Malecela John Samwel na Legacy yake. Kwanini aliitwa Jumanne?

Lunyungu

JF-Expert Member
Aug 7, 2006
8,873
1,882
Majuzi tulusoma kwenye vyombo vya habari kwamba Mzee Jumanne ilibidi akimbie ukumbi baada ya Msekwa kuwa nominated kuwa mgombea pekee wa nafasi yake. Hadi leo sijajua kwa nini Mzee alikimbia ukumbi ule wakati jana alisifiwa baada ya kukatwa mtama kwamba ni mvumilivu wa vishindo kama Kawawa.

Lakini siku za nyuma niliwahi kuuliza Mzee John Jumanne Samwel Malecela atakumbukwa kwa lipi. Leo narudia kuuliza what will be his legacy ndani ya Chama na Serikali?

Mzee aliluwa mtemi na busara chache. Alikuwa na maneno machafu lakini alitumiwa kugombea majimbo na kuzima migogoro ndani ya CCM. Mzee yeye CCM kama JK ilikuwa ya kwanza Tanzania na Watanzania baadaye. Ndiyo maana aliwahi kutamka maneno ya dharau dhidi ya Watanzania sawa na Msuya kwamba "Go to hell".

Msuya alisha sahaulika na hata kuingia katika migogoro ya kidini huko kwao. Malecela kapewa kifuta jasho kuwa mjumbe hadi kufa ila sijajua na Ubunge sasa ataachia kwa kuwa kazeeka ama ataendeleza kulifanya mali yake.

Baada ya haya yangu naomba kusikia toka kwako. Ni nini itakuwa Legacy ya Mzee huyu aliyeshindwa kusoma alama za Nyakati sawa na Msekwa ilivyo tokea?
 

Masatu

JF-Expert Member
Jan 29, 2007
3,276
116
Malecela atakumbukwa na CCM kama kiongozi aliesaidia sana kurejea majimbo yaliyochukuliwa na wapinzani.

Moja ya sifa zake mzee huyu ktk kampeni huwa anakwenda mpaka ktk ngazi ya mtaa kijijini kabisa ambako hakuna hata Hotel na atajibanza na wanakijiji kulala kwenye nyumba za nyasi na tope ktk kukitumikia chama.

Hayo ya Jumanne mapya kwangu....
 

Mtanzania

JF-Expert Member
May 4, 2006
4,812
636
Wapi huko ulikosoma kwamba Malecela alikimbia ukumbi? Wengine hatujaona hayo maandishi mahali popote.

Malecela katumikia CCM na serikali miaka mingi sana, inabidi kumpa heshima yake kwa hilo.

Muda wote kuna watu kung'atuka au kuachia madaraka, sioni kama hilo ni tatizo.
 

Idimi

JF-Expert Member
Mar 18, 2007
14,552
9,681
Pamoja na kukitumikia chama kwa muda mrefu sana, bado hajapewa thamani anayostahili ndani ya chama.

Mwaka juzi wakati wa kugombea uraisi wa Tanzania, jina la Mzee Malecela liliondolewa katika mazingira ya shaka sana katika wagombea watano wa juu. Mkapa akadai kuwa aliondoa jina lake ili asaidiane naye katika kazi ngumu ya uchaguzi, uonevu ulioje! Kwa nini asingechukuliwa mwingine kumsaidia Mkapa?

Hali kadhalika, Malecela alihukumiwa na wanamtandao kwa kitabu cha Mwalimu Nyerere, cha 'Uongozi wetu na Hatima ya Tanzania', kwamba alitajwa na mwalimu kuwa hakuwa msafi na hakuwa shupavu kwa kuruhusu hoja ya Utanganyika kujadiliwa bungeni. Ni kitabu hiki hiki ambacho kiliwahukumu Lowassa na Kikwete, kuwa walikuwa na mali zisizo na maelezo ya namna walivyozipata, na kuwa walipata wapi pesa za kukodia ndege kwenda Dodoma kupeleka fomu za ugombea mwaka 2005. Lakini hawa wawili hawakuhukumiwa na kitabu hiki mwaka 2005, kwa nini?

Baada ya kutotendewa haki ilibidi alalamike kuwa yeye anatumiwa kama tingatinga, ambalo haliruhusiwi kupita barabarani katika lami baada ya kuijenga. Hakuna aliyesikia kilio chake hiki! Akakashfiwa juu ya umri wake, kwamba ni mzee kustahili urais na mikiki yake. Mbona Msekwa kazidiwa mwaka mmoja tu na Mzee huyu? Yeye hastahili kupumzishwa?

Mzee Malecela pamoja na kauli zake tata juu ya wasio wana sisiemu, lakini bado ni mtu muhimu sana ndani ya chama, hadi kabatizwa jina la 'Tingatinga'. Kwa historia ya chama hiki, yeye mpaka sasa ndio makamu pekee wa mweyekiti aliyeshika madaraka kwa muda mrefu namna hiyo. Hii inamaanisha kuwa anaaminika, la sivyo lazima angetemwa mapema. Pamoja na kashfa zote za wanamtandao, bado mzee huyu kawa mvumilivu.

Tuendele kujadili 'legacy' ya Malecela, naamini JF ina historia nzuri ya mzee Malecela.
 

Gamba la Nyoka

JF-Expert Member
May 1, 2007
7,027
9,263
Mimi ningependa kufahamu utendaji wake wa kazi alipokuwa Umoja wa Mataifa. Je aliiwakilisha vyema TZ?
 

Keykey

JF-Expert Member
Dec 1, 2006
3,250
733
Legacy ya mzee huyu imo ndani ya kitabu cha Hayati Baba wa Taifa 'Uongozi wetu anhatima ya Tanzania'. Walikuwa wawili, mwenzie alishatangulia mbele ya haki miaka 10 iliyopita.

Wengi wetu tunamkumbuka alipokuwa waziri wa Mawasiliano na uchukuzi miaka ya mwanzo ya '80 alipowaambia waTanzania 'waende kuzimu'.

Najua kuna wana-JF wasingependa kuiona thread hii lakini nadhani inavyoendelea kuchangiwa tutayapata mengi.
 

Ledwin

JF-Expert Member
Oct 9, 2007
224
24
Jamani hilo ni fundisho kwa wale wenye tabia ya kujiona kuwa wao ndio wanaweza kuongoza tu.

Mbona Mwl Nyerere alipostaafu Urais baadae akaachia mwenyewe na uongozi ndani ya Chama,ilitakiwa Mzee Malecela(mimi hilo jina la Jumanne silifahamu) nae afuate nyayo hizo,angeheshimika zaidi.

Kuna kazi nyingi sana za kufanya za kimataifa kwa watu wenye uzoefu wa kiaiasa na kiserikali kama aliokuwa nae hasa kama angechukua mkondo huo miaka mitano iliyopita.

Mimi namshauri hata huo Ubunge pia angejiuzulu. Ila sifahamu kama ndio itabidi uchaguzi mdogo au vipi? Kama CCM wataweza kum-replace bila uchaguzi, that will be the best option for him.
 

Gaijin

JF-Expert Member
Aug 21, 2007
11,815
5,232
atakumbukwa kama kada mkubwa wa ccm, ana aliyekifanyia chama hicho mengi yaliyokiletea faida na yalisoyokuwa na faida.

atakumbukwa pia kama kiongozi wa chama, aliendelea kung'ang'ania amdaraka, hadi waliomzunguka kuona kuwa hafai tena kushika nafasi hizo nyeti bila ya yeye kujishtukizia.

kwenye buku la historia la chama, natumai atajama kurasa na nyengine zitabakia
 

Idimi

JF-Expert Member
Mar 18, 2007
14,552
9,681
Kuna kazi nyingi sana za kufanya za kimataifa kwa watu wenye uzoefu wa kiaiasa na kiserikali kama aliokuwa nae hasa kama angechukua mkondo huo miaka mitano iliyopita.

