Malezi ya watoto ni Taaluma sio kitu cha asili

OEDIPUS

JF-Expert Member
Oct 12, 2019
209
500
Na Justine P. Kakoko.

Ni kwa miaka mingi sasa jamii za Afrika zimekuwa zikiamini ya kuwa malezi ya watoto ni kitu cha asili, yaani mzazi/mlezi haitaji kutafuta wala kujiongezea maarifa yahusuyo malezi ya mtoto/watoto wake. Wazazi/walezi wengi wamekuwa wakijiuliza, kuna haja gani ya wao kujifunza malezi ya watoto wao wakati uwezo wa kulea ni uwezo ambao kila mtu anazaliwa anao tayari?

Imani na mtizamo huu umeendelea kuwafanya waafrika wengi kuwa ni watu wenye maarifa na taarifa chache sana zilizo sahihi kuhusiana na malezi chanya ya watoto wao ukilinganisha na watu kutoka mataifa mengine kama vile mataifa ya ulaya.

Malezi ya watoto yana mambo mengi sana ambayo ili mzazi/mlezi aweze kuyamudu kwa kiasi fulani ni lazima ajifunze kwa njia mbalimbali. Ni ngumu sana mtu kuzaliwa anajua saikolojia, elimu, hisia au magonjwa mbalimbali ya watoto bila kujifunza kutoka sehemu yoyote ile.

Katika makala hii nitaelezea japo kwa ufupi kwanini ni muhimu mzazi/mlezi ajifunze malezi ya watoto na ni njia zipi ambazo sehemu mbalimbali duniani zinatumika katika kujifunza malezi ya watoto.

Tuanze na ni kwanini wazazi/walezi wajifunze elimu ya malezi ya watoto wao:-

Malezi ni taaluma ili kuijua lazima mtu ajifunze.
Kama zilivyo taaluma nyingine kwa mfano, mapishi, ushonaji na uchongaji, malezi ya watoto pia ni taaluma hivyo ili mtu aimudu vizuri ni lazima ajifunze aidha kwa njia rasmi au isiyo rasmi. Ni ngumu sana mzazi/mlezi kuweza kujua namna nzuri za kumsimamia mtoto wake kufanikiwa katika elimu yake bila kujifunza kufanya hivyo au ni ngumu sana mzazi/mlezi kuweza kujua namna nzuri ya kuisimamia afya ya mtoto wake bila kujua misingi na kanuni mbalimbali za afya ya watoto.

Kulea mtoto ni kumjua mtoto. Kamwe mtu hawezi kufanikiwa kukiongoza au kukikuza kitu asichokijua; ni ngumu sana mkulima kuweza kuotesha zao la mpunga kama hajawahi kujifunza kuotesha zao hilo; vivyo hivyo, ili mtu aweze kumkuza mtoto ni lazima amjue mtoto, ni lazima ajue ni namna gani anakua, anahisi, anafikiri n.k ili aweze kumkuza kwa mafanikio.

Elimu ya malezi itampa mzazi/mlezi nguvu na kujiamini katika safari yake ya malezi. Mtu anapofanya kitu anachokijua mara nyingi huwa ni mtu anayejiamini, hali inayopelekea hata matokeo yake yawe mazuri. Mzazi/mlezi mwenye maarifa juu ya malezi ya mtoto/watoto wake huwa anakijua anachokifanya, kamwe hafanyi mambo yake kwa kuhisi, kudhani au kujaribu anafanya kwa uhakika. Mtu anayefanya kitu kwa uhakika huwa anafanya kufanikiwa.

Elimu ya malezi itapunguza matumizi ya nguvu na kuongeza matumizi ya fikra kwa wazazi katika malezi ya watoto wao. Wazazi/walezi wengi hutumia nguvu sana katika kulitekeleza jukumu lao la kulea, wengi hujikuta katika mkumbo wa kuwaburuta watoto wao kwa kutojua. Hali huwa tofauti kwa mzazi/mlezi anayejua anachokifanya, mzazi/mlezi anayejua anachokifanya hujikuta anatumia fikra tu kutoa muongozo na hatimaye kukamilisha jukumu lake kwa ufanisi.

Kupunguza changamoto mbalimbali wanazokumbana nazo watoto. Unyanyasaji, ukatili, anguko la maadili kwa watoto n.k vyote hivyo vitapungua endapo wazazi/walezi watajifunza juu ya malezi ya watoto wao. Changamoto nyingi za watoto barani Afrika hazitokani na chuki ya wazazi/walezi kwa watoto wao bali ujinga wa wazazi/walezi wao juu ya malezi yao.

Utandawazi umeleta changamoto nyingi sana katika malezi ili kukabiliana nazo ni lazima wazazi/walezi wajifunze juu ya malezi ya watoto wao. Uwezo wa watu duniani kote kuweza kuingiliana kirahisi kumeleta changamoto nyingi sana katika kulea watoto, changamoto za afya, tabia, kielimu n.k ili wazazi/walezi waweze kukabiliana na changamoto hizi ni lazima watafute maarifa juu ya watoto wao yatakayo wawezesha kulea watoto wao kwa mafanikio.

Yawezekana wazazi/walezi wanaona ya kuwa malezi ya watoto ni jambo la asili kutokana na kutojua njia mbalimbali ambazo zinaweza kutumika katika kujifunza malezi ya watoto.

Zifuatazo ni njia kadhaa ambazo zinatumiwa duniani kote katika kujifunza malezi ya watoto.

