Malecela aangukia pua kwa mara nyingine... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Malecela aangukia pua kwa mara nyingine...

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Indume Yene, Aug 14, 2010.

 1. Indume Yene

  Indume Yene JF-Expert Member

  #1
  Aug 14, 2010
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 2,932
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Habari kutoka Dodoma zinadai kuwa aliyekuwa mbunge wa Mtera Mh. Malecela amepigwa chini wakati akiwa anategemea kurudishwa kwenye ugombea wa jimbo hilo. Habari vilevile zinadai kuwa Mzee Ruksa ndiye aliyegongelea msumari kwenye kipara cha mzee Malecela baada ya kuwashawishi wajumbe wa NEC wamtose J4 baada ya kuona upepo mbaya kwa SISIEMU.

  My take: Viongozi wa SISIEMU wanajikosha kwa wananchi kuwa Slaa na Chadema si kitu, lakini in behind the scene wanakiri kuwa UPEPO si mzuri kabisa kwa SISIEMU. Hongera Mzee Ruksa kwa kutambua hilo, waache akina Makamba waendelee kuhubiri hizo ngonjera.
   
 2. V

  Vakwavwe JF-Expert Member

  #2
  Aug 14, 2010
  Joined: May 16, 2009
  Messages: 507
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Na matokeo mengine vp? kuna changes nyingi kutokea kura za maoni?
   
 3. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #3
  Aug 14, 2010
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,203
  Likes Received: 867
  Trophy Points: 280
  Mwinyi amtosa Malecela

  • Awaambia wajumbe NEC mwacheni aende

  na Mwandishi wetu, Dodoma

  HARAKATI za baadhi ya wagombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) waliobwaga kwenye kura za maoni hivi karibuni za kurejeshwa katika kinyang'anyiro cha kuwania udiwani, ubunge na uwakilishi zimeota mbawa.

  Miongoni mwa wanasiasa wakongwe waliokuwa wakitarajia busara za Halmashauri Kuu ni aliyekuwa mbunge wa Mtera, John Samwel Malecela, ambaye alibwagwa na mwanasiasa mchanga, Livingstone Lusinde.


  Rais mstaafu wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi, ndiye aliyeongoza jahazi lililomzamisha Malecela, ambapo aliwataka wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), wasithubutu kurejesha jina la mkongwe huyo.


  Habari kutoka ndani ya kikao hicho kilichoongozwa na Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Jakaya Kikwete, zilisema kuwa suala la Malecela ambaye aliwasilisha malalamiko kupinga kushindwa kwake, liliwagawa wajumbe wa NEC, huku idadi kubwa wakitaka arejeshwe ulingoni.


  Kwa mujibu wa chanzo kimoja cha habari cha Tanzania Daima Jumapili, kutoka ndani ya NEC, kilisema kuwa Mwinyi aliwaambia wajumbe wa mkutano huo kuwa hali ya upepo wa kisiasa si nzuri kwa CCM kama waatanza kuwarejesha wagombea walioshindwa kwenye kura za maoni.


  "Suala la mzee Malecela lilitusumbua sana, lakini mzee Mwinyi alifanikiwa kuwashawishi wajumbe kwa kuwataka wamwache Malecela aende zake, kwani hali ya upepo wa kisiasa nchini si nzuri kwa CCM, hasa katika kipindi hiki kama tutawabadilisha wagombea waliochaguliwa na wananchi," alisema.


  Kwa hatua hiyo, matumaini ya mzee Malecela kurejea bungeni kama alivyoahidi kwamba atamsaidia Samuel Sitta kurejea kwenye kiti cha uspika kupitia jimbo, yamefutika na sasa ana subiri huruma ya Rais Kikwete kupitia nafasi kumi za

  uteuzi alizonazo kwa mujibu wa Katiba.