Mimi namshauri hata huo Ubunge pia angejiuzulu.Ila sifahamu kama ndio itabidi uchaguzi mdogo au vipi?

Suala hili la kujiuzulu uongozi kwa Tanzania ni gumu sana, next to impossible.

Unaambiwa Msekwa alikuwepo bungeni tangu mwaka 1962 kwa vyeo mbali mbali, hadi alipobwagwa 2005. Na Kingunge je? Tusemeje? We unafikiri kuachia madaraka jambo rahisi eeh?
 

Masatu

JF-Expert Member
Jan 29, 2007
3,276
116
Ni kweli mazingira yaliyopelekea jina la Mzee Malecela kukatwa na CC yalikuwa ya uonevu, kama alivyoeleza Mzee Butiku Mkapa alimkata Malecela eti kwa sababu hakumshauri juu ya azma yake ya kugombea urais wakati yeye ni mwenyekiti wake. Mzee Butiku anahoji mbona na yeye Mkapa baada ya kuona jina la makamu wake kama wagombea asimwite na kushauriana nae namna ya mambo yatakavyokuwa.

Ikumbukwe ni Mkapa huyo huyo alie mtetea sana Malecela ktk CC kuelekea uchaguzi wa CCM 2002 wakati wakina Kingunge et al walipo gang-up kumng'oa Malecela kwa visingizio vya kitabu cha Mwalimu ulevi, uzinzi na uzee. Mkapa alisiamam kidete kumtetea kuwa mzee Malecela ndiye anaeifanya CCM iendelee kuwepo kwani yeye Mkapa kama Rais muda wote anautumia ktk mambo ya kiserikali na chama kamwachia Malecela ambae ndie alikuwa busy akipambana na wapinzani na kurejesha majimbo.

All in all mzee ame play his part tumwache na u back bencher wake plus U-CC na U-Nec wa maisha!
 

Rev. Kishoka

JF-Expert Member
Mar 7, 2006
4,525
1,521
Umeniwahi. Jana usiku nilikuwa nimeanza kucaha thredi mpya John's Legacy, nikapata wageni nikajisemea kesho (leo) nitaandika.

Wasifu wa John Malecela ni mkubwa sana kuliko kiongozi yeyote wa kale na wa sasa aliyeahai. Ukiondoa Uaris wa Mwinyi na Mkapa, wote wawili hawamfikii huyu kwa utu wake na mapenzi kwa Taifa!

Kwanza ni mkweli ambaye hakuogopa kusema ukweli wake wa moyoni hata kama uliudhi na hata kumfanya apoteze madaraka. Alipotoa lile tamko la kuenda kuzimu, ilikuwa ni mara ya kwanza kwa Watanzania kumsikia mwenzao ambaye ni kioongozi kutamka hadharani bila woga. Jee alichokikosea kilikuwa kipi? ni kutamka ukweli kwa ukali kuwa kama wasipoweza kujisaidia ni heri waende ahera? Sawa na Msuya aliposema kuwa kila mtu atabeba Msalaba wake, huo ulikuwa ni ukweli.

Tunapoimba Taarabu na mashairi, twapemba kusema ukweli kutumia mafumbo, lakini ikija kwa wanasiasa wetu katika hotuba twapagawa na kuogopa. Mmesahau yale ya "Kichwa cha Mwendawazimu, Wivu wa Kike" au Nyerere alipowapiga mkwara wanafunzi wa UDASA miaka ya 60-70 na kuwaambia "my foot up your.."?

Malecela alikuwa si mwoga wa utendaji kazi au kutoa maamuzi ambayo ni mlengo tofauti. Malecela, Msuya na Sokoine ni viongozi pekee ambao najua Mwalimu alikuwa inabidi afikiri mara mbili kabla ya kuwavaa. Hawa watatu walikuwa na uwezo w kufikiri na hata kumpinga Mwalimu bila woga!