Kujifunza kwa wazazi/walezi waliotangulia. Njia hii ni moja kati ya njia zinazotumiwa na watu wengi sana duniani, yaani mzazi/mlezi mpya anajifunza juu ya malezi ya watoto kwa kuwasikiliza au kufuata mbinu mbalimbali kwa wazazi/walezi wao. Faida ya njia hii ni rahisi sana mtu kujifunza kwa vitendo lakini madhara yake ni endapo maarifa aliyonayo mzazi/mlezi aliyetangulia sio sahihi basi yana hatari ya kuendelea kurithishwa kutok akizazi kimoja kwenda kingine bila kujua.

Kujifunza kwa jamii
. Wazazi/walezi kujifunza kwa kuangalia namna jamii yao inalea watoto.

Kusoma vitabu na machapisho mbalimbali. Njia hii inatumiwa sana na jamii za watu wanaopenda kujisomea vitabu. Wataalamu mbalimbali wa watoto wamefanya tafiti juu ya malezi kisha wakaandika mawazo yao kwa ajili ya wazazi/walezi kuweza kujifunza kwa kusoma.

Njia hii ni nzuri na rahisi sana kwani mzazi/mlezi anaweza kumudu kulea kwa kusoma tu kitabu. Njia hii inatumiwa kwa kiasi kikubwa katika mataifa yaliyoendelea kama vile Amerika.

Kusikiliza hotuba au mihadhara mbalimbali.
Hii ni njia nzuri sana pia, wataalamu mbalimbali hufanya semina juu ya malezi ya watoto hivyo mzazi/mlezi anaweza kujifunza malezi ya watoto kwa kuwasikiliza tu wataalamu wakiongea aidha katika kanda zilizorekodiwa au kwa kwenda kuwaona moja kwa moja.

Kujifunza kupitia taasisi za kidini kama vile kanisa au msikiti. Programu mbalimbali huendeshwa katika taasisi za imani zinazolenga kuwaendeleza waumini wao katika mambo mbalimbali yakiwemo mahusiano na malezi ya watoto. Mafundisho haya mara nyingi huegemea sana katika dini husika.

Kujifunza kupitia taasisi za elimu
. Katika taifa kama Marekani zipo taasisi za elimu ambazo mzazi/mlezi anaweza kulipa pesa na akajifunza mambo mbalimbali juu ya malezi watoto.

Kujifunza kupitia makosa.
Nakadiria njia hii inatumiwa na zaidi ya asilimia sabini (70%) ya wazazi/walezi katika mataifa yanayoendelea kama vile Tanzania.

Wazazi/walezi wanajifunza namna nzuri za kufanya malezi ya watoto baada ya kufanya makosa mbalimbali. Wazazi/walezi wengi wamepoteza watoto kwa magonjwa au kuwashindwa kabisa watoto kisha ndiyo wanapata funzo ya kuwa walipaswa kufanya tofauti na walivyofanya hapo awali. Njia hii ni moja kati ya njia hatari sana kutumiwa na wazazi/walezi katika malezi ya watoto.

Kwa kumalizia nitoe wito kwa wazazi/walezi hususani wa kiafrika waone haja ya kujifunza malezi ya watoto, kama wanavyoona ipo haja ya kujifunza kufuga kuku kutoka kwa wataalamu kabla hawajaanza na kufuga basi waione haja hiyo kujifunza malezi ya watoto kabla hawajaanza kulea pia.

1576559442614.png
 

Baba Joseph17

JF-Expert Member
Jul 15, 2013
8,622
2,000
Sikubaliani na kusema malezi ni taaluma, mihadhara ya kula pesa za watu tu, Wazazi wangu wametulea na wadogo zangu 7 na hawakupata taaluma kutoka popote, Tatizo naloliona kwa vijana wa leo mtu anafika umri wa kuoa au kuolewa hajawahi kulea mtoto wa ndugu au mdogo wake hili ni tatizo kubwa.
 

Nanye Go

JF-Expert Member
Oct 29, 2018
7,744
2,000
Malezi ya watoto siyo taaluma, niki ni kitu cha asili. Ndio maana hata wanyama porcini hulea watoto wao vyema kabisa.

Pesa hizi, zitatutoa roho kabisa.
 

Ncha Kali

JF-Expert Member
Sep 19, 2019
7,175
2,000
Malezi ya watoto siyo taaluma, niki ni kitu cha asili. Ndio maana hata wanyama porcini hulea watoto wao vyema kabisa.

Pesa hizi, zitatutoa roho kabisa.

Nimesoma uzi nikiwaza nikomenti hivi umenisemea mkuu, hizi fursa hizi mwisho tutaambiwa Waafrika hatufi vizuri tufundishwe namna njema ya kufa kama wenzetu.... malezi taaluma ambayo hayawani na ndege wa mwitu wamesomea wapi..?
 

Nanye Go

JF-Expert Member
Oct 29, 2018
7,744
2,000
Nimesoma uzi nikiwaza nikomenti hivi umenisemea mkuu, hizi fursa hizi mwisho tutaambiwa Waafrika hatufi vizuri tufundishwe namna njema ya kufa kama wenzetu.... malezi taaluma ambayo hayawani na ndege wa mwitu wamesomea wapi..?
Hahaha tutaambiwa hatuelewi sisi waafrika, lakini ulaya wazungu wanasomea ndio maana hatiendelei
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom