Malezi kwa watoto wetu. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Malezi kwa watoto wetu.

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Msindima, Oct 30, 2009.

 1. M

  Msindima JF-Expert Member

  #1
  Oct 30, 2009
  Joined: Mar 30, 2009
  Messages: 1,018
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Wana Jf tusaidiane katika hili,hivi inakuwaje unakuta mama anam-miminia mtoto wake matusi mazito mazito,bila kujali nani yuko hapo na anasikia hayo anayomwambia mtoto wake,mada ya jana ya Calnde ilinigusa sana,kuhusu majina ambayo tunawaita watoto wetu,ninapoishi kuna jirani mmoja kwa kweli huwa ananikera sana,yeye saa zote ni kumfokea mtoto na kumtukana,na mtoto mwenyewe ni wa miaka mitano,hivi hii jamani ni sawa?Imefikia sasa huwa akimgombeza mtoto nae ana mjibu,vibaya mama yake,nakumbuka siku moja huyo mama alianza kumfokea huyo mtoto,kilichofuata hapo mtoto alimjibu mama yake,na yule mama hasira yake ndo ikapanda zaidi akaanza kumshushia mtoto kipigo,ilibidi niingilie kati nimwulize shida ni nini,akaniambia mtoto kamjibu vibaya,nilimwacha hasira zake zipungue ila mtoto nilimchukua nikambembeleza aliponyamaza nikaongea nae taratibu nikamwelewesha kuwa mama yake anapoongea asimjibu asikilize na pia kama amekosea awe anamwomba mama yake msamaha,nilipomaliza kuongea na mtoto nikamfata yule mama nikaongea nae nikamweleza kwa kweli sio vizuri kila siku kumkaripia mtoto maana hiyo inaweza kujenga hali fulani kwa mtoto na anaweza kuhisi kuwa humpendi akaniambia huyu mtoto ni mtundu sana na huwa hasikii nikamwambia pamoja na hayo hata kama amekukosea kaa nae mwelimishe kwa upendo maana bado akili yake haijakomaa kama unavyofikiri,sasa basi maswali yangu ni haya:
  je tunawajengea msingi gani tunapokua tunawatukana na kuwaita majina ya ajabu ajabu?
  Pili je ikitokea wewe ndo baba na mama anamtukana mtoto mbele yako na kumporomoshea matusi mazito utafanyaje?
  Na pia katika ile hali ya ukali ambayo wazazi wanaionyesha kwa mtoto ina athari zozote hapo baadae kwa mtoto?
   
Loading...