Elections 2010 Malecela ahofia CCM kuwa katika hali ngumu 2010

huyu mzee bwana!............amesahau kwamba alishataka kuwa USTAADHI kwa tamaa za pesa!
 
Samahani mkuu, nilijua nitakukwaza maana kuna watu walijaribu kunitahadhalisha kabla, lakini hayo yalikuwa ni mawazo yangu na nimemnukuu Nyerere maana aliyasema pia kwenye kile kitabu chake cha Hatima ya uongozi.
Na najua Malecela amechaguliwa na watu.

- Unasema kwamba u-DC Tukuyu alichaguliwa na wananchi? Alipoteuliwa kwenda kubwa balozi UN alichaguliwa na wananchi? Unasema alipoteuliwa kuwa waziri EAC alichaguliwa na wananchi? Au alipoteuliwa kuwa waziri wa nje alichaguliwa na wananchi?

- Sasa weka facts, alichaguliwa na wananchi gani, wa jimbo gani au taifa lipi hilo?


- Samahani sana kwa kukukwaza.

Respect.

FMEs!


 
Na unajua c wote waliochaguliwa walichaguliwa kwa sababu kweli walikuwa ni watumishi wazuri, hapana. Kuna sababu nyingi tu zinazoweza kumfanya mtu achaguliwe hata kama hafai.
Ndio sababu sioni ajabu EL kuwekewa zuria wakati ana tuhuma kubwa za rushwa. Na sintaona ajabu kama wamasai watamchagua tena kuwa mwakilishi wao.
Na sioni ajabu Chenge akipokelewa kama mfalme wa wasukuma wakati wote tunajua nini alichofanya. Na sintaona ajabu kama atarudishwa bungeni na chama chake.
Na sioni ajabu hata rais akichagua fisadi Makamba na kumpa ukatibu mkuu wa chama chenu pamoja na tuhuma za ufisadi alizo nazo.
Nasema sintaona ajabu.
Samahani sana kaka kama nimekukwaza ila hapa nilitoa maoni yangu tu hata kama yanachoma moyo. Tuvumiliane tu.

- Sasa nielemishe jinsi kiongozi anayefaa kama Kambarage kuishia kuchagua viongozi wasiofaa, huku akijua hawafai ili walifanyie nini taifa? Kwa hiyo unasema Mwalimu alikuwa akichagua viongozi wasiofaa makusudi just because ana sababu! labda uiseme ni sababu ipi hiyo?

- Eti hizi ni logic au facts? Huwezi kunikwaza bila ya kuwa na facts ya unachokisema, infact unajikwaza mwenyewe so far, au?

Respect.

FMEs!
 
Cigwiyemisi John Samwel Malecela ni mtu mmoja atakayekumbukwa katika historia ya Tanzania kama kada wa CCM na Waziri Mkuu wa JMT aliyepigana kufa na kupona kuzuia upepo wa mageuzi mwaka 1991. Cigwiyemisi John Samwel Malecela alifikia hatua ya kuwafananisha wanamageuzi na sisimizi wa kusiginwa tu na kufilia mbali.

Kama si kwa Mwalimu kuingilia kati na kusema kuongelea mageuzi si dhambi, hakuna mwana CCM hata mmoja - si kiongozi wala mwananchama (mwenye kadi), aliyebariki mfumo wa vyama vingi. CCM ilijikuta inalazimika kusalimu amri na kukubali mageuzi kutokana na nguvu zilizokuwa nje ya uwezo wake japo kwa shingo upande.

Sera ya ufisadi ndani ya CCM ilianza pale ilipokataa kuridhia kuandikwa kwa katiba mpya iliyoendana na hayo mabadiliko makubwa. Hiyo iliwapa nafasi ya upendeleo maalum katika hatua zote za mwanzo tangu katika usimamizi na uandikishwaji wa vyama vipya. CCM imeendeleza hivyo hivyo ubabe wa kuwa mchezaji na mwamuzi vyote kwa pamoja.

