Malecela akiwa New York kumpongeza Balozi mpya na msaidizi wake

nngu007

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2010
Messages
15,870
Points
1,225

nngu007

JF-Expert Member
Joined Aug 2, 2010
15,870 1,225

Sunday, December 2, 2012

SHEREHE YA KUWAPONGEZA WAHESHIMIWA YA FANA NEW YORK
Sherehe za kuwa pongeza na kuwakaribisha waheshimwa ma balozi picha na matukio, hapa ni meza kuu ambayo waliketi waheshimiwa mabalozi na wageni wengine wahalikwa katika sherehe hiyo. Mh Balozi Manongi na Msaidizi wake Mh. Ramadhan Mwinyi walikaribishwa na kujitamburisha mbele ya watanzania wanaoishi New York na vitongoji vyake. Katika sherehe hiyo iliyo andaliwa na NYTC(Board na Exacutive Commitee.Sherehe hiyo ilifanyika New Rochelle, NY Hapa chini ni picha na matukio yaliyo jili katika sherehe hiyo.

Naibu mwakilishi wa balozi Mh. Ramadhan Muombwa Mwinyi akiwa na mama mwenye nyumba wake pembeni wakipata ukodak wa Vijimambo katika sherehe hiyo ya kumkaribisha.

Mh. Balozi Tuvako Manongi akiteta jambo ma Mh Malicela Prime Minister mstaafu, Mh Malicela alikuwepo pia katika sherehe hizo.

Mh. Ramadhan Mwinyi akipata ukodaki na Mh. Malicela

Ally Chunda akipata ukodak na Mh. Ramadhan na mama mwenye nyumba wa Mh. katikati

MC wa sherehe hizo bwana mwakalinga akiwa kazini kuwatangazia kila kilichotakiwa kuendelea ukumbini hapo

mama Kiswaga akitoa nasaha zake katika sherehe hizo

Picha za pamoja na viongozi wahusika, kwa picha zaidi nenda (read more)VIJIMAMBO
 

nngu007

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2010
Messages
15,870
Points
1,225

nngu007

JF-Expert Member
Joined Aug 2, 2010
15,870 1,225

PARTY INAENDELEA...


at 9:38 AM

WABONGO wanajua KUPATA RAHA... MZEE MALECELA kahamia NY? Au ni MGENI RASMI CCM IMEMPELEKA???


 

Gad ONEYA

JF-Expert Member
Joined
Oct 26, 2010
Messages
2,638
Points
1,195

Gad ONEYA

JF-Expert Member
Joined Oct 26, 2010
2,638 1,195
Mtuletee na picha za kukaribishana Riyadh, Tehran na kwingineko huku kwenye vurugu...sio kila siku New York, mara DVM mara London. Kwani huko tu ndio tuna mabalozi?!!!! Kha...
 

Honolulu

JF-Expert Member
Joined
Jan 20, 2012
Messages
5,649
Points
1,225

Honolulu

JF-Expert Member
Joined Jan 20, 2012
5,649 1,225
Upuuzi mtupu!! Sioni hata mantiki ya huu utumbo!!!! Hivi watanzania kwa nini mnajivunia Marekani??? Ni kwenu huko???!!!
 

Father of All

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2012
Messages
3,090
Points
1,225

Father of All

JF-Expert Member
Joined Feb 26, 2012
3,090 1,225
Mijitu mingine kwa ushamba. Hivyo vivazi vyao na ghafla yenyewe hata havifanani. Uhuni upuuzi mtupu nakubaliana na mchangiaji mwanangu Honolulu. Je hao wote waliohudhuria wana makaratasi na kama wameajiriwa kwenye ubalozi wamepata ajira kwa sifa au udugu na kujuana?
 

Kwameh

JF-Expert Member
Joined
Dec 3, 2011
Messages
1,279
Points
2,000

Kwameh

JF-Expert Member
Joined Dec 3, 2011
1,279 2,000
Picha sawa, zina kitu cha kuongeza katika maslahi ya taifa na ktk foreign policy ya Tanzania? Mtu wa Namtumbo anahitaji hizi picha?
Ndio utamaduni wa Kitanzania, hata wale ambao ungetegemea wana exposure kidogo, wapi, mtu akipata cheo anafanyiwa pati. Hatuchukulii kazi za uongozi wa umma kama ni majukumu na mzigo. Ushawahi kuona balozi au waziri wa Marekani kafanya pati baada ya kuteuliwa?

Tunataka uanze kazi mheshimiwa, sio bado unafinyiwa mapati mpaka leo. Watu wenyewe nao ambao tunaongozwa ndio hivyo tena mangumbalu watupu, ilibidi wamualike kwenye mkutano wa Watanzania aeleze international agenda ya Tanzania UN ikoje, amekuja na jipya lipi, askari wa Tanzania UN Mission wanaokufa The Horn of Afrika kwa kutumbukia kwenye vidimbwi vya maji inakuaje kuaje hapo. Badala yake cheo, pati.
 

