Malecela: Tanzania itakuwa ya 11 kiuchumi duniani miaka 20 ijayo

Huwaga inaniwia vigumu sana kuamini kitu chochote kinachosemwa na mtu au kiongozi wa CCM.....................huwa wanaropoka tu bila ya kuweka evidence
 
Hata growth rate yetu sasa hivi ingekuwa 20%(sasa hivi ni 7%) bado hatungeweza kuipita nchi kama Canada baada ya miaka 20.

Poor Sod...Barrick Gold ndio wanaanza kufunga virago Malecela ndio anaanza kuota!
 
Mimi nadhani sipo peke yangu katika kutafuta undani juu ya uhuni wa Malecela uliopelekea kulazimika kujiuzulu mwaka 1994. Kama una ufahamu wowote juu ya uhuni uliozungumzwa wakati ule, kindly share;

Kwa definition ya uhuni, kitendo cha yeye kugombea/kugombewa na wanawake wale wawili wa CCM, tayari alikuwa mhuni!!
 
Mzee Malecela amekuwa katika uongozi wa nchi hii kwa muda mrefu. Je, ameacha legacy gani mpaka ifikie mahali sasa tunamualika kwenye vipindi vya TV kutupa mawaidha yake?
 
Mzee malecela amesema kwa mujibu wa magazine moja linalochapishwa marekani, Tanzania itakuwa ya 11. Aliisoma magazine hii akiwa Marekani (hivi karibuni) hajasema lini.

Hiyo magazine ilisema miaka 20 ijayo, China itakuwa ya kwanza ikifuatiwa na India, ya tatu Marekani na Tanzania Ya 11. Amesema Tanzania ni ya 3 Africa kwa utoaji dhahabu, Soda ash ni ya pili Duniani baada ya Marekani, Makaa ya mawe tunayo mengi sana.

SISI SIYO MASKINI!..

Source: Dkk 45, ITV
eti eeeh
 
uyu mzee anazeeka vibaya...hahahahaha anawaza mia wakat uwezo wa kupata 5 hana!
 
Bila shaka kwa maswali haya hata wakiulizwa wachumi wa enzi zetu hizi ni lazima watatofautiana majibu. Mimi naona Babu alijitahidi ingawa inaelekea arguments zake bado zinatakiwa kutazamwa kwa mtazamo wa Kimagamba zaidi.
 
Hata mimi nilimsikiliza, awali nilidhani amechemka ila baada ya kutafakari kwa kina nikagundua ilikuwa ni lazima ajibu kwa kiwango kile ili wale watu wa kijijini kabisa waelewe vizuri kwanini kunamfumuko wa bei, maana angeingiza concept za uchumi kama anajibu mtihani asingeeleweka na walio wengi, hata Gavana alipohojiwa kuhusu ishu hiyo, alijibu kwa kiwango cha mtu wa kawaida kabisa kuelewa. Nakubaliana na wewe kabisa kuwa angejibu kisomi ila wangapi watailewa.
 
There is some light in his argument, but tatizo letu tunaanza na negativity or denial then build from there badala ya kuangalia suala zima objectively kwanza kwani regardless of the source, kama kigezo ni GDP forecasts, sioni ajabu yoyote Tanzania kuwa the 11th largest economy by 2030; Kama calculations zimetumia OUTPUT METHOD ambapo kinachotazamwa ni just the value of goods and services produced in a country, his statement can hold water.

This method takes into account bidhaa na huduma zote zinazo zalishwa ndani ya uchumi wetu katika kipindi cha mwaka mmoja; This includes output ya all FDIs – mining, oil, gas, na hata huduma za kibenki kwa sekta za oil, gas, mining n.k. Given resources tulizokuwa nazo Tanzania, sio ajabu in 25-30 years tukawa 11[SUP]th[/SUP] largest economy in the World.

Note – hapa welfare ya wananchi haipo katika mahesabu i.e. the issue of the said growth to trickle down to the rural mass isn’t taken into account;

Kuufikia ukweli kwa kuanzia in the middle i.e being objective ni rahisi zaidi kuliko kuanza kuangalia ukweli ukiwa tayari umeegemea to the left or right; ni vizuri mara nyingine tukatazama mambo kama haya bila ya kuweka negativity upfront kwanza, kwani ujenzi towards the truth utakuwa wa taabu sana;


