Malengo yangu mwaka ujao!

No Escape

JF-Expert Member
Mar 7, 2016
6,664
7,728
Muda sio rafiki wa binadamu hata siku moja Mwenyeezimungu alituumba sisi tuishi kwa wema bila kutendeana maovu,tuheshimiane ili kuweza kutekeleza malengo yetu ya kuumbwa hapa Duniani. Kuanzia mwaka ujao hawa watu nitakua nao mbali sana kwa njia yeyote:
1.Wanawake wasiojitambua_ Hawa watu wamefanikiwa kunirudisha sana miaka 5 iliyopita naamini ningekuwa nao mbali ningekuwa zaidi ya hapa nilipo.
2.Ombaomba_Sasa hivi kuna lindi la watu katika jamii yetu hawataki kufanya kazi,wao ni kupiga mizinga kwa kwenda mbele.
3.Marafiki wanafiki_Yes hili nimelianza muda sana,najua kabisa jinsi unavyoongeza marafiki ndivyo unavyoongeza maaadui mimi nimeanza kuwachuja!
SIKU ZILIZOBAKI KUMALIZA MWAKA NI CHINI YA HAMSINI HATA INGEKUWA PESA HAITOSHI HATA KUNUNUA ANDAZI...TUSHARE PAMOJA MAWAZO,JE WEWE UNA MALENGO GANI? J.PILI NJEMA TUSOGEE IBADANI MUDA HUU.
 
Mwakani kwangu.
1. Kujibana na kujipanga.
(4:4:2 au 4:1:4:1 au 5:4:1)
2. Upweke nimeuchoka
Mwakani nafanya kweli. Nitatafuta wakuyajenga naye
3. Naunga hoja yako namba 3.
 
Mi natembea kidogo kidogo nikinyata, kukamilisha malengo yangu ndani ya miaka 5 kuanzia sasa.
 
nimejitahid kuacha pombe na naiman mwakan ntakuwa nimeacha rasmi nguvu zangu zote ntaendelea kuelekeza kwa muumba! Suala la kuoa ndio litaanza kufikiriwa mwakan panapo majaliwa! Mwisho mafanikio ya mwana JF yoyote ni yetu sote! Nawatakia mafanikio mema! Mungu awawepesishie mafanikio!
 
Hebu tumalize mwaka kwanza inawezekana mwaka huu ukaendelea ili JPM aendelee madarakani
 
Nani kauona mwaka?nani kamakiza mwaka? Nimajaliwa yake Mungu wee kuona mwakaa(hayo maneno ya Msondo).Tuombe Mola ayatimize yaliyopo moyoni mwetu mana kupanga jambo 1 na kutekeleza jambo lengine.
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom