Malezi Mabovu..... Kosa la Wazazi au Jamii | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Malezi Mabovu..... Kosa la Wazazi au Jamii

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by VoiceOfReason, Feb 2, 2011.

 1. VoiceOfReason

  VoiceOfReason JF-Expert Member

  #1
  Feb 2, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 5,234
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 0
  Siku hizi imekuwa ni kawaida kuwalaumu wazazi / mlezi pindi mtoto anapokosa maadili, tukiangalia vizuri hata kama mzazi atakuwa anajua kulea kiasi gani mazingira yanachangia sana kumuharibu mtoto (we dont live in a vaccuum kwahiyo kama hata wako hajaoza wa jirani anaweza changia wako akaoza)

  • Zamani mtoto alikuwa sio wa fulani, ni wa jamii nzima kwahiyo popote anapokosa mtu yoyote alikuwa anamuadhibu (sasa people dont care)
  • Watu wazima wamekosa maadili sio role models (ufisadi mwanzo mwisho hakuna heshima)
  • Hivi serikali imeshindwa kuwachukua hao watoto wa mitaani wote na kuwaweka centre yenye ulinzi mkali ili wasitoroke na kuwapa elimu.... (this is a time bomb hivi hawa watoto ambao hawana elimu) wakija kuwa wakubwa watafanya nini.., hivi hatuoni au upeo wetu ni mfupi....? if you ask me hili ni janga kubwa its a time bomb
  Kwahiyo bila kurudi kwenye maadili yetu ya zamani.., kwamba watoto ni wetu wote na sio mtoto wa fulani hiki kizazi na kinachofuata kitakuwa cha watu wa ajabu sana, na kamwe mzazi hawezi kulea mtoto peke yake bila msaada wa jamii....,

  "We must learn to live together as brothers or perish together as fools. Martin Luther "

  Probably Babu na Baba Zetu ndio walikuwa walezi bora..., We are failing our Kids who will fail theirs, and I dont want to even think two generations from now.... Na hili sio la kwamba fulani kasema.... even though I dont have kids right now, lakini mimi wewe na yule we are all responsible for this.... I CHALLENGE ANYONE TO TELL ME OTHERWISE...
   
 2. Dena Amsi

  Dena Amsi R I P

  #2
  Feb 2, 2011
  Joined: Aug 17, 2010
  Messages: 13,137
  Likes Received: 255
  Trophy Points: 160
  Voice wewe acha tu Mtoto wa jamii?? Umpate wapi siku hizi??

  Dear jana mie nimechoka wakati narudi kazini naingia getini hivi kuna watoto wa jirani nao walikuwa wanashushwa na school bus sasa kwenda home housegirl katoka sijui kaenda sokoni au wapi sielewi maana wamegonga geti halijafunguliwa dah nilichokisikia toka kwa mtoto yule sikuamini mpaka leo nanukuu " Leo niko na stress zangu na dada ananiongezea" Nilichoka mind you huyo ni mtoto wa nursery school wala si primary kwa mtindo tunaelekea wapi??
   
 3. VoiceOfReason

  VoiceOfReason JF-Expert Member

  #3
  Feb 2, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 5,234
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 0
  Kweli kabisa.... hapo kama jamii ingebidi wewe uwaweke sawa..., huyo dada awazabe vibao na mzazi wao akija nae awakemee..., lakini sasa ukimgusa tu mtoto utaambiwa zaa wa kwako... lakini ubaya ni kwamba hata watoto wako hizi tabia za hao watoto zinawa-affect kwa njia moja au nyingine..., hivi kuna njia yoyote ya kuweza kuepuka hili janga au its too late
   
 4. NATA

  NATA JF-Expert Member

  #4
  Feb 2, 2011
  Joined: May 10, 2007
  Messages: 4,516
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Hakuna mtoto wajamii cku hizi. jamii yenyewe imeingiliwa na akina this no wazazi wanashindwa hata kuwonya watoto wao kwani wamejiengua kwa kushindwa kuwasialiana.

  Mzazi kanumba lugha haipandi mtoto mwingereza utawasiiana naye vp?

  Jamii imechanganikiwa kwa kifupi, hakuna chorus, kiitikio ziro
   
 5. VoiceOfReason

  VoiceOfReason JF-Expert Member

  #5
  Feb 2, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 5,234
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 0
  Lakini je unakubaliana na mimi kwamba haya makosa ni yangu mimi, wewe na yeye kwa namna moja au nyingine?
   
 6. NATA

  NATA JF-Expert Member

  #6
  Feb 2, 2011
  Joined: May 10, 2007
  Messages: 4,516
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Yawezekana!
   
 7. Chauro

  Chauro JF-Expert Member

  #7
  Feb 2, 2011
  Joined: Aug 20, 2010
  Messages: 2,969
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  kuna siku niliongelea hili jambo hapa ni kama watu wanaamini malezi ya mtoto ni ya mzazi pekee umeshawahi jiuliza muda gani unautumia kwa ajili ya mibangaizo ya maisha.na hawa watoto tunawaachia kina nani tusipokubali wakanywe na kulelewa na hawa tunaowaacha karibu yao.
  jamii yetu nayo imejaaa uozo, mkubwa kwa mdogo ni kuomba hekima ya Mungu tu.
   
 8. VoiceOfReason

  VoiceOfReason JF-Expert Member

  #8
  Feb 2, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 5,234
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 0
  Kinachosikitisha ni kwamba hapa tulipofika ni vigumu kujirudi sababu hata wazazi wa sasa ndio hao baadhi malezi yao yalikuwa yaleyale ambayo ndio wanatoa sahizi..., kuna jambo moja ambalo nilikuwa najisifia kwamba sisi tunalo na western countries hawana "MAADILI MEMA" lakini sahizi hata hilo hatuna..., kwa kweli sasa sioni kitu cha kujivunia ni uozo mtupu....
   
 9. Michelle

  Michelle JF-Expert Member

  #9
  Feb 2, 2011
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 7,364
  Likes Received: 196
  Trophy Points: 160
  Nakubaliana na wewe kwamba its a time bomb....hawa watoto tulipaswa tuwajibike kwao wote.....mtoto wa mwenzio ni wa kwako...matokeo ya huu ubinafsi wa kulea/kuelekeza wale walio wetu ni mabaya sana,kwakuwa hao watoto wa mitaani wakiwa wakubwa wataishi na watoto wetu ambao wana elimu na maisha mazuri pengine....wale wa mitaani watakuwa mizigo na taabu kwao....ndo haya mambo ya majambazi,wauaji,jamii iliyojaa frustrations na tension na ndiko wanakotoka watu wasiohofia hata kufa,wanajitoa muhanga as hawaoni thamani ya maisha.....ni jukumu letu sote kubadili hali hii,kwa manufaa yetu na ya kizazi kijacho.....tukishindwa tumeshindwa wote kama jamii na madhara yatakuwa kwetu kama jamii as tunaishi nao.
   
 10. Chauro

  Chauro JF-Expert Member

  #10
  Feb 2, 2011
  Joined: Aug 20, 2010
  Messages: 2,969
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  huwezi amini ni majuzi tu nilishuhudia kisa mtoto kaiba pesa kwa jirani jirani akenda kushtaki kwa mzazi badala ya yule mama kushukuru akaingia ndani kwa hasira akalipa ile hela halafu huku nyuma akaanza kumbembeleza mtoto na huyu ni msomi ana uelewa mzuri mtu wa mambo kwa kweli ilinisikitisha embu fikiria kizazi kinachozunguka hawa watoto wetu tunaotaka wawe na maadili mema kitakuwaje kama wazazi wenyewe hatukubali kukemea.

   
 11. M

  Marytina JF-Expert Member

  #11
  Feb 2, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 7,034
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  Kwa watoto waliochini ya mzazi flani kuharibika ni udhaifu wa huyo mzazi, wazazi wengine wanajifanya kuleta uzungu kwenye malezi kitu ambacho sio kabisa kwa mazingira yetu.(watoto hutofautiana tabia regardless wanasoma shule mmoja).During the holidays watoto wa ndugu husafiri kuja kwetu na kila mmoja anakatabia kake ila siku za kwanza nawacharaza mpaka wanakaa on line.KWA WATOTO WA MITAANI nakiri ni udhaifu wa jamii kwa ujumla kwenye malezi.
   