Kiserikali, alianzia Umoja wa Mataifa, Wizara ya Mambo ya Nje, Kilimo, Ujenzi, Ukuu wa Mkoa, Ubalozi hata Uwaziri Mkuu na Makamu wa Rais. Kichama alianzia ngazi za Kata, Tarafa mpaka Taifa.

Ndio, Malecela kama binadamu yeyote ana udhaifu wake. Katika yote mnayombeza kama ndio kumchafua umahiri wake wa uongozi, hakuna hata moja linalosema kuwa yeye ni mla rushwa, fisadi au mhujumu. Kama ni Ulabu na Uzinzi, ni nani katika viongozi tulionao ambaye havipendi?

Tumeshikana makoo jusi kugombea picha za JK za ufuska mpaka JF ikafungwa, sasa iweje tumshupalie Malecela kuwa mzinzi na mlevi? Uzee? mbona Msekwa na Kingunge bado wapo?

Laana ya Nyerere: Mtakimbilia sana kudai Mwalimu alimtungia kitabu, mnasahau kuwa mlengwa hasa wa kile kitabu alikuwa aliyekuwa Rais wa Jamhuri na Mwenyekiti wa chama? Je mmesahau kuwa Nyerere alikuwa bingwa wa mafumbo?

Kama ni mtu kupewa nafasi ya pili, tumempa Kikwete sasa ni Rais, Lowassa sasa ni Waziri Mkuu, iweje suala la Malecela, Mkapa na Kingunge waliliona kuwa ni baya? Jee si Kikwete na Lowassa bado wameendeleza udhalimu wao wa kifisadi usio na woga wala aibu?

Kosa la Malecela machoni mwa Mwalimu, lilikuwa ni ule uamuzi wa kijasiri ambao Malecela aliufanya kitimiza utashi wa Zanzibar na Tanzania Bara.

Kukubali Zanzibar iingie OIC, na kuruhusu muswaada wa kuirudisha Serikali ya Tanganyika hivyo kufanya Serikali iwe ni vipande vitatu, Tanganyika, Zanzibar na Muungano.

Jee hilo ni kosa machoni mwa nani? hizi chokochoko tulizonazo kuhusu hatima ya Muungano na kelele zote za Uzanzibara na Utanganyika, zingezimika kama azma ya Zanzibar kama sehemu ya Muungano wangepata walichokitaka na Bara kurudia Utanganyika wao na hivyo kuwa na Serikali halali zinazowakilisha pande zote za Muungano.

Hili lilimkera Mwalimu kuliko jambo lingine alilolifanya Malecela. Na nina hakika Mwalimu alijua siku Malecela akishita hatamu, atabadili mfumo wa muungano ili kukidhi matakwa ya pande zote za Muungano hivyo kuondoa vurugu mechi zilizosababisha kufukuzwa kazi kwa Jumbe na Sefu.

Malecela hakuhofia Zanzibar kuwa nchi ya Kiislamu, ni utashi wa Wazanzibari kujiendesha kama Taifa la Kiislamu. Malecela hakuona shida ni kwa nini Tanganyika isirudi kuwa Tanganyika na hivyo iweze kujikwamua kama Taifa!

Hivyo basi, ngozi na maamuzi ya Malecela ya kidemokrasia wakati wa ule mtafuruku wa OIC na G55 ndio mpaka kesho tunautumia kama kivuli cha kumbeza? jee Muafaka wa CCM na CUF chimbuko na suluhisho lake ni nini kama si kuachia Zanzibar ijiendeshe kikamilifu kama Tifa bila kudhin=bitiwa na Serikali ya Muungano?

Leo hii na amini kuwa Mwalimu akipewa nafasi kurudi hata kwa dakika 5, atajutia uamuzi wake alioufanya kumpa Mkapa hatamu za nchi.

