Malecela: Tanzania itakuwa ya 11 kiuchumi duniani miaka 20 ijayo

tenende

JF-Expert Member
Jan 10, 2012
6,511
500
Mzee malecela amesema kwa mujibu wa magazine moja linalochapishwa marekani, Tanzania itakuwa ya 11. Aliisoma magazine hii akiwa Marekani (hivi karibuni) hajasema lini.

Hiyo magazine ilisema miaka 20 ijayo, China itakuwa ya kwanza ikifuatiwa na India, ya tatu Marekani na Tanzania Ya 11. Amesema Tanzania ni ya 3 Africa kwa utoaji dhahabu, Soda ash ni ya pili Duniani baada ya Marekani, Makaa ya mawe tunayo mengi sana.

SISI SIYO MASKINI!..

Source: Dkk 45, ITV
 
Katika interview iliyokuwa inarushwa na ITV leo, Mzee Malecela aliulizwa na mtangazi kuhusu inflation inavyomgusa Mtanzania. Kwa kweli it was very poor analysis for a person with such extensive CV.



John Malecela is one of the most experienced Tanzanian politicians. However his efforts to seek his party's nomination for presidential candidacy did not yield any favorable results on his part both in 1995 and 2005.
[h=2]Positions held[/h]
  • Tanzania Permanent Representative to the United Nations - 1964-1966
  • Tanzanian Ambassador to Ethiopia and the OAU - 1967
  • Minister of Foreign Affairs - 1972-1973
  • Communication and Transport - 1973-1974
  • Mineral Resources and Agriculture 1975-1975
  • Minister in the East African Community - 1975-1976
  • Regional Commissioner of Iringa - 1980-1984
  • Member of the Group of Eminent Persons of the Commonwealth on South African situation - 1985
  • Tanzanian High Commissioner to the United Kingdom - 1989-90
  • Prime Minister and First Vice President 1990-1994
  • Vice Chairman of the ruling Party, Chama cha Mapinduzi (CCM) - 1995 to 2007
  • Member of Parliament for Mtera - 1990 - 2010
 
Magazine gani isiyo jina hiyo? Hebu tutajieni watu tuna ma Lexisnexis tupeni mpaka issue number tuangalie ubunifu gani huu unaongelewa.
Unajua tena kipindi chenyewe recorded, na Muongozaji amemuacha mzee bila kutaja hiyo magazine wala kutoa maelezo tutafikaje huko!.
 
kati ya watu walioongea bila point ni huyu mzee wangu. nilivumilia sana kuangalia kipindi chake tangu mwanzo hadi mwisho. hakuna hata point aisee, ndo maana tunasema hii nchi inatakiwa kuongozwa na vijana, wazee hawana kitu aisee, amekuja tu kuwaaibisha wazee wenzie kuwa ukizeeka mwili hata akili inazeeka.
 
Haa haaa,hajajua hayo ni maneno ya wazungu ili waendelee kutuvuna ..........sifa nyingine si za kubweteka nazo!
 
Mkuu labda ungeelezea hiyo iterview na alichemka maeneo yapi,by the way mzee kashazeeka bhana
 
ukiwa na rais kama huyu, nchi inaweza kurudi kwenye zama za ujima. hivi mzee kumbe huwa namheshimu nikijua kuwa anao uelewa wowote wa namna ya kuikomboa hii nchi, kumbe hamna kitu kabisa aisee, sijui uzoefu wake wote ni diplomasia za kirussia zinazowafanya watu wawe mambumbumbu kwa kudanganywa kwenye chama chake....nimepoteza muda kuangalia kipindi kile aisee.
 
You scratch my back, I scratch your !!!!!

Tutasikia mengi sana mpaka kufika uchaguzi wa 2015.

Nitafutie atlas niione Tanzania anayozungumzia Mzee Malecela.
 
Sishangai Tz kuwa ya 11 kiuchumi duniani miaka 20 ijayo kwa sababu CCM wakati huo itakuwa kaburini kwa miaka 17. Kifo cha CCM ndiyo nusura ya taifa hili, eleweni hili ndugu zangu! Baada ya kifo cha CCM tunahitaji miaka 15 tu tukiwa chini ya serikali yoyote makini (kama ya Kagame) kuushangaza ulimwengu kiuchumi na maendeleo!
NAUNGA MKONO HOJA!
 
Malecela once again has proved kwamba nje ya Sokoine na Nyerere, Tanzania haijawahi kuwa na Waziri mkuu mwingine mwenye uwezo wa kiuongozi kama mzee huyu; I remain to wonder mambo mawili:

1. Uhuni wake ambao tuliambiwa ndio ulipelekea ashinikizwe kujiuzulu ulikuwa ni uhuni wa namna gani? Wengine tulikuwa wadogo kuelewa mambo kwa undani;

2. Ingetokea Malecela akawa Rais wa tatu au wa nne wa Tanzania, angefanya kitu gani tofauti?
 
alinichosha na nikabadili stesheni aliposema tatizo letu ni kuwa tuna rasilimali ilahatuna mtaji wa kuzibadili zile rasilimali kuwa bidhaa. anasema wasukuma walikuwa wanachimba vyoo kwenye alimasi. akaongezea kuwa alipokuja mzungu akachukua almasi na kuifanya kuwa bidhaa. sasa hajasema kwa nini mpaka sasa wasukuma ni masikini?
huyu mzee anazeeka vibaya.
 
Unajua tena kipindi chenyewe recorded, na Muongozaji amemuacha mzee bila kutaja hiyo magazine wala kutoa maelezo tutafikaje huko!.

Bongo watu wanaigiza tu.

Wanahabari si wanahabari hasa, wanaigiza tu kama wanahabari.

Wanasiasa nao wanaigiza tu kama wanasiasa.

Mtu habari nyeti kama hii kwa nini muendesha kipindi asimbane tupate uhakika zaidi?

Mwishowe tutauziwa hadithi ziso mwisho, ikifika miaka 20 tutaambiwa miaka 20 mingine mpaka watu wanakufa.
 
Miaka hamsini ya kujitawala tupo kumi bora ya fukara wa kutupa duniani. Mzee wa watu ama anajifurahisha au doing substance abuse.
 
Back
Top Bottom