Malecela ahofia CCM kuwa katika hali ngumu 2010 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Malecela ahofia CCM kuwa katika hali ngumu 2010

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Keil, Aug 6, 2009.

 1. K

  Keil JF-Expert Member

  #1
  Aug 6, 2009
  Joined: Jul 2, 2007
  Messages: 2,214
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Malecela ahofia CCM kuwa katika hali ngumu 2010

  *ASEMA WABUNGE WENGI WATABWAGWA

  Jackson Odoyo na Neema Rugemalira

  MAKAMU Mwenyekiti Mstaafu wa CCM, John Samuel Malecela amekitabiria chama hicho wakati mgumu katika uchaguzi mkuu ujao 2010.

  Akijibu swali la waandishi kuhusu ufisadi na uchaguzi ujao wakati akikabidhi vifaa kwa walemavu vilivyotolewa na Askofu wa Kanisa la Christian Mission Fellowship, Mgullu Kilimba jana, Malecela alisema chama hicho kitakuwa na wakati mgumu kutokana baadhi ya wabunge wake kutotekeleza ilani ya chama na vita dhidi ya mafisadi.

  “Uchaguzi mkuu ujao utakuwa mgumu kwa CCM hasa wabunge kwa sababu baadhi yao hawaendi majimboni na hawafuati ilani ya CCM. Ugumu mwingine upo katika suala zima la mafisadi,” alisema Malecela na kuongeza:

  “Vita dhidi ya mafisadi ni ngumu kwa sababu ndani ya CCM kuna baadhi ya watu wanaokichafua chama kwa tabia zao za kuungana na mafisadi.”

  Mzee Malecela alisema hayo wakati tayari kukiwa na mvutano mkubwa ndani ya CCM baina ya kambi zilizojengeka ndani ya chama, huku kila kambi ikiituhumu nyingine kwa ufisadi.

  Malecela alisema baadhi ya wabunge wa CCM wanakiweka chama hicho katika wakati mgumu kwa sababu ya tabia zao za kutokwenda kwenye majimbo yao na kwamba, hawafuati ilani ya uchaguzi ya chama hicho.

  Hata hivyo, akizungumzia uchaguzi wa rais alisema atakuwa na wakati mzuri kwani kwa upande wake hali bado ni njema.

  Alisema pamoja na jitihada za mafisadi kutafuta kila njia ya kuungwa mkono na baadhi ya wana CCM ndani na nje ya bunge, ukweli ni kwamba vita hivyo ni vigumu na kwamba anaamini kuwa mwisho wa siku wapinga ufisadi watashinda.

  “Tunaopiga vita suala la ufisadi ndani ya CCM tutaendelea kusimama imara mpaka dakika za mwisho, mfano mzuri ni kile kilichotokea kwenye mkutano wa Bunge safari hii, nadhani mliona mambo yalivyokuwa moto. Hii yote ni kuhakikisha kuwa mafisadi yanashindwa,” alifafanua Mzee Malecela.

  Akitaja baadhi ya mambo ambayo mafisadi hayo yalipanga yafanyike ndani ya bunge hilo lakini wakashindwa, Makamu Mwenyekiti huyo mstaafu alisema kuwa ni pamoja na suala la uchimbaji wa madini kwenye mbuga za wanyama, Richmond pamoja na mgodi wa Kiwira.

  “Ndugu zangu ninawaambia, Tanzania ya leo hakuna uwezekano wa mpiga kura kununuliwa, watajaribu watashindwa; sana sana watajaribu kuleta hizo fedha zao ziliwe na wasipate kura na hiyo ndiyo njia pekee ya Mungu kuwaadhibu, kwa sababu hizo ni fedha za wananchi,” aliongeza Malecela.

  Hata hivyo alisema watakapo fanikiwa kuzima moto wa mafisadi kazi yao itakuwa ni moja tu ya kupambana na wapinzani wao ambao nao watajitahidi kutafuta mbinu za kuibuka na ushindi katika uchaguzi huo.

  “Baada ya vita vya mafisadi kumalizika tutabakia kazi ya kupambana na wapinzani wetu kwa sababu wao pia wanatafuta mbinu za kushinda uchaguzi ingawa tuna mbinu nyingi za kuwashinda,” alifahamisha Malecela.

  Alisema CCM ina mbinu nyingi na hawajawahi kuzitumia zote katika chaguzi zao na kwamba, baadhi ya mbinu mpya walizonazo walizitumia katika chaguzi ndogo zilizopita hivi karibuni na wakaibuka kidedea.

  “Tuna mbinu nyingi za kuwashinda wapinzani wetu, baadhi yake zilitumika katika chaguzi zilizopita na katika uchaguzi mkuu mwaka ujao tutazindua mbinu mpya ambazo hatujawahi kuzitumia.”

  Katika hatua nyingine Malecela alisema kutokana na vita hivyo kuwa vikali, ndiyo maana Spika wa Bunge, Samuel Sitta alisema kuwa matatizo makuu yanayowakabili ni vita dhidi ya mafisadi.

  “Vita ni vikali na mimi sina shaka yoyote kwamba mafisadi hao watashindwa, isipokuwa tunapaswa kuendeleza kasi ya kupambana nao.”

  Malecela alikuwa mgeni rasmi katika hafla ya kutoa vifaa mbalimbali vyenye thamani ya Sh58 milioni kwa walemavu vikiwemo viti, baiskeli za magurudumu matatu, vyoo magongo ya kutembelea na vingine vilivyotolewa na Kanisa la Christian Mission Fellowship.

  Hafla hiyo imefanyika nyumbani kwa mzee Malecela jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na Mbunge wa Same Mashariki, Anne Kilango Malecela.

  Askofu Kilimba wa kanisa hilo amesema tangu waanze kutoa huduma hiyo miaka minne iliyopita, wameishayafikia majimbo ya uchaguzi 38.

  ***************************************************
  Afadhali amekubali kwamba mwakani ngoma itakuwa nzito sana, na kitakachowatesa ni hizo agenda za ufisadi.

  Je, yaliyotokea juzi Bungeni inaweza kuwa ni sanaa ya CCM kuwahadaa wadanganyika kwamba wabunge wao (majority wakiwa wa CCM) wako makini kutetea maslahi ya taifa?

  Hizo mbinu walizonazo ni zipi? Wizi wa kura ama kutumia jeshi la polisi na tume ya uchaguzi ama ni zipi hizo?

  Kwanini kwenye ufisadi haongelei KAGODA? Maana wameikalia kimya kabisa as if imesahaulika.

  Ngoja tuone sanaa ya Bunge kwenye kikao cha 18 mwezi Novemba.
   
 2. Ncha

  Ncha JF-Expert Member

  #2
  Aug 6, 2009
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 254
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  wanampango wa kuiba kwa kutumia uchawi labda ndio style ambayo bado
   
 3. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #3
  Aug 6, 2009
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Mhuni tu huyu, hana jipya. ******* kuwa wana mbinu mpya.

  Hivi wizi ni kitu cha kujivunia mbele za watu na mbele ya wachungaji?


  Nasema ni mhuni hana nyimbo mpya huyu.

  Kambarage alikuwa sahihi kuhusu mhuni huyu!
   
  Last edited by a moderator: Aug 9, 2009
 4. Komamanga

  Komamanga JF-Expert Member

  #4
  Aug 6, 2009
  Joined: May 2, 2009
  Messages: 221
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Ni kweli inawezekana na namuomba sana Mungu iwe hivyo na naamini asilimia kubwa ya wabunge wa sasa hawatarudi kwenye nafasi hizo kwa kusindwa ila tuu kutakuwa na sura mpya ndani ya CHAMA CHA MAPINDUZI ambazo ndizo zitarejea
   
 5. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #5
  Aug 7, 2009
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,187
  Trophy Points: 280
  Hawaendi majimboni kwa sababu wanaogopa kuzomewa na kupopolewa kwa mawe na hapa washukuru vyombo vya dola walivyoviweka mfukoni kuwalinda. Pamoja na hayo ufisadi na uCCM kamwe haviwezi kutenganishwa.

  Kama hao wanaokichafua chama ndani ya CCM ni wachache, kwa nini wasitimuliwe ? Ukweli ni kuwa ni wengi, kama si wote, na wana nguvu na ndio maana vita dhidi yao ni ngumu. nani amfukuze nani ?

  Hii yote ni usanii - hao mnaowaita mafisadi ni wenzenu, mnakaa nao, mnakula nao na mnaishi nao. Hamuwezi kuwachukulia hatua madhubuti kwa maana kufanya hivyo ni sawa na kukata tawi la mti mliolikalia, hiyo haiwezekani kwa sababu hamtatoka salama. Mnaweza kukuta mwinda anakuwa mwindwa na hilo mnalijua sana.

  Mzee Malecela unakaa dunia gani hiyo, mbona kasi ya watu kununuliwa, kuzugwa na kulaghaiwa ndio inaongezeka. Wewe mwenyewe siku hizi unawasimamia vijana wako wakigawa chumvi hadi kanga kwa walalahoi ambao sera mbovu za CCM zimewalemaza toka wakiwa watoto hadi sasa wananza kuzeeka. Bahati yenu Tume ya Uchaguzi ikiongozwa na kada wa CCM Jaji Makame inawapakata, bila hivyo ni kuanguka tu !

  Inategemea baada ya hiyo unayodai vita vya mafisadi nani atakuwa kidedea ndani ya CCM. Ishara zote zaonyesha kuwa hao wanaopiga vita mpaka sasa hawasongi popote na kila wanapojaribu wananyamazishwa kisayansi (kwa rushwa? na hao hao mafisadi.

  Hii ni kweli mbinu za kuwashinda wapinzani mnazo kama kutoa rushwa, kununua shahada, kutumia jashi la polisi, tume ya uchaguzi n.k. Hiyo mbinu mpya tayari tunaona ikitumiwa Pemba katika uandikishaji wa daftari la kudumu la wapiga kura. Bila hizi mbinu CCM, kama Paulo mwenye mikono, haiwezi kuruhusiwa na wazalendo kukaa meza moja kula nao.

  Eti vita ni vikali, sorry Mzee Malecela, endelea kuamini hivyo lakini usijekuta mwisho wa siku umeachwa kwenye mataa !
   
 6. G

  Gashle Senior Member

  #6
  Aug 7, 2009
  Joined: Mar 30, 2007
  Messages: 116
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Binafsi yangu nafikiri wazee wetu kuna umri wakishafikia, ama uwezo wa kufikiri unakuwa unapungua kwa maana ya busara zinaanza kupungua taratibu, ama hawaishi kwenye realities! Alianza mzee wetu Kingunge, alivyomaliza kusema kila mtu akatamani bora asingesema aliyosema. Jana kumsikia Mzee Malecela anaongea kuhusu mbinu mpya ambazo hawaja release... kwangu nilipata simanzi.

  Tofauti na Mwl. Nyerere na hawa ndugu zetu ni kwamba Mwl alikuwa anaongelea wazi wazi uwezekano wa ku ditch CCM kama akiona imeacha misingi yake. Wazee wetu wenywe wako tayari kuibuka na mbinu mpya hata kama Chama kimeoza tayari.

  Mungu ibariki Tanzania
   
 7. M

  Mukubwa Senior Member

  #7
  Aug 7, 2009
  Joined: Aug 20, 2007
  Messages: 124
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Kwa kusema hivi ina maana bado atagombea tene mtera 2010? maana hajafanya lolote tangu enzi za mwalimu. pamoja na madaraka aliyoshika hata barabara ya lami kwenda kwao Mvumi hakuna sasa anasemaje wabunge hawafuati ilani ya uchaguzi ya ccm?
   
