Malecela, Chitalilo Vs Dr Slaa

Asha Abdala

JF-Expert Member
Mar 21, 2007
1,131
40
Malecela, Chitalilo Vs Dr Slaa

Jana John Malecela alimjia juu Dr Slaa, na kumpasha kuwa hoja za ufisadi si za upinzani, ni za CCM ndio iliyoanza kuibua mambo yote. Amesema hoja ya EPA ilianzishwa na Dr Chegeni wakati hoja zingine zimeanzishwa na Anna Kilango. Amesema mambo mengi sana. Kama kuna mwenye Hansard ya jana atuwekee maana bunge halijarushwa jana.

Leo muda huu sasa Chitalilo amemjia juu Dr Slaa kwa kuetengeza maswala ya ufisadi ambayo ameyaiita majungu. Amesema watu waache kumfuata fuata Mkapa, wamheshimu!. Na amesema Chenge, Lowassa hawajavunja nyumba kuiba, wamewajibika tu.

Wote hawa hawajamtaja Dr Slaa kwa jina ila wamemjibu moja kwa moja kutokana na hotuba yake ya jana.

Asha
 
macinkus

JF-Expert Member
Sep 15, 2007
260
19
naona asha yupo bungeni. kwani haya ya chitalilo ndio amemaliza kusema sasa hivi. asante kwa kutuweka up to-date

macinkus
 
Field Marshall ES

JF-Expert Member
Apr 27, 2006
12,655
944
Jana John Malecela alimjia juu Dr Slaa, na kumpasha kuwa hoja za ufisadi si za upinzani, ni za CCM ndio iliyoanza kuibua mambo yote.

Kwenye hili mzee amekosea sana, originally hoja ya mafisadi ilianzishwa na Dr. Slaa hilo halina ubishi, yeye alichotakiwa kusema ni CCM na serikali zimefanya nini about it zaidi tu ya kamati zisizoisha na hakuna matokeo, sasa ni haki ya Dr. Slaaa kuuliza wazi kuwa CCM wamefikia wapi na hili la ufisadi maana wananchi hatuoni kilichofanyika on a serious note!

Kumbe ndio maana wanazima TV huko? Na huyu Chitalilo naye yumo kule nini?
 
Jobo

JF-Expert Member
May 15, 2008
586
42
Malecela, Chitalilo Vs Dr Slaa

Jana John Malecela alimjia juu Dr Slaa, na kumpasha kuwa hoja za ufisadi si za upinzani, ni za CCM ndio iliyoanza kuibua mambo yote. Amesema hoja ya EPA ilianzishwa na Dr Chegeni wakati hoja zingine zimeanzishwa na Anna Kilango. Amesema mambo mengi sana. Kama kuna mwenye Hansard ya jana atuwekee maana bunge halijarushwa jana.

Leo muda huu sasa Chitalilo amemjia juu Dr Slaa kwa kuetengeza maswala ya ufisadi ambayo ameyaiita majungu. Amesema watu waache kumfuata fuata Mkapa, wamheshimu!. Na amesema Chenge, Lowassa hawajavunja nyumba kuiba, wamewajibika tu.

Wote hawa hawajamtaja Dr Slaa kwa jina ila wamemjibu moja kwa moja kutokana na hotuba yake ya jana.

Asha

Anna Kilango kaanzisha hoja gani??? Siyo kwamba amedandia tu hoja ambazo zimeishajadiliwa?? Huyu mzee kwa kweli ameanza kuwa senile!
 
Jamco_Za

JF-Expert Member
Jul 14, 2007
1,330
192
Hivi huyu chitalilo si ndo yule aliyeforge vyeti na kudanganya amemaliza kidato cha sita kumbe aliishia kidato cha pili, mtu kama huyu anawajibika kuwatetea wakubwa wake mpaka mate yakauke mdomoni kwani akifukuzwa kwenye chama atakwenda wapi bila shule.

Tinga tinga anamwonea wivu Dr. siraa anaona kama anataka kuchukua sifa za mkewe, kumbe anamuunga mkono mke wake kwa siri, kuwa muwazi CCM wakujue kuwa na wewe wakati ulikuwa makamu mwenyekiti unawapinga walioiba unawaona na ukakaa kimya.
 