 12. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #12
  Feb 2, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Kwenye ulimwengu wa leo kumkemea/kanya mtoto wa mwenzio ni kosa zaidi ya alichofanya huyo mtoto!Wale ambao malezi yamewashinda ukifanya hivyo wanaona kama unawakosoa na hawataki!Kwahiyo kosa sio langu wala lako..ni la mzazi asiyetaka mtu mwingine asaidie kumrekebisha mwanae!Binafsi kama sio mtu wa karibu nakaa mbali kwasababu hata nikijaribu najua itanirudia!Worse mtu mwingine anaweza kuona mtoto wake amekosea kweli..ila kwasababu mtu baki ndo amekua wa kwanza kumuonya atareward lile kosa!
   
 13. VoiceOfReason

  VoiceOfReason JF-Expert Member

  #13
  Feb 2, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 5,234
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 0
  Je mzazi katika masaa 24 anakaa na mwanae masaa mangapi? kumbuka kuna shule, kucheza n.k. Hata ukiwa mzazi mwenye maadili kiasi gani kama jamii iliyokuzunguka yote imeoza ni rahisi kwa watoto kubeba tabia chafu kutoka nje...., na huwezi ukawa na full control sababu environment inachangia sana kwenye maadili ya mtoto...., kwahiyo mimi huwa sio mwepesi kuwalaumu mzazi mwenye mtoto sometimes mtoto anapotoka hata kama mzazi akiwa safi kiasi gani. Ingebidi kila mtu awe mlezi..., mtoto wako akija kwangu mimi inabidi nimfunze, akiwa shule mwalimu amfunze na tukiwa mitaani tukiona upuuzi inabidi tuukemee bila kuoneana aibu..., Lakini haiko hivyo sababu jamii sasa haikubali mwingine akemee mtoto wa mwingine..., kwahiyo collectively kama jamaa we have failed our children
   
 14. VoiceOfReason

  VoiceOfReason JF-Expert Member

  #14
  Feb 2, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 5,234
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 0
  Kosa ni letu sababu tumeacha hii kasumba iingie bila kufanya chochote wala kukemea....., hata tukiona meli ina tundu na inazama.., ingawa hakuna mtu ambae kazi yake ni kuziba tundu, lakini sababu wote tumekaa tu na kuangalia maji yanaingia..., boti itakapozama wakati tunatapapa..., we will all be the ones to blame, kwamba kwanini hakuna aliyechukua initiave ya kuziba matundu
   
 15. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #15
  Feb 2, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 589
  Trophy Points: 280
  Jamii na mazingira kwa ujumla ndio yana nafasi kubwa ya kumuharibu mtoto kuliko wazazi.
  Binafsi nimelelewa na mzazi mmoja na ni mzazi aliyekuwa busy sana. Kutoka asubuhi kurudi usiku, hakuwa hata na muda wa kuangalia madaftari wala kunichunga chunga zaidi ya kuhakikisha nimepata mahitaji yangu muhimu.
  Ila mazingira niliyoishi yalikuwa poa na jamii iliyonizunguka haikuwa na tabia za ajabu ajabu.
  Nafikiri jamii ingekuwa mbaya ningeharibikiwa.
   
 16. VoiceOfReason

  VoiceOfReason JF-Expert Member

  #16
  Feb 2, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 5,234
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 0
  Kweli kabisa, hatuwezi kumumlaumu mzazi / mlezi pekee

  Ingekuwa hivyo basi watoto wengi ambao walikuwa geti kali au wazazi wao ni wachungaji wangekuwa malaika....,

  Na je wale ambao watoto wapo boarding school ? mzazi pia alaumiwe...

  Kweli Hus ni kwamba nchi yetu imepoteza dira na hatujui tunakokwenda anymore
   
Loading...