 8. J

  Jibaba Bonge JF-Expert Member

  #8
  Aug 7, 2009
  Joined: May 6, 2008
  Messages: 1,224
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  Nilifikiri mbinu ni kutekeleza ahadi na hivyo kuwashawishi wapiga kura ili wawapigie wagombea wa ccm! Kumbe ziko mbinu nyingi tu duu!

  hata hivyo hizi zimeshatumika sijui ambazo bado zitakuwaje.
  kutumia dola
  Kuiba kura
  Kuongeza masanduku yenye kura za wagombea wa ccm
  Kuwanunua wagombea wa upinzani ili wajitoe kwenye uchaguzi
  Kuwatisha wananchi kuwa hawatawaletea maendeleo ambayo hata hivyo hayapo hata kwa majimboyanayoongozwa na ccm
  Kuwatisha wasimamizi wa uchaguzi kuwa watapoteza kazi wakitangaza ushindi kwa wapinzani - mfano Biharamulo -Makamba
  Kutumia tume ya uchaguzi kutowapitisha kugombea wagombea wa upinzani
  Kutumia tume ya uchaguzi kuwapitisha kugombea wagombea wa ccm hata pale ambapo hawana sifa kisheria
  Kuhonga kwa kutumia mapesa ya EPA.
  Kununua shada za wapiga kura wanaodhaniwa ni wa upinzani
  Kukataa kuwaandikisha wapiga kura wanaostahili- pemba
  Kupandikiza mamluki kwenye vyama vya upinzani

  nafikiri kinachofuata ni ushirikina!
   
 9. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #9
  Aug 7, 2009
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 688
  Trophy Points: 280
  Huyu mzee anakichaa!! si mhuni, ni mwendawazimu........yani anaongea hadharani kuwa watashinda kwa mbinu???..............Lakini utaona Mitanzania mingine inakaa kwenye mistari ya kwenda kupiga kura na kuwapa kura....Ni laana au???!!

  Hakuna wakati mwingine.
   
 10. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #10
  Aug 7, 2009
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  Hivi lini CCM wamekuwa na wakati rahisi..ni majizi tu ya kura hasa huyu malecela ndo kinara wa mbinu za kukwiba kura..
   
 11. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #11
  Aug 7, 2009
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Hakika utabili wake bila shaka utakuwa kweli.

  naona sasa wananchi engi wameweza kujua haki zao bali tu wanaogpa vitisho.

  haya tusubiri.
   
 12. S

  Sebere Member

  #12
  Aug 7, 2009
  Joined: Jan 16, 2009
  Messages: 16
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  huyu mzee amechanganyikia kuhusu mbinu za uchaguzi. ccm haina mbinu mpya zaidi ya kutumai jeshi la polisi , kuhonga kanga ,tshirt na kofia.
   
 13. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #13
  Aug 7, 2009
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Ongezea chumvi na chupi kwenye orodha yako.
  Shame to John Malecela. Shame!
   
 14. Mateso

  Mateso JF-Expert Member

  #14
  Aug 7, 2009
  Joined: Aug 6, 2008
  Messages: 240
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  *****. Mbona hizo mbinu hakutumia kule Tarime. Yamezoea kutumia vyombo vya dola kushinda bila woga. Afadhali amejua kuwa watakuwa na hali ngumu jambo muhimu ni kuhimiza wapiga kura kutoogopa mbwa yoyote yule atakayesogelea kwenye kampeni au sehemu za kupigia kura. Kama wataleta polisi au wanajeshi kama Zanzbar piga mawe mpaka wafe. Wakati wa ukombozi umefika na tusipoutumia uchaguzi ujao vizuri watanzania watakuwa na maisha magumu kuliko yale ya miaka ya 80 tuliyokuwa tunaunga mstari kupata unga wa yanga na sukari ukilazimishwa kununua kibiriti na majani ya chai.Naomba tuzidi kuahanasisha wananchi kwa kila njia inayowezekana. Kama una ughungu na nchi yako ANZA SASA KUANDALIA NJIA ZA KUJIKOMBOA 2010.
  FIKRA SAWA KWA WOTE. MUNGU IBARIKI TANZANIA MUNGU WABARIKI WANAOPENDA UKOMBOZI.
   
