Sella turcica
Senior Member
- Oct 13, 2020
- 104
- 193
Habari wanabodi, sote tunajua ukizungumzia mpira wa Tanzania basi unazungumzia Simba na Yanga. Kwa miaka minne mfululizo timu ya Simba imefanikiwa kutawala soka la Tanzania kwa kubeba ubingwa mara 4 mfululizo na sasa imejikita zaidi katika michuano ya kimataifa.
Katika kipindi hicho malengo ya Yanga yalikuwa kuifunga Simba. Yani hata wakikosa ubingwa sawa, ilimradi mtani amekufa. Msimu huu naona wamejipanga kwelikweli na sioni cha kumzuia Yanga kuchukua ubingwa, labda kumzuia kuchukua bila kupoteza mchezo.
Lakini perfomance ya Yanga kwa upande wa kimataifa imekuwa sio nzuri. Mimi sijui historia sana ila hii timu huwa inatamba hapa nyumbani tu, ikitoka nje ya mipaka ni aibu tupu.
Challenge waliyo nayo sasa ni kufanya vizuri kimataifa. Tuachane na kufika robo fainali kama ambavyo Simba ilifika msimu uliopita, angalau wafuzu kuingia kwenye hatua makundi.
Timu iliyoanzishwa mwaka 1935 haitakiwi kuishia kuwaza kuwa bingwa wa ligi kuu bara pekee, inatakiwa iwaze kupambana na miamba mingine ya Africa na dunia kwa ujumla.
Ubingwa msimu huu watachukua, swali ni je, watafika makundi au ndo yale yale kufungwa nyumbani na ugenini? Naamini muda utatupa majibu.