Malecela: Msinigombanishe na Serikali(BABU AOGOPA MPUNGA)!!!

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
52,883
25,249
[LEFT Malecela: Msinigombanishe na Serikali


Na Kulwa Mzee, Dodoma

MBUNGE wa Mtera, Bw. John Malecela (CCM), amewasilisha
hoja binafsi bungeni huku akivijia juu baadhi ya vyombo
vya habari kwa kutoa habari zenye lengo la kumgombanisha
na Serikali.

Akitoa hoja hiyo jana bungeni, alisema upotoshaji huo ni wa
kitoto na usio na nia njema kwa nchi.

Bw. Malecela alisema alipoomba taarifa ya Kamati ya Rais ya Kuishauri Serikali kuhusu madini ijadiliwe na wabunge, alikuwa na nia nzuri na kwamba madai ya baadhi vya vyombo vya habari kuandika kuwa anaitega Serikali ni ya kichochezi.

“Huu ni upotoshaji mkubwa wa nia nzuri niliyokuwa nayo ya
kuliwezesha Bunge kuijadili taarifa hiyo kwa kina, ili
Taifa lipate sera na sheria ya madini bora,” alisema.

Mbunge huyo alisema Rais Jakaya Kiwete aliunda kamati
hiyo kwa nia njema ya kuitafutia sekta ya madini ufumbuzi wa kudumu wa matatizo mbalimbali ya kisera na kisheria iliyonayo.

Alisema uundaji huo wa kamati ya madini ni sehemu ya
utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ambayo inatamka kuwa Serikali ya CCM itapitia upya sera ya madini kwa lengo la kuiboresha katika maeneo mbalimbali.

Alisema uamuzi aliotoa Naibu Spika, Bibi Anne Makinda wa kulipa suala hilo muda maalumu kulijadili ni mzuri na wenye
tija kwa Taifa.

"Tafsiri kwamba hatua hii ni mtego kwa Serikali ni porojo,
na upotoshaji wa kitoto usio na nia njema kwa nchi yetu,
niliona niutolee maelezo mbele ya Bunge hili Tukufu,” alisema Bw. Malecela.
Tuma
 
Dk. Migiro atua Dar kwa mapumziko

2008-07-19 08:57:17
Na Mwandishi Wetu

Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Dk. Asha-Rose Migiro yuko nchini kwa mapumziko.

Dk. Migiro aliwasili jijini Dar es Salaam juzi na kulakiwa na Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa Bw. Oscar Fernandes Taranco, Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. Bernard Membe, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Bw. Abbas Kandoro, baadhi ya wafanyakazi wa ofisi za UN nchini pamoja na familia yake.

Naibu Katibu Mkuu huyo wa kwanza mwanamke kutoka Afrika, anatarajiwa kushiriki kwenye majukumu mbalimbali ya hisani yanatakayofanyika Bara na Visiwani.

Leo Dk. Migiro anatarajiwa kukutana na wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari.

Akiwa nchini, Dk. Migiro atashiriki uchangiaji wa fedha kwa ajili ya shule za Zanzibar pamoja na mikoa ya Dar es Salaam na Pwani.

* SOURCE: Nipashe
 
Analinda Mpunga Wake Jamani Inasemekana Hata Humo Ndanisiku Mama Akimwaga Sumu Akkaliki Anamgombeza Kweli Watatuua Hawa Darling
Tutakufa Bila Kuaga Sweetheart Wangu!!!!

Kazi Ipo
 
kuna mtu ana taarifa kuhusu vijana ambao baadhi ya matokeo ya masomo yao hayakuonekana hapo UD kwa Mkandala?Huo ni uzembe wa hali ya juu na sijuii nini hatima yake?
 
Back
Top Bottom