ili awe huru kufunguka kwako, hapo utajua yanayomkuta shule, watu anaokutana nao, marafiki zake wakoje, fikra na mitazamo yake ikoje ili umshape. Needs a high commitment!
Nidhamu na kujiota kwa wazazi katika kulea watoto ni muhimu sana. Mara zote wazazi wengi wamewaacha watoto wakae na walezi wao kuliko wao. Kama kuna kitu watoto hawapendi katika maisha yao ni kuona wazazi hawana nidhamu, kila wanachoongea kinakinzana na kile wanachowafanyiwa watoto. Wazazi hawaongei ukweli kwa watoto na kuwapelekea watoto kuishi bila kujua misingi ya familia inaelekea wapi.

Adhabu wanazopewa watoto haziilingani na kosa alilofanya mtoto (never displine a child in anger)
Watoto wanahitaji malezi ya usawa, hasa wale tunaolea watoto wa ndugu zetu na wetu, ni vizuri mzazi ukatengeneza usawa. Kama unaleta zawadi, basi leta zawadi zinazofanana.
Usiruhusu watoto wako kwenda kinyume na yale maelekezo uliyowapa au kubalidili maelekezo bila kuwashirikisha na kuhakikisha waelewe kwa nini umebadili.
Mtoto aheshimiwe, usipende sana kumkaripia mtoto au kumpiga mbele ya rafiki zake au kadamnasi, unamjengea hofu.
Watengenezee ratiba watoto wafanye nini na kwa wakati gani, hakikisha watoto wanaangalia au kusoma vitu vinavyowatengenezea ubongo wao kukua katika maadili.

Wazazi, tengenezeni ratiba za watoto wenu pamoja, elewaneni, ikitokea mtoto kakosea, asipate sababu ya kukimbia jukumu lake.
Watoto wanaumie sana wanapoona wazazi mnagombana kila kukicha, hakuna siku hamrushiani maneno ya hovyo mbele ya watoto wenu bila kufikiria ni kiasi gani mnaawathiri.

Watengenezee watoto wenu muda wa kukaa pamoja, watengenezee muda wa kuwapa kalamu na karatasi waandike yale wanayohisi yanahitaji kufanyiwa marekebisho, acha watoto wakutathimini utendaji wako, usiwaburuze ukahisi hawaelewi au hawana cha kukwambia. wanaogopa.

Zingatia kuwafundisha watoto siyo kuwaadhibu.
 
Caroline Danzi

JF-Expert Member
Dec 19, 2008
3,711
1,249
Umemaliza kila kitu mkuu. Na mtoto anachohitaji zaidi ni wewe kuwa karibu naye. Ajue kuwa anapendwa, anajaliwa na kwamba yuko salama. Ukimfanya kuwa rafiki yake na mkaaminiana basi kazi yako itakuwa rahisi sana kwa sababu atakuwa anakusikiliza, si kwa sababu ya hofu bali ile heshima, uaminifu pamoja na urafiki wenu. Na ukiweza msogeze kwa Mungu. Sali naye. Nenda naye kanisani. Soma naye Neno na mruhusu ajihusishe na kuchangamana na marafiki zake wa huko kanisani; hasa wale wenye interests kama zake.

As a single father of a 13 yrs old girl, hii fomyula imenisaidia sana mpaka malezi yameonekana kuwa rahisi...
Salute you! hongera kwa kuwa baba mwema.

Kuishi kwenye neno la Mungu ndio mpango mzima, ukisoma kitabu cha Mithali, malezi ya watoto wetu yako pale. Mzazi kuyajua na kuyaishi.

Tuendelee kupeana dondoo za malezi, tuokoe kizazi kijacho.
 
Caroline Danzi

JF-Expert Member
Dec 19, 2008
3,711
1,249
Ibada njema huanzia nyumbani vivyo ivyo katika malezi japokuwa mtaa unaweza mlea mtu na kumkuza vizuri inategemea watu gani anajichanganya nawo
Ukimlea vizuri toka nyumbani, atakuwa na uelewa achangamane na watu gani.
 
Evelyn Salt

JF-Expert Member
Jan 5, 2012
57,924
88,563
Wanangu wanapigana jamani, ni wanazichapa, naongea hadi najiona redio katika masaa matatu wanayocheza basi mawili wanatumia kupigana....hivi nifanyeje?!
 
Distant Relatives

JF-Expert Member
Nov 21, 2020
415
720
Hongera, ni ishara kuwa wana afya njema.

Waite kaa nao in lovely but serious tone.

Waulize kuwa kwanini mnapenda kupigana? Kisha waulize, mnajua sipendi mpigane?
waulize, mnanipenda?
kisha waulize kama mnanipenda kwanini mnafanya kitu sikipendi na mnanikwaza?

Jibu watakalo kupa, wafanye wakuahidi kuwa hawatopigana tena.
 
Hata hawaelewi nadhani umri wa kuelewa bado miaka 6 na 3
 
Ngalikihinja

JF-Expert Member
Sep 1, 2009
26,439
21,573
ikikupendeza, elezea kidogo ni wapi kama wazazi tunakosea na tufanye nini ili tuzalishe kizazi chenye maadili?
1. Mzazi mmoja kuwa kimbilio la mtoto anapopewa adhabu na mzazi mwingine
2. Mzazi mmoja kumsema mzazi mwingine au kutaka mapungufu ya mzazi mwingine mbele ya watoto
3. Mzazi mmoja kumfokea mzazi mwingine mbele ya watoto
4. Kuruhusu mtoto kupewa kitu anachokitaka kwa kukililia
5. Mzazi mmoja kuzuia mtoto kutumwa na mzazi mwingine
6. Mtoto kutoruhusiwa kufanya vishughuri vidogo vya nyumbani, mfano kujifulia Soksi etc
7. Kulala na mtoto huku ana umri wa kujua mazingira yake au wanapuliza sana maswali
etc
 
3 Reactions
Reply
Top Bottom