  Last edited by a moderator: Aug 9, 2009
 15. J

  Jibaba Bonge JF-Expert Member

  #15
  Aug 7, 2009
  Joined: May 6, 2008
  Messages: 1,224
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  John Malecela: Tingatinga la CCM

  TINGATINGA lina majina mengi. Wapo wanaoliita gari, lakini pia wapo wanaoliita kuwa ni chombo au mashine inayotumika kuchonga au kutengeneza barabara.

  Lakini tabia moja ya tingatinga ni kwamba likishamaliza kazi ya kutengeneza au kuchonga barabara, haliruhusiwi tena kupita kwenye barabara hiyo, na badala yake magari mengine ndiyo yanayofaidi barabara iliyochongwa na tingatinga.

  Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), John Samwel Malecela, aliwahi kujifananisha na tingatinga na kuongeza kuwa sasa amechoka kuwa tingatinga ambalo linatumika kwa kazi muhimu na kusaulika baadaye.

  Malecela alijifananisha na tingatinga alipokuwa akirejesha fomu ya kuwania kiti cha urais mwaka 2005. Aliulizwa kwanini anawania nafasi hiyo wakati umri wake umemtupa mkono.

  Kutokana na swali hilo, Malecela alisema kwanini suala la umri wake linaonekana wakati wa kuwania urais lakini wakati mwingine anatumiwa kama tingatinga linalochonga barabara na kusaulika?

  Alikuwa na maana moja kubwa, nayo ni kwamba wakati wa shughuli nyingine muhimu, CCM humtumia na kumwona muhimu na hasa wakati wa kampeni za uchaguzi mdogo kama ule ambao kampeni zake zinaendelea Tunduru, lakini inapofika wakati wa kuwania urais, anawekewa mizengwe kama aliyowekewa mwaka 1995 na 2005 wakati anawania urais.

  Baada ya uchaguzi wa mwaka 2005 na jinsi CCM ilivyoendesha kampeni za mizengwe kumpata mgombea wake, mchakato ambao Malecela hakupendezwa nao, duru za siasa zilibashiri kuwa huenda Malecela angejitoa kwenye nafasi yake ya sasa ya Makamu Mwenyekiti, kwani baada ya Uchaguzi Mkuu, alitangaza kujiuzulu nafasi yake ya ukamanda wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM).

  John Malecela ni jina zito kwenye medani za siasa nchini tangu nyakati za uhuru. Ukiachia mbali ‘uhuni’ ambao marehemu Baba wa Taifa Mwl. Julius K. Nyerere alidai anao Malecela, bila kutoa maelezo. Malecela ni kigogo wa siasa za nchi hii.

  Si muiti mhuni kwa mapenzi yangu, la hasha, bali narejea kitabu cha Mwalimu Nyerere: ‘Hatima ya Tanzania na Uongozi Wetu’. Lakini kuna wahuni wengine serikalini ambao hata kama Nyerere hakuwataja kwenye kitabu chake, aliwahi kuwapayukia.

  Viongozi hao leo wapo madarakani kutokana na dhana ya kubebana na uana mtandao, lakini mbele ya Mwalimu wanabaki kuwa ni ‘wahuni’.

  Kutokana na umaarufu wake nchini, Malecela anaposema au kufanya jambo, mwangwi wake husikika nchi nzima. Kwani yeye kama si kukosa bahati, ukimuondoa mzee Rashid Kawawa, ndiye anayefuatia kwa ukongwe kwenye siasa za CCM na Tanzania kwa ujumla.

  Lakini je, ukongwe wake umemsaidia nini zaidi ya kumletea majuto na shinikizo na kubaki kuwa tingatinga? Kusema ukweli kama Malecela hatakaa akapanga jinsi ya kujionyesha kama mtu anayetabirika, ataziaga siasa akiwa hana heshima hata kidogo.

  Sana sana atakumbukwa kama kigeugeu na mtu anayelazimika kufanya kile asichotaka kukifanya, kutokana na kauli yake kuwa anafanywa tingatinga na asingependa kuona anaendelea kutumika kama tingatinga.