  • Wakahatamia katiba na kuifanya ajenda yao binafsi - ufisadi namba moja.
  • Wakatwaa mali zote zilizochangiwa kwa pamoja -- ufisadi namba mbili.
  • Wakafunga milango ya kudai haki na usawa- ufisadi namba tatu.
  • Wakateua kada wao kuongoza tume ya uchaguzi - ufisadi namba nne.
  • Wakabuni hila chafu chafu za kubaki madarakani - ufisadi namba tano
Kote huko Cigwiyemisi John Samwel Malecela alikuwa kamanda muhimu.

Na sasa Cigwiyemisi John Samwel Malecela, mzee aliyetakiwa kung'atuka na kuwaachia wajukuu wake ulingo wa siasa anasema mbinu mpya ziko jikoni zinapikwa ! Anayejaribu kutenganisha CCM na hii kasi ya ufisadi tunayoshuhudia sasa hivi ni heri akanunue miwani. Mwana CCM anayedai yeye si fisadi na kuwaelekezea vidole makada wenzake ndani ya CCM ni limbukeni wa kutupwa - and that's a memo !!

- Hii ninamuachia Mkulu Engineer aje kujibu, maana mimi siwezi mapigo haya BWa! ha! ha! ha! ha!

Respect and Out!

FMEs!
 
- Sasa nielemishe jinsi kiongozi anayefaa kama Kambarage kuishia kuchagua viongozi wasiofaa, huku akijua hawafai ili walifanyie nini taifa? Kwa hiyo unasema Mwalimu alikuwa akichagua viongozi wasiofaa makusudi just because ana sababu! labda uiseme ni sababu ipi hiyo?

- Eti hizi ni logic au facts? Huwezi kunikwaza bila ya kuwa na facts ya unachokisema, infact unajikwaza mwenyewe so far, au?

Respect.

FMEs!

- Unasema kwamba u-DC Tukuyu alichaguliwa na wananchi? Alipoteuliwa kwenda kubwa balozi UN alichaguliwa na wananchi? Unasema alipoteuliwa kuwa waziri EAC alichaguliwa na wananchi? Au alipoteuliwa kuwa waziri wa nje alichaguliwa na wananchi?

- Sasa weka facts, alichaguliwa na wananchi gani, wa jimbo gani au taifa lipi hilo?

- Samahani sana kwa kukukwaza.

Respect.
- Unasema kwamba u-DC Tukuyu alichaguliwa na wananchi? Alipoteuliwa kwenda kubwa balozi UN alichaguliwa na wananchi? Unasema alipoteuliwa kuwa waziri EAC alichaguliwa na wananchi? Au alipoteuliwa kuwa waziri wa nje alichaguliwa na wananchi?

- Sasa weka facts, alichaguliwa na wananchi gani, wa jimbo gani au taifa lipi hilo?

- Samahani sana kwa kukukwaza.

Respect.

Mkuu FMES watu hubadilika kutoka wakati mmoja hadi mwingine. Mzee alivyokuwa yaani zile colours alizokuwa nazo at that time Nyerere anamchagua kuwa kiongozi huko kote ulikosema si hizi alizokuwa nazo baada ya Mwalimu.
Huyu huyu alikuwa wa kwanza pamoja na kundi lake kulizika azimio la Arusha.
Na ni kwa huyu huyu Nyerere alijuta kumuweka kwenye system yake hadi kamtungia kitabu. Ina maana kama Nyerere angepewa nafasi ya kutawala tena nakwambia hata anayozungumza leo asingeweza kusema neno.
Na unaweza kuona kweli kwamba huyu sasa anaonyesha true colours kwa uoza anaosema leo bila hata haya.
Hivi wizi wa kura na mbinu zingine chafu ni vitu vya kujivunia kwa mtu kama mzee huyu? Au labda tuseme uzee unamfanya mtu apunguze uwezo wa kufikiri kabla ya kusema?
Respect mkuu
 


Mkuu FMES watu hubadilika kutoka wakati mmoja hadi mwingine. Mzee alivyokuwa yaani zile colours alizokuwa nazo at that time Nyerere anamchagua kuwa kiongozi huko kote ulikosema si hizi alizokuwa nazo baada ya Mwalimu.
Huyu huyu alikuwa wa kwanza pamoja na kundi lake kulizika azimio la Arusha.

