Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,675
- 40,555
Kama kuna kiongozi katika CCM ambaye kwa haki angeweza kulia na kulalamika mbele ya wananchi na kuandaa waandishi wa habari wamsafishe na kujijenga upya ni Mhe. S. J. Malecela (Mtera - CCM). Mzee Malecela ni moja wa wa viongozi ambao siyo tu wameitumikia Tanzania kwa muda mrefu lakini pia amewahi kushika nafasi nyingi za juu ukiwemo Uweziri wa Mambo ya Nje na juu kabisa ni Uwaziri Mkuu. Kwenye chama alifikia kuwa Makamu wa Mwenyekiti Taifa (Bara) kwa muda mrefu tu.
Hata hivyo mara kadhaa katika njia yake ya kisiasa amejikuta akikutana na kila aina ya magogo na mahandaki ambayo mengine aliweza kuyahamisha lakini mengine alikubali yamemzidi kimo, au kwa hekima akayapa ushindi wa kimkakati.
Mojawapo ya matukio ambayo yanakumbukwa sana na kugongana kwake na Mwalimu Nyerere ambako inadaiwa kulichangia kwa kiasi kikubwa kuvuruga nafasi yake ya kuwa mgombea wa CCM mwaka 1995. Chochote kilichotokea na licha ya uwezo wake wa kumwambia Nyerere ukweli pasipo haya Malecela hakuwahi kusimama na kumshambulia Nyerere au kwa namna yoyote ile kumfanya awe duni mbele ya wananchi. Alikubali kushindwa mbele ya Nyerere lakini aliendelea kulitumikia Taifa lake na wapiga kura wake.
Na hata baadaye tena alipojaribu kupata nafasi ya kumrithi Mkapa na licha ya madai kuwa alimzunguka Mkapa na kutangaza nia yake ya kugombea bado aliamini ana mvuto mkubwa kwa chama. Mvuto huo ambao unadaiwa ni wa kweli na si wa masikhara nusura umpatie ushindi kwenye mchakato wa kutafuta mgombea. NI mpaka pale Mkapa alipofanya kile kinachoitwa "Mizengwe" ndipo jina la Malecela likachomolewa na majina mengine yakapita.
Kitendo cha jina lake kuenguliwa na kunyimwa nafasi ya kuletwa kwenye Halmashauri Kuu ya Taifa (ambako inadaiwa alikuwa na nguvu sana) siyo tu kilimuumiza lakini kilimkera hasa. Hata hivyo kwa mara nyingine hakusimama hadharani au kwa wapiga kura wake (ambao walimchagua kwa zaidi ya asilimia 90) kuanza kulalamika kuwa "alionewa na hakupewa nafasi ya kusikilizwa". Alikubali na kuendelea na nafasi yake hadi pale alipokuwa tayari kuachia Umakamu na kubakia mbunge wa kawaida. Na kwa hakika baada ya kuzidiwa kete na mtandao, Malecela hakusimama kuanza kuonesha upinzani wa wazi dhidi ya Kikwete. Hadharani mara zote amekuwa akimuonesha heshima ambayo sitashangaa itazawadiwa muda si mrefu.
Ninafahamu, pembeni ambako akiwa na marafiki, ndugu na watu wa karibu ana maneno hasi ambayo anaweza kuyaelezea kuhusu kuenguliwa kwake na matukio ambayo anajua si ya haki. Hata hivyo hajaingia kwenye rekodi kusema mambo hayo na wananchi wakayasikia. Yeye kwa hakika ni kada mzuri wa chama kwa uzuri na kwa ubaya.
Hata hivyo, kwa upande wa Lowassa hilo ni kinyume naye. Matukio yaliyofuatia kujiuzulu kwake yamethibitisha kitu kimoja; Lowassa anaamini kuwa anastahili kuwa kiongozi wa ngazi za juu na ya kuwa hakuna mtu yeyote ambaye anaweza kumzuia na yuko tayari kufanya lolote lile kujijengea jukwaa la kujisafisha.
Lowassa siyo tu ameamua kujisafisha lakini ni wazi kabisa ameamua kuchallenge siyo tu nguvu ya Rais bali pia chama chake na kwa hakika Bunge la Jamhuri ya Muungano. Kwa mtu mwenye jazba kama Lowassa neno hekima na busara viko mbali naye na hisia za kisasi na kustahili zinamuongoza.
Ni kwa sababu hiyo kabla ya kutumiwa ujumbe hivi juzi, ujumbe uliokuwa loud and clear alikuwa ameaanda mkakati wa "full throttle" wa kuchallenge maamuzi ya Bunge, ukimya wa Rais kumtetea n.k Na zaidi alifikia uamuzi huo baada ya kuamua kutomjulisha Rais kuwa anaenda kujiuzulu hadi pale Rais aliposikia kwenye TV kama Watanzania wengine.
Kitendo chake kile kilikuwa na lengo la kumtangazia Rais Kikwete kuwa "urafiki" wao umefikia kikomo na kwa vile JK hakuweza kumtetea kwenye CCM na kwa vile licha ya JK kukataa kuingilia kati ripoti ya Mwakyembe na kukataa kuiona kabla, ni wazi kuwa EL anaamini kabisa kuwa kuanguka kwake kisiasa kumehusishwa kabisa na maamuzi ya kutofanya lolote ya JK.
Lowassa siyo tu anataka kurudi katika uongozi bali pia anaandaa kisasi; kisasi ambacho kitaonekana zaidi siku zijazo ambapo Rais Kikwete anatarajiwa kufanya mabadiliko makubwa ya wakuu wa mikoa na wilaya akizingatia kile kinachofanyika Kyela kuhusu Mwakyembe.
Siyo hivyo tu, mkakati wa Agenda 21 sasa hivi ni kupitia Bungeni ambapo baadhi ya wajumbe wa Kamati Teule ambao na wenyewe walipata mikopo toka Benki Kuu hata kama ni ya halali kiasi gani wamewekwa kwenye shabaha ambapo na wenyewe watatajwa kuhusika na "ufisadi". Lengo ni "mmetuchafua, tutawachafua". Mbinu hii ya Kibunge itaonekana siyo kwenye kikao kijacho tu bali kile cha bajeti pia ambapo msishangae kuona Kamati Teule inaundwa kuhusu BoT ili iende kunasa wengine.
Hivyo, ni wazi kuwa licha ya wanasiasa hawa wawili kukabiliwa na mitikisiko mikubwa ya kisiasa ambayo imetishia maisha yao ya kisiasa, ni wazi kuwa wameamua kufuata njia mbili tofauti njia ambazo zimemfanya Malecela kuendelea kuwa mzee anayeshimika ndani ya CCM na Lowassa kuwa ishara ya kuangaliwa na jina la kutolewa mfano!
Endapo Lowassa hataweza kukaa chini na kutulia busara na hekima katika kushughulikia mgongano wake na JK ajue kabisa kuwa anajitengenezea mazingira siyo tu ya kukataliwa na wana CCM wenzake bali pia kuonekana mbele ya wananchi kama adui wa Rais. Sidhani kama anataka hilo la pili kwani licha ya matatizo mengi yaliyopo Tanzania watu wengi bado wanamhusudu na kumheshimu Rais Kikwete (licha ya madhaifu yake mengi ya kiuongozi)kama Rais Halali wa Jamhuri yetu.