Candid Scope

JF-Expert Member
Joined
Nov 8, 2010
Messages
11,882
Points
1,250

Candid Scope

JF-Expert Member
Joined Nov 8, 2010
11,882 1,250

Sunday, December 2, 2012

SHEREHE YA KUWAPONGEZA WAHESHIMIWA YA FANA NEW YORK
Sherehe za kuwa pongeza na kuwakaribisha waheshimwa ma balozi picha na matukio, hapa ni meza kuu ambayo waliketi waheshimiwa mabalozi na wageni wengine wahalikwa katika sherehe hiyo. Mh Balozi Manongi na Msaidizi wake Mh. Ramadhan Mwinyi walikaribishwa na kujitamburisha mbele ya watanzania wanaoishi New York na vitongoji vyake. Katika sherehe hiyo iliyo andaliwa na NYTC(Board na Exacutive Commitee.Sherehe hiyo ilifanyika New Rochelle, NY Hapa chini ni picha na matukio yaliyo jili katika sherehe hiyo.
http://2.bp.blogspot.com/-R6MqDjph_Uw/ULswae0oosI/AAAAAAAAN40/tjTZNsk7M4g/s1600/IMG_7645.JPGVIJIMAMBO
New Rochelle napakumbuka ni sehemu ambayo watanzania hupenda kwenda kuonyeshana mambo yao pale. Ni kitongoji katika viunga vya jiji la New York.

Nilipokuwa huko nilifanikiwa kuhudhuria matukio mawili.
Part ya Watanzania huko New Rochelle nilivutwa na wajuaji eti kuna mkutano wa watanzania twenda tukajumuike. Nikaomba ajenda wanipe nijiandae kuchangia, nikaambiwa tutapewa huko huko na kusomewa minutes za mkutano uliotangulia. Nikajikokota nikaone kulikoni na nilichokishuhudia ni kwenye bar fulani tulikokutanika na kisha kila mmoja anunue vinywaji vyake ndiyo faida ya mwenye bar. Sikuona mkutano zaidi ya miziki na vinywaji ambavyo wengine viliwaathiri hadi kusaidia kufikishwa makwao. Kumbe ni party ambayo haikuandaliwa ila ni kukusanyika kwenye bar na kila mmoja kununua vinywaji na nyamachoma.​


  • [*=1]Niliapa sitarudia na sikurudia hadi nilipoondoka maana sikuona cha maana na kwamba maana yao ya kukutana, wanawake kugombania wanaume na wanaume kuchaniana mashati sababu ya kugombea wasichana, niliona kama nitakuja kujidhalilisha hata siku ikitokea nitakuja kuwashangaza wengi kulikoni kwani wanajua si hulka yangu.
Mkutano wa pili ni kwenye nyumba anayokaa Balozi wa Tanzania kwa Umoja wa mataifa eneo la Westchester County. Mkutano ulianza vizuri na Mkapa aliongea mengi mazuri na kujibu maswali mbalimbali tuliyomwuliza na tukafurahi kusikia ya nyumbani.​


  • [*=1]Baada ya Mkutano kukawa na party ya watanzania kwenye makazi hayo ya balozi na chini kwenye basement baada ya maakuli disco la kufa mtu ambako sikuingia kwani kilichonipeleka kilikamilika siku ile ya Jumapili na sasa kilichonijia akilini ni kurudi kulala home kisha kesho yake niwahi kibaruani na alasiri niende class College. Ilikuwa kazi nzito kuondoka maana wajuaji niliowasaidia usafiri hawakuwa tayari kuondoka na kuliacha disco lao. Basi kwa haidhuru tu wakaamua kutii vinginevyo ningewaacha jijini NY maana kwangu mimi majukumu ni muhimu kuliko maraha bila kuwa na ratiba.

Huo ukawa mwanzo na mwisho wangu, kwani nilijiona kufuata tu ni mkumbo na huenda mambo hayo yakanisababishia siku nichelewe darasa maana mahudhuria darasani Marekani ni sheria la sivyo termination.

Kweli Watanzania wanapenda raha, lakini si wote, wengi waliotulia na wanaajira zao wanajali sana shughuli zao kuliko sherehe ambazo ukikosa hakuna athari kwa kazi au chuo.

Tangu hapo nikawa mwanajopo la kundi la wastaarabu wenye kujali zaidi heshima na utu wao pamoja na familia zao. Itokeapo sherehe basi safari hii kwa fulani na ifuatayo kwa fulani basi ni mzunguko wenye kutia raha vile si mwajua!
 

jamii01

JF-Expert Member
Joined
Oct 1, 2010
Messages
1,886
Points
2,000

jamii01

JF-Expert Member
Joined Oct 1, 2010
1,886 2,000
Mbona sherehe yenyewe imekaa kilocal sana..kwa maana wameshidwa kununa vyakula vya maana na vinywaji?wanakunywa soda za kwenye makopo hakuna glass za maana?ingekuwa sherehe ya wenzetu wakenya ungeshaa..Watanzania sijui tunashida gani,,kila kitu tuko nyuma hata kwenye chini za wenzetu mambo ni yale yale tu.
 

Kiranga

JF-Expert Member
Joined
Jan 29, 2009
Messages
50,285
Points
2,000

Kiranga

JF-Expert Member
Joined Jan 29, 2009
50,285 2,000
Kuwa na ulazima au kutokuwa na ulazima ni suala lake mwenyewe. Wewe umejuaje kama hakuwa na ulazima? Uliingia kwenye akili yake?
Huyu hapa sio tu anahitaji somo la netiquette 101, lakini inawezekana anahitaji kumuona shrink kwa sababu this self exposure is beyond simple home training issues.
 

Forum statistics

Threads 1,392,812
Members 528,696
Posts 34,118,688
Top