- Unajua hapa sasa ndipo unafurahisha sana mkuu, umesema Mwalimu alimchagua pamoja na kwamba alijua kuwa sio kiongozi safi, sasa umebadili kwamba alikuwa safi lakini alibadilika, sasa chagua mwenyewe unataka kusimamia hoja ipi kati ya hizo mbili zinazopingana ulizozitoa mwenyewe! Bwa! ha! ha!

- Azimio la Arusha lilizkwa na rais wa jamhuri na mwenyekiti wa CCM, then Mwinyi, lilipozikwa Mwalimu alikuwepo hawakumzunguka walifanya wazi kwenye kikao cha CCM Zanzibar, sio Malecela aliyevunja rekebisha hilo.

Na ni kwa huyu huyu Nyerere alijuta kumuweka kwenye system yake hadi kamtungia kitabu. Ina maana kama Nyerere angepewa nafasi ya kutawala tena nakwambia hata anayozungumza leo asingeweza kusema neno.


- Sawa sawa, sasa simamia tena hoja yako, wakati Mwalimu anampa Mkapa urais na uenyekiti wa CCM, kwa nini alimruhusu Malecela kuwa makamu wake huku tayari akiwa ameandika kitabu chake? Bwa! ha! ha! unaona mambo ya kurukia treni kwa mbele sasa Bwa! ha!

Na unaweza kuona kweli kwamba huyu sasa anaonyesha true colours kwa uoza anaosema leo bila hata haya.
Hivi wizi wa kura na mbinu zingine chafu ni vitu vya kujivunia kwa mtu kama mzee huyu? Au labda tuseme uzee unamfanya mtu apunguze uwezo wa kufikiri kabla ya kusema?
Respect mkuu
- Kwa nini hakuiba kura za Tarime? Au Kigoma kwa Zitto? Acha kurukia treni mkuu na habari za kusimuliwa na alinacha, tafuta facts mwenyewe kabla ya kukurupuka na lugha za hovyo hovyo ambazo haziwezi kutusaidia taifa mkuu Bwa! ha! ha! tizama unavyojikanyaga kanyaga Ha! ha! ha! Inawezekana haya ya uzee una experience nayo, labda ungetoa definiton kwanza on uzee, maana kama wewe kijana unashindana na Mzee Malecela kila kukicha anakushinda kwenye uchaguzi, then something is wrong na hii theory yako ya uzee, kwani Makamba sio mzee mbona hakushinda Tarime? Kwa nini wazee Makamba na Msekwa hawakuiba kura Tarime?

- Anyways samahani nilitaka tu kukupa darasa kidogo tu juu ya tabia ya kudandia treni kwa mbele, sasa unaweza kuendelea na matusi yako, Bwa! ha! ha! Ndugu a great thinker ndani ya The home of the great Thinkers!

Respect.

FMES!
 
Mzee pamoja kwamba huyu mzee ni baba yako , lakini kwa maneni yake haya nadhani anastahili kulaaniwa .Bura nzuri ni kama nyie mtamshauri akae pembeni sasa amesha choka na wenzake kama akina Kingunge wana haribu.Yes Tarime hawakuweza kwa kuwa wanaume walisimama kule .Kote kote alikosimamia aliendesha zoezi wa wizi wa kura si kuiba ma box bali kupora ushindi kwa kusema sisi ni Serikali Tangaza tumeshinda na ikawa hivyo .
 
Mzee pamoja kwamba huyu mzee ni baba yako , lakini kwa maneni yake haya nadhani anastahili kulaaniwa .Bura nzuri ni kama nyie mtamshauri akae pembeni sasa amesha choka na wenzake kama akina Kingunge wana haribu.Yes Tarime hawakuweza kwa kuwa wanaume walisimama kule .Kote kote alikosimamia aliendesha zoezi wa wizi wa kura si kuiba ma box bali kupora ushindi kwa kusema sisi ni Serikali Tangaza tumeshinda na ikawa hivyo .

MvutaKamba unanipa raha!
 
Mzee pamoja kwamba huyu mzee ni baba yako , lakini kwa maneni yake haya nadhani anastahili kulaaniwa .Bura nzuri ni kama nyie mtamshauri akae pembeni sasa amesha choka na wenzake kama akina Kingunge wana haribu.Yes Tarime hawakuweza kwa kuwa wanaume walisimama kule .Kote kote alikosimamia aliendesha zoezi wa wizi wa kura si kuiba ma box bali kupora ushindi kwa kusema sisi ni Serikali Tangaza tumeshinda na ikawa hivyo .

- Labda ni baba yako wewe, ila hapa JF huwa hatujali baba wa nani tunakata ishu tu bila uoga wala vitisho au kuogopa matusi, kwenye siasa kuna laana ya wananchi na huionyesha kwenye vibox vya kura.

- Lakini hao wanaume wakashindwa kusimama Biharamulo na Busanda, another mufilisi theories, kwa hiyo una maana katika majimbo yote ya Tanzania, ni Tarime peke yake kwenye wanaume huku kwingine ni wanawake watupu? Bwa! ha! ha! pole sana great thinker!

- Na how do you define wanawake wa majimbo mengine ya Tanzania na hii theory yako ya siasa za wanaume na wanawake?

- Sasa kaanze kuwaondoa wazee kina Ndesamburo na Slaaa, halafu uhamie CCM, huyu baba yako aliweza kuiba kura kwingine kote lakini akashindwa kuiba Taarime na Kigoma, si unaona unavyochekesha! Bwa! ha! ha!

- Mapovu mengi kama una hoja kumbe ni mtupu kama aliyekutangulia! ya kudandia treni kwa mbele unaona sasa aibu na huyo baba yako! Bwa! ha! mkuu naona ndio kwanza umeingia hii JF hapa huwa hatujali baba wa mtu wala wa member huwa ni fimbo tu! Hoja hujibiwa kwa hoja na viroja hujibiwa na viroja,

- karibu sana JF, maana ninakukumbuka kutoka forums moja kule vichochoroni, hapa umeingia kwenye ngoma kubwa, yaani the home of great thinkers sasa jaribu ku-adjust maana hapa ya baba hayana nafasi ni taifa mbele tu na masilahi yake!

Respect.

FMEs!
 
Wee mvutakamba,
Walishatuonya kuhusu kumsema mzee wetu kwa nini umethubutu?
Sasa unaona mashambulizi?
Masanilo asante kwa kutupa tahadhali. Hata hivyo message sent.
 
Kwa hakika ni mwelekeo mzuri, lakini inafaa wengi wapate ujasiri na kuanza kuzungumza na wazungumze kwenye vile vikao rasmi, ni wakati wa kuachana na zidumu fikra...

Unajua ndani ya Chama Makamba amehakikisha kuwa agenda ya ufisadi haijadiliwi katika vikao halali vya chama na hili kwa kiasi fulani amefanikiwa.Kwa kuwa hilo limetokea wanachama wa CCM hawana fursa nyingine ya kusema ufisadi wazi wazi isipokuwa kwenye vyombo vya habari,na kwenye mikutano yao isiyo rasmi.

Mimi naona huu ni mwanzo tu wa mambo mazuri kuja hapo baadae ambapo wanachama wa ccm wataacha uoga na kuelezana ukweli wazi wazi.Unajua kuna wazee waliobobea kwenye siasa kama Mzee Malecela ukitaka kumtuhumu katika vikao halali ndani ya chama lazima uwe umejipanga kweli kweli na umejiandaa vya kutosha kwa hoja yako.Vinginevyo hoja yako itakurudia wewe mwenyewe na kuishia kuadhibiwa na chama.