Sidhani hapa kama kuna negativity in the comments of the people but people are disturbed and confused by the man of that caliber to give such a narrow conclusion. Kwanza that dosctrine of no research and no right of speech has been sabotaged maana magazine moja isiyokuwa na jina haiwezi ikawa na reliability. Utafiti hauwezi kutegemea kijarida kimoja na siku zote unakuwa fair enough kutaja reference hiyo na mwandishi/waandishi wake. Hoja hiyo ingetolewa na mtu ambaye sio wa CV ya Maricela wala tunachoongea tusingekuwa tunakiongea. Lakini yeye kwa nyadhifa alizopata, shule alizosoma kwa gharama ya walipa kodi na kiinua marupurupu anayopata ambayo yamwezesha kusoma vitabu, majarida na kukutana na think tanks hatutegemei atoe shallow conclusion kama hiyo. Halafu haya ya GDP umesema wewe maana yeye hakusema kama argument yake was based on GDP. And if we concur with what you have analysed yet wananchi hawataki kusikia maendeleo ya uchumi yasiyowagusa ya mashimo makubwa ya madini, mahekalu kila kona, mahoteli makubwa wasipoweza hata kusogelea wao wanahitaji simple equations that touch their daily lives- clean, safe and reliable water infrustructure, good houses built in safe landscapes, barabara passable for all weather conditions, shule/skuli zisizo na chembe ya ubaguzi na zenye standards and quality to be called schools but not pretense of schools or an abolition, viwanda vya kutengeza bidhaa inayotumika katika viwanda vingine, huduma za afya that are affordable, reliable and of high quality and mengine mengi that ensures them to be consumers and enjoy bread and butter. Kinyume chake huo sio uchumi wala maendeleo hata kama defintion inatoka kwa Keyns na Tailors
 
Mzee malecela amesema kwa mujibu wa magazine moja linalochapishwa marekani, Tanzania itakuwa ya 11. Aliisoma magazine hii akiwa Marekani (hivi karibuni) hajasema lini.

Hiyo magazine ilisema miaka 20 ijayo, China itakuwa ya kwanza ikifuatiwa na India, ya tatu Marekani na Tanzania Ya 11. Amesema Tanzania ni ya 3 Africa kwa utoaji dhahabu, Soda ash ni ya pili Duniani baada ya Marekani, Makaa ya mawe tunayo mengi sana.

SISI SIYO MASKINI!..

Source: Dkk 45, ITV
Huyo mzee kama alieleza kuwa utabiri wa hiyo magazine, ulieleza kuwa after 2015, nchi itaendeshwa na chama kingine na siyo CCM, angalau kidogo madai hayo yangeweza kuingiaingia kichwani. Kwanza imagine hata kama hiyo magazine imetabiri hivyo kwa kuzingatia ugunduzi mkubwa wa gesi na mafuta nchini kwetu, lakini uongozi huo huo wa magamba ndiyo tunaambiwa tayari weshahongwa mabilioni ya pesa na hayo makampuni ya kuchimba gesi na mafuta na kuyaficha kwenye mabenki ya uswisi, hivyo kwa mazingira hayo, unategemea muujiza gani wa uongozi wa design hiyo, kututoa kutoka among 10 poorest countries in the world, na kuwa among 12 richest countries in the world!! Huo utakuwa moja ya miujiza mikubwa kutokea duniani, tokea kuumbwa kwake!!
 
Mhhh yaani tuwe wa 11 kwa uchumi bora baada ya miaka 20?China,India,USA;Japan,UK,Germany, Sweden,Norway,Denmark,UAE;Tanzania then zinafuatia Uholanzi,Italy,SA,Brazil,Ureno,Spain;Uswisi;France,Finland,Luxemborg na zinginezo au??(Jamani pangeni wenyewe hizo nchi na TZ iwe ya 11 ahahahaha)

Ahahahaha Malecela bana!yaani wana siasa wetu wana vituko kama tu ma dr wa Muhimbili!Hata kama tutakuwa na potential za uhakika TZ haiwezi kuwa nchi ya 11 kwa uchumi bora duniani baada ya miaka 20 tu!Wanao ongoza kwa uchumi bora duniani waliutengeneza uchumi wao kwa zaidi ya miaka hiyo Malecela aliyotaja!
 
Sidhani kuwa nawaabisha wazee. Wazee wengi wana busara sana. Kuna vijana wengi ambao hawana akili kupita hata hyo Mzee malecela.

Akili haizeeki kiasi ya kwamba mtu kusema utumbo tu. Hawa ni wazee ambao walipata hivyo vyeo kwa kuwa ndiyo walio onekana wamesoma, enzi hizo. Binafsi sikuwahi hata siku moja kumsikia Malecela akisema point hata enzi za ujana wake.
 
huyu mzee anazeeka vibaya..ama hamjui?

hamjamuelewa alikuwa anazungumzia utajiri wa viongozi wa serikali, ambayo itakuwa inapandishwa kila mwaka, na wafanyakazi wengine mkigoma dawa wanayo si mnawaona madaktari? Hicho ndicho alichokisema ndugu malechela, samahani sikumwita mhe kwani hajawahi kuifanyia kitu cha maana tz
 
Back
Top Bottom