  Kabla ya kuwapo kwa zoezi la uchaguzi mdogo wa Jimbo la Tunduru unaofanyika Machi 18, baada ya aliyekuwa mbunge wake, Juma Akukweti, kufariki dunia kutokana na majeraha aliyoyapata kwenye ajali ya ndege iliyotokea Mbeya mwaka jana, Malecela hakutarajiwa kwamba angekwenda kuwa tingatinga katika uchaguzi huo.

  Binafsi nilidhani asingetia mguu Tunduru kwa sababu ya kuepuka dhana ileile ya kutumika kama tingatinga wakati wa uchaguzi mdogo na kuonekana hafai wakati wa kuwania urais.

  Kwanza, Malecela ana umri mkubwa na uzoefu usio kifani katika siasa za Chama Cha Mapinduzi, ambapo mizengwe ndiyo kanuni kuu. Bahati mbaya pamoja na uzoefu wake katika mizengwe, amekuwa muathirika namba moja wa mizengwe yenyewe.

  Ukiachia hili, ndiye mtu aliyefanya kazi serikalini kwa muda mrefu kuliko wote walio hai Tanzania.

  Kwani alianza kazi pindi tu tulipopata uhuru. Na alitumika katika serikali zote kwenye ngazi za juu kama uafisa wilaya, ubalozi, uwaziri na uwaziri mkuu na umakamu wa rais ukiachia mbali ubunge alioumiliki kwa muda mrefu.

  Wasifu wake unatisha, japo haumpi nafasi anayopaswa kuwa nayo katika siasa za Tanzania, zaidi ya kutumika kama tingatinga.

  Kwa wanaojua wasifu wake na umri wake, bila shaka walidhani anamaanisha alichokuwa akisema kwamba hataki kutumika kama tingatinga.

  Kwanza, nakubaliana naye kuwa kweli John Malecela ni tingatinga. Na kama tingatinga, siku zote linapotengeneza barabara huwa haliitumii. Maana kazi ya tingatinga ni kutengeneza barabara na si kuitumia. Tingatinga ni kama sufuria au kijiko, kazi ya vifaa hivi ni kuwatumikia wanaovimiliki.

  Hadi anashiriki kwenye Uchaguzi Mkuu mwaka 2005, Malecela amesimamia chaguzi ndogo za marudio 26 na kushinda kwa ‘tsunami’, na uchaguzi wa Tunduru utakuwa wa 27 kusimamiwa na tingatinga hilo. Malecela ambacho akijui ni kuwa ‘he is a tool in the hands of somebody’ (ni kifaa kinachotumiwa na mmiliki).

  Na kama asingekubali kutumika hivyo, bila shaka angeweza kukiweka pabaya Chama Cha Mapinduzi, si Tunduru tu, bali nchi nzima.

  Malecela ametia timu Tunduru, Je, ameahidiwa nini na chama 2010? Je, ni nafasi yake ya kutaka kuendelea na nafasi ya umakamu mwenyekiti? Je, uchaguzi huo wa Tunduru, unamjenga au unambomoa ndani ya chama chake?

  Laiti wananchi wa Tunduru wangejua kuwa wanayemsikiliza akiwapa matumaini na ahadi ni tingatinga linalotumika kwenye chaguzi kama hizo tu, wangemuadhibu kwa kutomchagua mgombea anayempigia debe.

  Kwa anayemjua Malecela, nyota yake ilizimika siku alipokaa Zanzibar na kupitisha maazimio ya kulibomoa azimio la Arusha, ambalo lilikuwa kama mwana kipenzi wa Mwalimu aliyelenga kuiondoa nchi hii kwenye unyang’au wa wenye madaraka popo, kutumikia mabwana wawili, yaani wananchi na matumbo yao.

  Tumkumbushe ya mwaka 1995 Malecela alipokuwa amejiandaa kugombea urais kwa tiketi ya CCM. Kwa waliokuwa wako karibu na kambi yake wanasema aliishawaahidi kuwa asingezuilika.