Kama tumemsema Mwinyi kwa Rukhsa na Azimio la Zanzibar, basi tusimsahau Mkapa na mazuri yake yote ya kiuchumi, kwa kulea Rushwa na Udhalimu uliokubuhu wa viongozi.

Malecela ama Tingatinga, ataendelea kuwa mtu pekee ambaye angejali maslahi ya Taifa kwanza, kumjali Mtanzania kwanza kabla ya tumbo lake. Na hilo ndilo pekee lilolowaogopesha waliotajwa kwenye orodha ya mafisadi!

Ujinga na mkataba wa kulindana katika kulihujumu Taifa, ndiko kulikomfanya aukose Urais.

Kosa lake la dhati ni kuamini kuwa angepata nafasi ingine kulijenga Taifa akiwa Mwana CCM. Hilo amecheza pata potea. CCM hawamuamini kwa maana atavunja mirija yao ya ulafi.
 

JokaKuu

Platinum Member
Jul 31, 2006
27,594
48,172
Ledwin, Kakalende, Murangira,

hata Mwalimu naye hakujiuzulu kwa kupenda mwenyewe, alilazimika kufanya hivyo baada ya kuwekewa vikwazo vya misaada na nchi za magharibi.

John Malecela alimsaidia sana Mzee Mwinyi maana yule nchi ilimshinda. Hata wabunge wa CCM walikuwa wamemchoka Mzee Mwinyi, na ile hoja ya Tanganyika ilikuwa ni kutoa madukuduku yao dhidi ya utawala wake mbovu.

Nimekisoma kitabu alichoandika Mwalimu Nyerere. Katika kitabu hicho Mwalimu amewashambulia Malecela na Kolimba kwa kubadili "msimamo" wao dhidi ya hoja ile. Hilo ndilo lilikuwa kosa lao!

Hoja ya Mwalimu ilikuwa kwamba Malecela na Kolimba walipaswa kujiuzulu nafasi zao kabla ya kuunga mkono hoja ile. Hakuna mahali ambapo Mwalimu alimtuhumu Malecela au Kolimba kwa kula rushwa au kwa ufisadi wa aina yoyote ile.

Kuna habari kwamba Malecela aliwaambia wananchi wanaolalamikia usafiri wa reli ya kati "they can go to hell!" Binafsi sikumbuki kusoma alitoa kauli hiyo wapi na ktk mazingira gani. Nalazimika kuamini kwamba kauli hiyo aliitoa katika faragha na ilivujishwa na wale waliokuwa hawamtakii mema kisiasa.

Binafsi naamini kama binadamu hatujakamilika. Haingewezekana Malecela awe ktk utumishi wa chama na serikali miaka yote na asitoe kauli yoyote ile itakayowaudhi au kuwakosea wananchi.

Hata Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere alitoa kauli ambayo ni dharau kwa wanawake alipodai Raisi Mwinyi anafanya maamuzi kwa kufuata ushauri wa mkewe.

Mwalimu Nyerere alieleza kabisa kwamba hoja ya Tanganyika ilitokana na hasira ya wabunge dhidi ya rushwa,utawala mbovu,na kuona hali ya waziwazi ya Wazanzibari "kupendelewa" dhidi ya Watanganyika.

Katika kukisoma kwangu kitabu kile, sikuona ulazima wa Mwalimu kumuandama Malecela badala ya walarushwa na wale waliokuwa wakileta mgawanyiko baina ya wazanzibari na watanganyika.

Zaidi kwanini ktk kitabu chake Mwalimu aling'ang'ania Malecela ajiuzulu Uwaziri Mkuu, na siyo pamoja na Umakamu wa Mwenyekiti wa CCM? Hiyo haileti mantiki kwasababu Mwalimu alimlazimisha Kolimba ajiuzulu Ukatibu Mkuu wa CCM!!!

