Malezi: Wazazi ambao hawapo pamoja wanaweza kulea watoto katika mazingira bora

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
2,771
2,000
Kutokana na sababu mbalimbali, Wazazi wanaweza kufikia uamuzi wa kutoendeleza mahusiano lakini bado wakadhamiria kumpa Mtoto/Watoto wao malezi bora. Ni muhimu kuzingatia yafuatayo:

Mtoto apewe kipaumbele. Ni muhimu kuweka yaliyotokea na kuwepo jitihada kubwa katika kumpa mtoto au watoto wenu malezi na bora.

Mawasiliano. Pale unapozungumza na Mzazi mwenzio tumia lugha nzuri. Ni vema zaidi kuwasiliana moja kwa moja kuliko kufikisha ujumbe kupitia watu wengine.

Kusikilizana ni jambo la msingi baina ya Wazazi kwakuwa inasaidia pande zote mbili kusikika na kueleweka. Vilevile, pale ambapo Mzazi mwenzako anafanya jambo linalokupendeza, sio vibaya kumpongeza.

Wazazi ambao hawapo pamoja wanapaswa kuepuka kuongeza vibaya kuhusu wenzao kwa Watoto, au kuwaomba wachague upande wowote.

Zaidi >>> Co-Parenting: Tips, Creating a Plan, Things to Avoid, and More
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom