Umeniwahi. Jana usiku nilikuwa nimeanza kucaha thredi mpya John's Legacy, nikapata wageni nikajisemea kesho (leo) nitaandika.
Wasifu wa John Malecela ni mkubwa sana kuliko kiongozi yeyote wa kale na wa sasa aliyeahai. Ukiondoa Uaris wa Mwinyi na Mkapa, wote wawili hawamfikii huyu kwa utu wake na mapenzi kwa Taifa!
Kwanza ni mkweli ambaye hakuogopa kusema ukweli wake wa moyoni hata kama uliudhi na hata kumfanya apoteze madaraka. Alipotoa lile tamko la kuenda kuzimu, ilikuwa ni mara ya kwanza kwa Watanzania kumsikia mwenzao ambaye ni kioongozi kutamka hadharani bila woga. Jee alichokikosea kilikuwa kipi? ni kutamka ukweli kwa ukali kuwa kama wasipoweza kujisaidia ni heri waende ahera? Sawa na Msuya aliposema kuwa kila mtu atabeba Msalaba wake, huo ulikuwa ni ukweli.
Tunapoimba Taarabu na mashairi, twapemba kusema ukweli kutumia mafumbo, lakini ikija kwa wanasiasa wetu katika hotuba twapagawa na kuogopa. Mmesahau yale ya "Kichwa cha Mwendawazimu, Wivu wa Kike" au Nyerere alipowapiga mkwara wanafunzi wa UDASA miaka ya 60-70 na kuwaambia "my foot up your.."?
Malecela alikuwa si mwoga wa utendaji kazi au kutoa maamuzi ambayo ni mlengo tofauti. Malecela, Msuya na Sokoine ni viongozi pekee ambao najua Mwalimu alikuwa inabidi afikiri mara mbili kabla ya kuwavaa. Hawa watatu walikuwa na uwezo w kufikiri na hata kumpinga Mwalimu bila woga!
Kiserikali, alianzia Umoja wa Mataifa, Wizara ya Mambo ya Nje, Kilimo, Ujenzi, Ukuu wa Mkoa, Ubalozi hata Uwaziri Mkuu na Makamu wa Rais. Kichama alianzia ngazi za Kata, Tarafa mpaka Taifa.
Ndio, Malecela kama binadamu yeyote ana udhaifu wake. Katika yote mnayombeza kama ndio kumchafua umahiri wake wa uongozi, hakuna hata moja linalosema kuwa yeye ni mla rushwa, fisadi au mhujumu. Kama ni Ulabu na Uzinzi, ni nani katika viongozi tulionao ambaye havipendi?
Tumeshikana makoo jusi kugombea picha za JK za ufuska mpaka JF ikafungwa, sasa iweje tumshupalie Malecela kuwa mzinzi na mlevi? Uzee? mbona Msekwa na Kingunge bado wapo?
Laana ya Nyerere: Mtakimbilia sana kudai Mwalimu alimtungia kitabu, mnasahau kuwa mlengwa hasa wa kile kitabu alikuwa aliyekuwa Rais wa Jamhuri na Mwenyekiti wa chama? Je mmesahau kuwa Nyerere alikuwa bingwa wa mafumbo?
Kama ni mtu kupewa nafasi ya pili, tumempa Kikwete sasa ni Rais, Lowassa sasa ni Waziri Mkuu, iweje suala la Malecela, Mkapa na Kingunge waliliona kuwa ni baya? Jee si Kikwete na Lowassa bado wameendeleza udhalimu wao wa kifisadi usio na woga wala aibu?
Kosa la Malecela machoni mwa Mwalimu, lilikuwa ni ule uamuzi wa kijasiri ambao Malecela aliufanya kitimiza utashi wa Zanzibar na Tanzania Bara.
Kukubali Zanzibar iingie OIC, na kuruhusu muswaada wa kuirudisha Serikali ya Tanganyika hivyo kufanya Serikali iwe ni vipande vitatu, Tanganyika, Zanzibar na Muungano.
Jee hilo ni kosa machoni mwa nani? hizi chokochoko tulizonazo kuhusu hatima ya Muungano na kelele zote za Uzanzibara na Utanganyika, zingezimika kama azma ya Zanzibar kama sehemu ya Muungano wangepata walichokitaka na Bara kurudia Utanganyika wao na hivyo kuwa na Serikali halali zinazowakilisha pande zote za Muungano.
Hili lilimkera Mwalimu kuliko jambo lingine alilolifanya Malecela. Na nina hakika Mwalimu alijua siku Malecela akishita hatamu, atabadili mfumo wa muungano ili kukidhi matakwa ya pande zote za Muungano hivyo kuondoa vurugu mechi zilizosababisha kufukuzwa kazi kwa Jumbe na Sefu.
Malecela hakuhofia Zanzibar kuwa nchi ya Kiislamu, ni utashi wa Wazanzibari kujiendesha kama Taifa la Kiislamu. Malecela hakuona shida ni kwa nini Tanganyika isirudi kuwa Tanganyika na hivyo iweze kujikwamua kama Taifa!
Hivyo basi, ngozi na maamuzi ya Malecela ya kidemokrasia wakati wa ule mtafuruku wa OIC na G55 ndio mpaka kesho tunautumia kama kivuli cha kumbeza? jee Muafaka wa CCM na CUF chimbuko na suluhisho lake ni nini kama si kuachia Zanzibar ijiendeshe kikamilifu kama Tifa bila kudhin=bitiwa na Serikali ya Muungano?
Leo hii na amini kuwa Mwalimu akipewa nafasi kurudi hata kwa dakika 5, atajutia uamuzi wake alioufanya kumpa Mkapa hatamu za nchi.
Kama tumemsema Mwinyi kwa Rukhsa na Azimio la Zanzibar, basi tusimsahau Mkapa na mazuri yake yote ya kiuchumi, kwa kulea Rushwa na Udhalimu uliokubuhu wa viongozi.
Malecela ama Tingatinga, ataendelea kuwa mtu pekee ambaye angejali maslahi ya Taifa kwanza, kumjali Mtanzania kwanza kabla ya tumbo lake. Na hilo ndilo pekee lilolowaogopesha waliotajwa kwenye orodha ya mafisadi!
Ujinga na mkataba wa kulindana katika kulihujumu Taifa, ndiko kulikomfanya aukose Urais.
Kosa lake la dhati ni kuamini kuwa angepata nafasi ingine kulijenga Taifa akiwa Mwana CCM. Hilo amecheza pata potea. CCM hawamuamini kwa maana atavunja mirija yao ya ulafi.