  Lakini nadhani wote bado tunakumbuka. Mwalimu alipoingia katika Ukumbi wa Chimwaga na kuuliza kama John alikuwamo kwenye orodha, na kutishia kuachana na CCM, akimtaka Malecela aondoe jina lake.

  Mara ya pili ilikuwa ni kwenye uchaguzi wa 2005. Kwa waliofuatilia vibweka, maandalizi na mikakati ya kusalitiana ili kupata kuteuliwa, hapana shaka wanakumbuka mzee mzima alivyokuwa amejipanga.

  Lakini yaliishia wapi? Kamati Kuu ya CCM iliamua kufunika jina lake, tena bila kutoa sababu.

  Malecela asiyefaa kwenye urais, sasa yuko Tunduru. Anaandaa njia ili bwana harusi apite. Yeye ni sawa na Yohana Mbatizaji. Tofauti ni kwamba Yohana Mbatizaji hakuwa kigeugeu wala mtu wa kupuuzwa.

  Laiti ningekuwa Malecela, siku mtu kama Kingunge Ngombale-Mwiru ambaye ni mgeni kwenye CCM akilinganishwa na Malecela alipoanza kuonekana kama ndiye namba mbili baada ya Kawawa badala ya Malecela, ningeachana na siasa za mizengwe za CCM.

  Hebu angalia Kingunge pamoja na kuvuka umri wa kuhudumia, bado yuko kwenye baraza la mawaziri akikaa bila kufanya kazi yoyote. Amepewa cheo hiki ili kuonyesha chama na rais wanavyomheshimu.

  Kwani ukifuatilia kwa karibu umri wake na wizara yake, hana kazi yoyote ya maana anayofanya kwenye baraza la mawaziri zaidi ya kuwa mzigo kwa mlipa kodi. Hayo tuyaache, yana mahali pake.

  Tukirejea kwa John Samwel Malecela, tusemezane na kusutana. Mtu mzima hasutwi. Adui wake ni yeye mwenyewe, kwa kukosa msimamo.

  Inakuwaje msomi na mtu mzima mwenye uzoefu usio kifani kama yeye, akaamua na kukubali kuendelea kuwa tingatinga huku akijua fika kuwa CCM haitaki awe rais!


  http://www.freemedia.co.tz/daima/2007/3/7/makala2.php
   
 16. Monsignor

  Monsignor JF-Expert Member

  #16
  Aug 7, 2009
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 523
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nawaoneeni huruma jamaa zangu subirini watu waamke waje wakute "MZEE" mmemsema vibaya. Hivi hamjui kuwa mzee huyu ni ifallible?
   
 17. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #17
  Aug 7, 2009
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,635
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Kauli ambazo huwapa Ushindi CCM siku zote ni kama hizi hapa chini:-

  Kauli kama hizi uweza kutolewa na Vichaa tu!
   
 18. Bill

  Bill JF-Expert Member

  #18
  Aug 7, 2009
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 4,145
  Likes Received: 1,238
  Trophy Points: 280
  Hawa akina Malecela ikiwa wanaipenda hii nchi waache kuiba kura, kisha bunge lijalo liwe na wabunge halali toka CCM na Kambi ya upinzani kwani hii italeta changamoto kubwa.

  Halafu sioni tatizo wabunge wengi wa CCM kuanguka. Kwa maslahi ya Taifa ni vyema zaidi wabunge wengi wa CCM wakapukutika.
   
 19. F

  Froida JF-Expert Member

  #19
  Aug 7, 2009
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,900
  Likes Received: 1,328
  Trophy Points: 280
  Namwonea huruma mzee mzima anasema mbinu wazijuazo wapinzani hazitatumika tena manake nini sasa watatumia jeshi manake wanaona polisi hawatatisha wananchi, wawe macho wananchi nao wanatafuta mbinu mpya wamechoka kudhurumiwa hawatakubali kupiga kura na kunyimwa haki ya kuwa na kiongozi wampendae ,lakini bora amekili kwamba CCM wanahali ngumu sana mwakani
   
 20. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #20
  Aug 7, 2009
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Call a spade, spade. Spade is not a spoon:eek:
   
Loading...