Balvejmumt
JF-Expert Member
- Aug 10, 2015
- 2,149
- 2,784
Habarini wakuu,
Mimi si mwandishi mzuri lakini naomba tusaidiane katika hili.
Naomba nianze na visa kama viwili nilivyokutana navyo siku za karibuni
Wiki mbili zilizopita,
Wakati nipo mapumziko ya kimatembezi baada ya kuihudumia jamii yangu kwenye masuala ya kitabibu ndipo nilipo kutana na hili tukio la kwanza. Ambapo niliitwa na Bibi ambaye Yuko jirani na taasisi ninayoifanyia kazi ambaye alikuwa akiambatana na kijana wake (mjukuu wa kiume) age ni kama 17-19 hivi ,sababu zilizompelekea Bibi huyo kuniita ni kunifanyia utambulisho kwa mjukuu wake huyo wa kiume ambaye mara nyingi alikuwa akija ofisini huniambia anamjukuu wake anasomea Udaktari, nilisalimiana naye na swali la kwanza nilimuuliza unasoma chuo gani? Namna alivyofungua mdomo Tu na kuanza kuzungumza huku akirembua na namna alivyosimama kulinipa wasi wasi mkubwa wa jinsia yake.
Alinijibu kuwa Yuko A-level kwenye combination ya science akipambana nayo huko.
Baada ya Hilo jibu, nikaona ngoja niende maana sioni cha muhimu nilimsihi tu apambane katika elimu na dhamira aliyo nayo
Kisa cha Pili ni hivi majuzi,
Alikuja msichana age 23-27 hivi akiwa na mtoto wa kiume age ni 2.5 hivi
Niwapo katika majukumu yangu nina katabia fulani baada ya kunielezea kilichokutoa nyumbani huwa na tabia ya kuunganisha au kujaribu kutizama tatizo lako usikute limechangiwa na tabia tulizo nazo kwenye jamii.
Baada ya kujua tatizo la mtoto nilianza kumtizama na kumfanyia uchunguzi nikagundua katika moja ya vidole vya mikono mtoto kapakwa rangi, sikuhangaika kumuuliza mama kulikoni?
Nilimuuliza baada ya kugundua mikono yote na miguu imepakwa rangi, nikamuuliza kwa upole mama imekuwaje mtoto wa kiume kupakwa rangi mikononi na miguuni tena yote? Akanieleza kuwa wenzie ndio walio mpaka, ikabidi niwe mkali kidogo kwenye kuhoji ndipo nilipo gundua ni Mama ndiye kafanya hiyo kazi ya kumpaka mtoto rangi mikononi na miguuni.
Kwanini nimeleta hii mada kwenu?
Nimeileta baada ya kuwaza na kujiuliza hawa watoto wote wawili yule wa kwanza na huyu wa pili ijapokuwa ni mdogo wote wanalelewa na mzazi mmoja (single parent) nikiwa na maana wanalelewa na mama pekee lakini maadili na ukuzwaji uko sahihi? Hasa linapokuja suala la mtoto wa kiume kulelewa kwenye maadili au muundo wa jinsia ya kike?
Mimi ni miongoni mwa vijana wa kale tuliolelewa na mzazi mmoja (mzazi wa kike) lakini hatukuwa hivyo kama tuonavyo katika makuzi ya kizazi hiki cha sasa kinacholelewa na vijana age 27-45 . .. Simaanishi wote hapana.
Najiuliza tunaenda kuwa na kizazi cha aina gani baada ya miaka 50? Je, ni jukumu la nani kuhakikisha haya madhila ninayo yawaza kipindi kijacho ni Nani wakulaumiwa?
Bado sielewi!
Balvejmumt
2022