Primera dama

JF-Expert Member
Apr 21, 2008
827
164
Jamani huu uchama chama utaisha lini?mimi sioni maana ya kutafuta nani aliyeanzisha hoja!hoja ipo mezani kilichobaki ni kushughuikia mafisadi basi!yaani utafikiri watoto wadogo mimi ndo niliyeanzisha siyo wewe!Jamani siasa bwana ni mchezo mchafu!
 
Kuhani

JF-Expert Member
Apr 2, 2008
2,944
62
Kwenye hili mzee amekosea sana, originally hoja ya mafisadi ilianzishwa na Dr. Slaa hilo halina ubishi...

Field Marshall, huyu ni wewe huyu, au nina makengeza?

Ok, for the record, hongera kwa kuwa objective, independent, fair-minded and genuinely patriotic, for once.

Sio binadamu wengi duniani wanaweza kufanya ulichokifanya hapo.
 
Field Marshall ES

JF-Expert Member
Apr 27, 2006
12,655
944
Mkuu ndilo tatizo lenu wote mnaofikiria mnanifahamu, sasa labda nafikiri utaelewa kuwa sina mchezo na taifa hata siku moja, kwenye hili mzee amekosea period Dr. Slaa ndiye muanzilishi wa ishu ya mafisadi, na mimi ndiye niliyekuwa wa kwanza hapa kuleta list ya mafisadi kabla haijawekwa hadharani,

Na ninajua nilikoitoa ile list ndio maana ninasema wazi kuwa kwenye hili mzee yupo off the line! It is about our nation sio individual, haina nafasi hapa kabisaa!
 
Mtu wa Kwao

JF-Expert Member
Jan 15, 2008
258
21
Kwenye hili mzee amekosea sana, originally hoja ya mafisadi ilianzishwa na Dr. Slaa hilo halina ubishi, yeye alichotakiwa kusema ni CCM na serikali zimefanya nini about it zaidi tu ya kamati zisizoisha na hakuna matokeo, sasa ni haki ya Dr. Slaaa kuuliza wazi kuwa CCM wamefikia wapi na hili la ufisadi maana wananchi hatuoni kilichofanyika on a serious note!

Kumbe ndio maana wanazima TV huko? Na huyu Chitalilo naye yumo kule nini?
Chitalilo fisadi period.nimemsikiliza kwa kweli anatoia hasira kwa kusema wabunge wanarudiarudia hoja kila siku,epa kiwira richmond sijui nini huyo jamaa ni kichaa kwa kweli.
 
Mtu wa Kwao

JF-Expert Member
Jan 15, 2008
258
21
jamani Huu Uchama Chama Utaisha Lini?mimi Sioni Maana Ya Kutafuta Nani Aliyeanzisha Hoja!hoja Ipo Mezani Kilichobaki Ni Kushughuikia Mafisadi Basi!yaani Utafikiri Watoto Wadogo Mimi Ndo Niliyeanzisha Siyo Wewe!jamani Siasa Bwana Ni Mchezo Mchafu!
n I Kweli Mkuu Asubuhi Kwenye Kipindi Cha Jambo Tz Tbc1.dr Slaa Alisema Haya Hatuangalii Nani Muasisi Wa Hoja Kinachoangaliwa Ni Masilai Ya Nchi
 
mwanatanu

JF-Expert Member
Jan 22, 2008
854
126

Field Marshall, huyu ni wewe huyu, au nina makengeza?

Ok, for the record, hongera kwa kuwa objective, independent, fair-minded and genuinely patriotic, for once.

Sio binadamu wengi duniani wanaweza kufanya ulichokifanya hapo.

Mkuu naamini huu ni UTAIFA mbele

14:: Mheshimiwa Spika,
Kambi ya Upinzani inatoa rai kuwa ili tufanikiwe katika mipango yetu ya maendeleo yetu, ni lazima tuondokane na dhana ya itikadi katika masuala yanayogusa maslahi na ustawi wa Taifa. Maendeleo Mhe. Spika hayajui itikadi.

15:Mheshimiwa Spika,
Barabara ni barabara tu haijali chama na watu wa vyama vyote wanapita. Maji hayana sura, na wananchi hawatajali chama bali wataangalia nani kawaongoza kupata maji. Hivyo, Ofisi ya Waziri Mkuu, ambayo ndiyo Mratibu wa Vyama vya Siasa, ni vyema ikaandaa utaratibu wa kujenga imani kwa Watanzania kufanya kazi pamoja bila ya kuangalia itikadi za kisiasa. Utamaduni wa amani na mshikamano hujengwa hauji tu kwa miujiza.

Mheshimiwa Spika, Nawasilisha.