Kuna tetesi kwamba Malecela hakuwa "mwanafunzi mtiifu" wa Baba wa Taifa kama walivyokuwa Ben Mkapa na Salim Salim. Inasemekana Malecela alikuwa akijiamini mno, na wakati mwingine kuchukua maamuzi bila kumtaka "ushauri" Baba wa Taifa. Inasemekana hali hiyo ndiyo iliyomfanya asidumu kama Waziri wa Mambo ya Nje.

Binafsi naamini there was more btn Mwalimu na Malecela kuliko hayo yaliyoandikwa kwenye kitabu. Kwa mfano kuna wanaodai kwamba Mwalimu alitishia kurudisha kadi ya CCM kama Malecela hangeondoa jina lake ktk kugombea Uraisi. Mbona Mwalimu hakufanya hivyo kwa Njelu Kasaka kiongozi wa G-55?

Mwisho:
Je, Malecela ni fisadi ama mla rushwa? Sijasikia mtu yeyote yule akisema Malecela ana majumba ya kifahari au ardhi kubwa.

Wanawe wote wamesoma Tanzania, sifa tunayompa Baba wa Taifa. Wawili wamesoma Muhimbili which is the toughest college in Tanzania. Hata marehemu mke wake alisoma na kuhitimu Sheria UDSM na wasichana wadogo alioweza kuwazaa. Watoto wake wawili wa mwisho ndiyo walisoma UK wakati akiwa balozi.

NB:
Malecela naye anapaswa kuandika kitabu ku-clear wingu la kisiasa lililomuandama ktk utumishi wake kwa Chama na Serikali.
 

Kamundu

Platinum Member
Nov 22, 2006
5,723
7,006
John Malecela
From Wikipedia, the free encyclopedia
• Ten things you may not know about Wikipedia •
Jump to: navigation, search
John Samuel Malecela
7th Prime Minister of Tanzania
In office
November 9, 1990 – December 7, 1994
President Ali Hassan Mwinyi
Preceded by Joseph Sinde Warioba
Succeeded by Cleopa David Msuya
Born 1934
Dodoma, Tanzania
Political party Chama cha Mapinduzi

John Samuel Malecela (born 1934) in Bugiri Dodoma, was Prime Minister of Tanzania from 1990-11-09–1994-12-07. He is currently vice-chairman of the CCM, and a member of the CCM Central Committee.

[edit] Education

* Secondary Education - Minaki secondary school 1957-1958
* Bachelor of Commerce - Bombay University 1958-1959
* Post Graduate Studies - Cambridge University 1961-1962
* Ph.D. Honoris Causa (Humanities) - University of Texas 1977

John Malecela is one of the most experienced Tanzanian poliiticians. However his efforts to seek his party's nomination for presidential candidacy did not yield any favorable results on his part both in 1995 and 2005.

[edit] Positions held

* Tanzania Permanent Representative to the United Nations - 1964-1966
* Tanzanian Ambassador to Ethiopia and the OAU - 1967
* Minister of Foreign Affairs - 1972-1973
* Communication and Transport - 1973-1974
* Mineral Resources and Agriculture 1975-1975
* Minister in the East African Community - 1975-1976
* Regional Commissioner of Iringa - 1980-1984
* Member of the Group of Eminent Persons of the Commonwealth on South African situation - 1985
* Tanzanian High Commissioner to the United Kingdom - 1989-90
* Prime Minister and First Vice President 1990-1994
* Vice Chairman of the ruling Party, Chama cha Mapinduzi (CCM) - 1995 to date
* Member of Parliament for Mtera - 1990 to date
 

Kazi Ndiyo Kipimo Cha Utu

JF-Expert Member
Mar 8, 2006
1,213
226
Mapungufu ya Kibinaadamu wote tunayo Lakini Ufisadi Malecela hakuwa nao na hakuwa na tabia hata ya kuwapendelea wanae na ndiyo maana pamoja na kuwa ndani ya Chama na serikali kwa muda mrefu hadi leo hata huyo mwanae ambaye ni Daktari,anafanyakazi Songea na Hakung'ania Kukaa Mjini wakati uwezo huo angekuwa nao au wizarani au hata ikulu Kama tunavyoona watoto na ndugu wa wengine wenye madaraka.

Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni.

Vile Vile ana miradi ya kawaida kama ya kilimo akimiliki shamba la mizabibu Lakini hajawahi kuwa Mwenyekiti wa bodi ya watendaji wa makampuni binafsi au Kumiliki Kampuni binafsi ambayo imeweza kutambulika na watu na kuwa na ushahidi.
 

Lunyungu

JF-Expert Member
Aug 7, 2006
8,873
1,882
Katika yote nasema Mzee John Jumanne Malecela hakuwa fisadi wala mla rushwa ila aliishi na kula na hata kuwatetea wala rushwa.Kwa hili sijui namweka wapi huyu Mzee .Ila siasa za mabavu , wizi wa kura nk ni vyake huyu mzee mwenye majina kama Tingatinga,nk.

Jina la Jumanne wote tunajua wakati mwalimu ana andika kitabu ilikuwa ni kumkata makali ya kugombea Urais ili Mkapa apite na hapo ilisikika kwamba kabadili dini na kuwa Muislam ili apate funds za Iran ambazo sasa alizichukua JK kupitia kwa mshikaji wake RA.

Alikuwa anaswali msikiti wa pale Sinza . Rev. Kishoka ukiitafuta ile thread ya zamani utaona maneno ya wananchi kila kitu kipo wazi juu ya jina hili.Lakini my point bado nataka kujua Legacy ya Mzee huyu . Je atasahaulika kabisa kama Msuya ?
 

Masatu

JF-Expert Member
Jan 29, 2007
3,276
116
Mapungufu ya Kibinaadamu wote tunayo Lakini Ufisadi Malecela hakuwa nao na hakuwa na tabia hata ya kuwapendelea wanae na ndiyo maana pamoja na kuwa ndani ya Chama na serikali kwa muda mrefu hadi leo hata huyo mwanae ambaye ni Daktari,anafanyakazi Songea na Hakung'ania Kukaa Mjini wakati uwezo huo angekuwa nao au wizarani au hata ikulu Kama tunavyoona watoto na ndugu wa wengine wenye madaraka.

Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni.

Vile Vile ana miradi ya kawaida kama ya kilimo akimiliki shamba la mizabibu Lakini hajawahi kuwa Mwenyekiti wa bodi ya watendaji wa makampuni binafsi au Kumiliki Kampuni binafsi ambayo imeweza kutambulika na watu na kuwa na ushahidi.

Brilliant intervention... kwa kuongeza wala hajataka awe daktari wa BOT.....
 

Masatu

JF-Expert Member
Jan 29, 2007
3,276
116
Katika yote nasema Mzee John Jumanne Malecela hakuwa fisadi wala mla rushwa ila aliishi na kula na hata kuwatetea wala rushwa.Kwa hili sijui namweka wapi huyu Mzee .Ila siasa za mabavu , wizi wa kura nk ni vyake huyu mzee mwenye majina kama Tingatinga,nk.

Jina la Jumanne wote tunajua wakati mwalimu ana andika kitabu ilikuwa ni kumkata makali ya kugombea Urais ili Mkapa apite na hapo ilisikika kwamba kabadili dini na kuwa Muislam ili apate funds za Iran ambazo sasa alizichukua JK kupitia kwa mshikaji wake RA.

Alikuwa anaswali msikiti wa pale Sinza . Rev. Kishoka ukiitafuta ile thread ya zamani utaona maneno ya wananchi kila kitu kipo wazi juu ya jina hili.Lakini my point bado nataka kujua Legacy ya Mzee huyu . Je atasahaulika kabisa kama Msuya ?


Hivi Jumanne ni jina la kiislam? naomba elimu hapo..
 
0 Reactions
Reply
Top Bottom