Mimi nachukia ufisadi na wizi wowote wa rasilimali za Tanzania,wizi huu ni pamoja na wizi wa kura kwani kwa kufanya hivyo kunawanyima watanzania walio wengi fursa ya kupata viongozi watakao waletea maendeleo.Kwa hili Mzee Malecela hana pa kuponea ni lazima awaombe watanzania msamaha kwa kuwachagulia viongozi/wabunge kwenye chaguzi ndogo ndogo ambao kwa kiasi kikubwa wameonyesha kupwaya katika masuala ya uongozi.

Dawa ya ufisadi Tanzania tufanye kama China,kiongozi akituhumiwa kwa ufisadi anaachia madaraka kupisha tume huru kufanya uchunguzi.Na ikigundulika kuwa ameshiriki kwenye ufisadi au ubadhirifu wa mali ya umma ananyongwa hadharani na mali zake kutaifishwa na kuwa mali za serikali.

Tutakapo pata kiongozi mkuu wa nchi anayeweza kusimamia hili Tanzania tutaruka kwenda mbele katika maendeleo.Mfano wa nchi ya China kuwaadhibu mafisadi ni mfano wa kuigwa na kila kiongozi mwanamapinduzi apendaye maendeleo ya watu wake.Kinyume cha hapo ni usanii tuu ambao hauna maana katika uongozi.
 
Ufisadi kwa makada wa CCM ni siri na budi uongelewe ndani ya vikao vya Chama na si barabarani. Mjumbe CCM amewajia juu wanaotabiri CCM kupata wakati mgumu kwenye uchaguzi ujao na kuanika siri za chama kwa kuwahusisha baadhi ya viongozi na ufisadi !

"Hawa wanaokitabiria chama mabaya kwenye chaguzi zijazo ni wajumbe wa NEC, wao wana nafasi ya kuingia kwenye vikao na kuyazungumza haya. Inakuwaje leo wazungumzie uchochoroni,"alihoji na kusisitiza: "Sisi vijana wa CCM tunao wajibu wa kukipinga kitendo hiki kwa nguvu zoeti."

Alisema kama suala hilo litaachwa liendelee, watakaoteseka ni vijana ambao wana muda mrefu wa kuendelea kukitumikia chama hicho.

"Ndugu zangu hili ni jambo la kusikitisha sana kuona watu wenye nafasi ndani ya vikao vya halimashauri kuu wakilizungumzia suala hilo uchochoroni kama tutaacha liendelea sisi ndio tutakaotaabika,"alisema Bashe.
Asante mjumbe - kumbe ufisadi ni sera ya siri ya CCM, kaazi kweli kweli, duh !
 
Naye mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi(CCM), Bw. Salum Londa amesema viongozi na wanachama wa CCM wanaokitabiria mabaya chama hicho wanatia shaka.

Huwezi mtu ukajitokeza tu na kusema CCM itashindwa, kwa tathmini gani uliyofanya? 'no reserch no right to speak (usizungumze bila utafiti)' nalazimika kuyasema haya kutokana na kauli za baadhi ya wana CCM ambazo zinatia shaka.
Haiwezekani chama kikazungumziwa nje ya chama, hii inaonesha maadili yamekwisha na ukizungumzia huko juu kwa juu inatuonesha kuwa huna mapenzi mema na chama chako na unatia mashaka makubwa.
CCM hatuna shaka na ushindi mwakani, hata bila wao CCM itashinda kwa kuwa haijawa mbaya kiasi hicho na bado inaaminika kwa wananchi wake hivyo tabia za kupaka matope kwa nia ya kupotosha iachwe mara moja.

Huyu ndiye Salum Londa, Meya na kinara wa mipango ya ufisadi wilayani Kinondoni - akiwataka wanachama wa CCM kutokuwa tayari kupokea kauli za viongozi au wanachama ndani ya chama hicho eti wanaopiga vita ufisadi.