…………………………………………………
Dr. Willibrod Peter Slaa (MB),
Jimbo la Karatu,
MSEMAJI MKUU WA KAMBI YA UPINZANI-
OFISI YA WAZIRI MKUU/TAMISEMI.
23 June, 2008, Dodoma
.
 
Mtu wa Kwao

JF-Expert Member
Jan 15, 2008
258
21

Field Marshall, huyu ni wewe huyu, au nina makengeza?

Ok, for the record, hongera kwa kuwa objective, independent, fair-minded and genuinely patriotic, for once.

Sio binadamu wengi duniani wanaweza kufanya ulichokifanya hapo.
Kuhani kama kuna mtu mimi nampongeza ni FMES, huyu bwana huyu ni mtu anayetetea maslahi ya nchi na si chama chake na huwa anasimamia kwenye haki .si umeona hapo mkuu.
 
KakindoMaster

JF-Expert Member
Dec 5, 2006
1,357
83
Naona sasa tunarudi tulikotoka, John amekosea sana hata hakumbuki kuwa ni juzi tu angalau ndipo CCM wameanza kuongelea hili suala. Kinachotakiwa hasa hasa ni utekelezaji.

Mafisadi amewashika pabaya muda si murefu tutawaona kabisa wazi wazi na wapambe wao.

Nafikiri sasa tuanaanza kujua kuwa tatizo la kukomboa nchi si dogo
 
Mwikimbi

JF-Expert Member
Mar 8, 2008
1,762
805
malecela hana jipya, sanasana, hata kama atawasema mafisadi si kwa sababu ya uzalendo wake, bali ni kupambana na wale walimfanya kuwa tinga tinga. lakini pia akina malecela wamezeeka. wako wapi wabunge vijana kama akina fuya kimbita, kijana wa miaka 40 wa jimbo la hai, tena msomi? wako wapi wabunge vijana huko ccm wanaoweza hata kufika nusu ya mama ana kilango?
 
Halisi

JF-Expert Member
Jan 16, 2007
2,802
609
Huyu ndiye Chitalilo mwenye kesi ya kughushi vyeti, lakini tusubiri kijana mbichi, mtoto wa Kigoma, Peter Serukamba, ametajwa kuchangia muda si mrefu nadhani baada ya nusu saa hivi.... Kazi kweli kweli, angalia wanaotetea moja kwa moja... rekodi zao zinatia shaka..... hii ni dalili njema kwa wapambanaji maana kama hao ndio wanaoshirikiana nao basi tujue wamezidiwa. Angalia jana Mama Mkapa alipewa ushirikiano na mama Lowassa na wakamuweka mama wa watu pale Mama Maria Nyerere kufunika "mshikamano" wao.
 
Kuhani

JF-Expert Member
Apr 2, 2008
2,944
62
Kuhani kama kuna mtu mimi nampongeza ni FMES, huyu bwana huyu ni mtu anayetetea maslahi ya nchi na si chama chake na huwa anasimamia kwenye haki .si umeona hapo mkuu.

Hapa hatuongelei chama hapa.

Huwa, nakataa 99% ya anavyovisema jamaa, na hasa style yake ya majadiliano pale anapokuwa cornered ku defend "dataz" zake kwa wale tunaokataa kuzibugia bugia kama maji ya sharbati.

Hapa nimekusanya nguvu kumpa credit kwa ile comment kwa sababu zisizohusiana na itikadi za chama hata kidogo.

Notice, nimesema sio binadamu wengi wanaweza kufanya alichosema pale. Kama ni objectivity kwenye siasa za vyama ni wengi tu wako fair-minded kwenye hilo. Kwa hapa kuna nobility that runs deeper that party politics.
 
KakindoMaster

JF-Expert Member
Dec 5, 2006
1,357
83
Nafikiri Mbunge Kijana kama Serukamba kuanza kujiunga na wahujumu uchumi kwa sasa ni dalili mbaya sana kwa taifa hapo baadae naona sasa wanajipanga vya kutosha kuhakikisha hata watawala wa baadae wanakuwa wahujumu kweli kweli
 
Mtu wa Kwao

JF-Expert Member
Jan 15, 2008
258
21
Ngoja tumuone fisadi mwingine akiongea jamani mana hawa akina serukamba na chitalilo kama wamelipwa kuwatete mafisadi badala ya taifa.eti chenge hajavunja nyumba ya mtu kuiba .
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Top Bottom