SoC02 Malezi bora kwa familia zetu

Stories of Change - 2022 Competition

Aidarus Ally

Member
Aug 18, 2022
8
7
Familia ni muunganiko wa baba mama na watoto lakini inaweza kuwa familia ya mzazi mmoja au ya namna nyingine, familia nyingi za kitanzania huhusisha ndugu mchanganyiko kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kufanya kazi.
Malezi ni kitendo cha kulea lakini malezi bora ni kitendo cha kulea katika misingi iliyobora na sahihi.

FAMILIA BORA
Hii ni ile familia iliyoundwa na watu wenye maadili mazuri ndani na nje ya familia.Maadili yanaanza kwa wazazi au walezi kisha kwa watoto ni ngumu sana wazazi wasiwape watoto wao malezi yaliyokuwa sahihi kisha watoto wakawa wana maadili,hivyo ujenzi wa maadili mzuri kwa watoto yanaanza kwa wazazi kwanza na kupelekea kupatikana kwa familia bora.


ASILI YA FAMILIA
familia yoyote ile muanzilishi wake ni mwanaume ambaye ndio baba wa familia,kwani yeye ndio mwenye kuamua pale anapoona amefikia wakati wa kuoa,basi anaoa mwanamke ambaye ndiye mama kisha baadae wanapata watoto na huo ndio mwanzo wa familia.


NAMNA NZURI YA KUJENGA FAMILIA BORA

(1) Uchaguzi sahihi wa mwanamke;

Miongoni mwa msingi mzuri wa kujenga familia bora ni pale tu mwanaume anapo taka kuanzisha familia basi azingatie uchaguzi sahihi wa mwanamke kwani Mama ni kitovu cha malezi ya watoto hivyo kama mwanaume akichagua chaguo sahihi litapelekea watoto kulelewa katika malezi bora lakini kama mwanaume ataoa tu ili mradi itaweza kupelekea watoto kukosa malezi bora na Kuwezesha kutopatikana kwa familia bora,hivyo kwa namna ilivyo mwanaume anatakiwa azingatie vizuri chaguo sahihi la mwanamme ambaye atakaye kuja kuwa mama watoto wake.

(2) Kuwalea watoto katika misingi ya dini;
Vilevile ili iweze kupatikana familia bora hapana budi wazazi au walezi kuwalea watoto wao katika misingi ya dini kwani kwa ujumla hakuna dini yenye kuharibu maadili bali dini zote zina amrisha kufanya mambo yaliyomema,hivyo kama mtoto mkristo basi atalelewa katika misingi ya kikristo au kama ni muislamu basi mtoto huyo atalelewa katika misingi ya kiislamu na dini nyinginezo,jambo likifanywa kwa na wazazi au walezi kwa usahihi basi kutapatikana familia bora sana kwa kuwa watoto watakuwa na hofu ya Mungu tangu wangali wadogo na sote tunatambua kwamba watoto ni taifa la kesho,yaani mtoto mwema wa leo basi ni mzazi wa kesho,hivyo wazazi na walezi wajitahidi sana kuwapatia watoto malezi sahihi.

(3) Kuwachagulia marafiki wema watoto zetu
Pia katika mambo muhimu ni uchaguzi sahihi wa marafiki kwa watoto zetu,kwani iwapo watoto wakichangamana katika michezo au kwa namna yoyote na watoto wenye tabia mbaya basi watoto hao inakuwa rahisi na wao kuiga tabia za marafiki zao,hivyo ni muhimu kuwaambia watoto wachague marafiki wenye tabia nzuri ila vizuri zaidi mzazi akawa anawaelekeza watoto ni marafiki gani wakucheza nao na ambao sio wakucheza nao,ili kuendelea kuwa katika mstari ulionyooka.

(4)Walezi kutoonesha tofauti zenu kwa watoto;
Hii inaweza kutokea pale walezi ambao ni baba na mama kutofautiana kwa namna yoyote,kisha kujaribu kuonesha tofauti zao kwa watoto,suala hili si zuri kwani litajenga chuki kwa watoto na hata kupelekea mpasuko na watoto kudharau mlezi mmoja wapo,hivyo ni muhimu walezi kutoonesha tofauti zao kwa watoto ili waweze kuwa na tabia njema.


HASARA ZA KUKOSA MALEZI BORA KWA WATOTO

(1)Kuwepo kwa mmonyoko wa maadili ;

Watoto wanapokosa malezi bora kutoka kwa wazazi au walezi huweza kusababisha mmomonyoko wa maadili kwenye familia na hata kwa jamii pia,watoto kutoshimu wakubwa zao na kujiingiza katika tabia mbaya ya wizi,uporaji,na matumizi ya pombe kali.

(2) Kutotambua wajibu wake kama mtoto;
Malezi bora yanapokosekana hupelekea mtoto kukosa kutambua wajibu wake hasa ni upi,kama vile kuhakikisha anasoma kwa bidii,ana wasaidia wazazi wake shughuli ndogondogo,yote hayo kama hatopata malezi bora ataona ni mzigo mzito na hatoweza kuyafanya.


UHUSIANO WA FAMILIA NA JAMII

Kuna uhusiano mkubwa kati ya familia na jamii,kwani jamii ni mkusanyiko wa familia mbalimbali ambazo zinaishi katika mazingira maalumu,kama vile jamii ya wafugaji (kuna wafugaji wa familia tofauti tofauti ambao wanaunda jamii inayoitwa jamii ya ufugaji) basi mienendo ya familia ni msingi mzuri wa utambuzi wa jamii husika,hivyo kama familia zitakuwa na malezi bora ambayo yatapelekea tabia na mwenendo mwema kwa watoto hata na jamii itakuwa na muonekano mzuri katika suala la malezi na tabia njema,hivyo ujenzi wa jamii huegemea namna ya familia zilivyo katika jamii husika.


MALEZI YA MAMA KWA WATOTO WAKE

Katika suala la malezi mama ni nahodha, yeye ndio mwenye kuwaongoza watoto na kuwapa malezi bora,hivyo inatakiwa mama kupata muda wakutosha kuwalea watoto hata kama si mama wa nyumbani kwa kusoma mienendo ya watoto wako,njia itakuwa rahisi kubaini ni mtoto yupi anaenda kinyume na mtoto yupo yuko katika njia ya sawa,na kuwapa maneno mazuri watoto kwani itawajengea utambuzi wa maneno yanayostahili kusemwa na yasiyo stahili.


USHIRIKIANO BAINA YA MAMA NA BABA KATIKA MALEZI YA WATOTO

Licha ya kuwa mama ni kitovu wa malezi bora kwa watoto lakini pia baba ana paswa vilevile kwenye suala la malezi kwa kushirikiana na mama watoto kama vile kucheza na watoto na kuwatembeza maeneo mazuri kama kwenye vivutio na sehemu nyinginezo.


HITIMISHO;
Malezi bora ni suala muhimu sana kwa familia na jamii zetu kwa ujumla na ili yaweze kupatikana malezi bora basi angalau kwa uchache yawepo mambo hayo manne niliyo yazungumzia.
 
Back
Top Bottom