Kutokana na haya ya upotoshaji unaofanywa nakumbuka kauli ya Mzee wetu Kawawa ( Mzee Rashid Kawawa) ambaye alisema mkiona mmoja wenu ndani ya boti mnayosafiria anatoboa, mtoseni afe peke yake ili ninyi msizame '...hivyo hatuko tayari kubaki na watu hao ndani ya chama

Huyo ndiye mtuhumiwa wa ufisadi wa viwanja Kinondoni anayetaka wale wote wanaodai kupiga vita ufisadi ndani ya CCM watoswe ili boti isizame.. wabaki mafisadi tuuu !
 
Naye KATIBU Mkuu wa CCM, Yusuf Makamba amepinga kauli ya makamu mwenyekiti wa zamani, John Malecela kwamba, chama hicho kitakuwa na wakati mgumu katika Uchaguzi Mkuu ujao.

Ufisadi anaozungumzia Malecela kwamba utakisambaratisha chama hicho mwakani ni wa kufikirika kwa sababu mpaka sasa hakuna mwenye ushahidi unaodhihirisha kwamba fulani ni fisadi.
Mimi siwajui hawa mafisadi. Hebu wewe nitajie jina la mtu mmoja ambaye una ushahidi kuwa ni fisadi, siyo kweli ila ni jambo ambalo linakuzwa tu.

Huyu ndiye Yusufu Makamba, aliyedai EPA ni mambo ya kufikirika tu na kuyaita uzushi. Makamba anayedai CCM yake haikufaidika kwa namna yoyote na KAGODA. Masikini Makamba yuko tayari kufa na tai shingoni !!
 
Hivi ni nani asiyejua kuwa Londa ni fisadi na mchumia tumbo. Kuchaguliwa kuwa mjumbe wa NEC kwa kumshinda Shy-Rose Bhanji kwa kariibu anataka kuonesha kuwa na yeye mrija wake umeongezeka kipenyo na umeshaingia kwenye buyu kubwa la asali. Ukweli ni kwamba TINGA TINGA alichoongea amekifanyia utafiti from the ground (field work) si yeye ndiye alikuwa "BUSANDA" na "BIHARAMURO" ambako anajua fika kuwa hawakushinda bali waliiba kura!. Sasa kazi itakuwa ngumu mwakani kuiba kura majimbo yote!?, Hawa vibaraka waache woga, maisha hayapo kwenye 10% tu za miradi, wafanye kazi kama wanataka kuendelea kupata " KURA" siyo longolongo kwani zina mwisho wake.
 
Naye NAIBU Waziri wa Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana, Dk Makongoro Mahanga amesema makada wa CCM wanaodai kupambana na ufisadi wanapaswa kudhibitiwa ili wasikivuruge chama kwa kuwa mafisadi ndani ya chama hicho hawazidi wanne.

Hawa wanaoitwa mafisadi wako wangapi? Mbona hawatajwi? Kuna watu ndani ya chama wamedhamiria kuiangusha CCM huku wakijifanya wanapambana na mafisadi ndani ya chama.
Suala hilo linapozungumzwa hadharani na wanachama wa CCM ni hatari. Hapa wanakichafua chama na ndio wanaosaidia vyama (vya siasa) vya upinzani.
Kama kuna tatizo, lipelekwe kwenye vikao na siyo kwenda kupiga kelele kwenye majukwaa na kukichafua chama machoni pa wananchi.
Namna suala hilo linavyozungumzwa sasa, inaonyesha kana kwamba kuna kundi kubwa la wanaCCM wanaojihusisha na ufisadi, lakini ukweli ni kwamba watuhumiwa wa ufisadi, hawazidi wanne !
Huo ni woga tu. Hakuna kitu kama hicho. Naunga mkono maelezo yaliyotolewa na Katibu wangu Mkuu (Yusuf Makamba) kupitia gezeti lenu (Mwananchi) toleo la leo jana akisema hayo ni mambo ya kufikirika.

Kaazi kweli kweli !
 
Back
Top Bottom