  Mbali na hatua hiyo, NEC imeridhia mawaziri wote walioshindwa kwenye kura za maoni wasirejeshwe kwa mlango wa nyuma, licha ya kuwapo kwa baadhi ya shinikizo la kutaka warejeshwe kutokana na mchango wao walioutoa.


  Duru za siasa kutoka ndani ya kikao hicho zilisema kuwa NEC haikutaka kuangalia malalamiko na mapingamizi yaliyowasilishwa katika baadhi ya majimbo ya mawaziri walioanguka, lakini wana haki ya kutafuta haki zao kwenye vyombo vya sheria.

  Hata hivyo ndoto za aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Soka nchini (TFF), Fredrick Mwakalebela, kuwania ubunge wa Jimbo la Iringa Mjini, zilitoweka baada ya NEC kwa kauli moja kuamua kulikata jina lake, kwa madai kuwa amefunguliwa kesi ya kutoa rushwa na Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (TAKUKURU).

  Nafasi hiyo ya Mwakalebela sasa itazibwa na mbunge aliyemaliza muda wake, Monica Mbega, ambaye alikuwa akikabana koo na katibu mkuu huyo wa zamani wa TFF.

  Mgombea mwingine aliyeonja chungu ya NEC ni Hussein Bashe, aliyemshinda Mbunge wa Nzega, Lucas Selelii, ambapo NEC ilibariki uamuzi wa Kamati Kuu wa kutengua ushindi wake kutokana na utata wa uraia alionao kada huyo.

  "Kwa kifupi katika maeneo mengi, NEC imerejesha majina yale yale ya washindi wa kura za maoni, lakini bado tuna mikoa kumi ambayo haijapitiwa na tunatarajia kurejea saa tatu usiku kumalizia mikoa mingine, wabunge wa viti maalumu na Baraza la Wawakilishi," alisema.


  Mawaziri ambao walitemwa katika kinyang'anyiro hicho ni Diodarus Kamala (Ushirikiano wa Afrika Mashariki), Shamsha Mwangunga (Maliasili na Utalii) na Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Mwantum Mahiza.


  Wengine ni Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Aisha Kigoda na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, Joel Bendera.


  Tanzania Daima Jumapili imedokezwa kuwa baadhi ya wagombea walioshindwa hivi sasa wana mpango wa kuhamia vyama vya upinzani lakini wanaogopa kushughulikiwa na chama chao, hasa kwa wale wanaotuhumiwa kwa kutoa rushwa.


  Wagombea hao wana hofu kuwa iwapo watahama, CCM inaweza kuweka mkono wake kwa TAKUKURU ili kuwafikisha mahakamani kwa lengo la kuwakomoa.


  Miongoni mwa wanaotajwa kujiunga na CHADEMA ni aliyekuwa Mbunge wa Maswa, John Shibuda, ambaye wiki iliyopita aliweka wazi kuwa kura za maoni za chama hicho zilitawaliwa na rushwa.


  Shibuda aliweka wazi nia yake ya kuhama chama hicho iwapo malalamiko yake hayatafanyiwa kazi na vikao vya juu vya chama hicho vilivyoketi mjini Dodoma.
   
 4. Mwawado

  Mwawado JF-Expert Member

  #4
  Aug 14, 2010
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 998
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 35
  Kutoka NEC wagombea wa CCM ni hawa


  ARUSHA

  i. Arusha: Dr. Batilda BURIANI
  ii. Arumeru East: Jeremiah SUMARI
  iii. Arumeru West: Goodluck Ole MEDEYE
  iv. Karatu: Dr. Wilbald LORRI
  v. Longido: Michael LAIZER
  vi. Monduli: Edward LOWASSA
  vii. Ngorongoro: Saning’o Ole TELELE

  IRINGA

  i. Iringa Urban Monica MBEGA (Fredrick Mwakalebela - NJE)
  ii. Isimani: William LUKUVI
  iii. Kalenga: William MGIMWA
  iv. Kilolo: Prof. Peter MSOLLA
  v. Ludewa: Deo FILIKUNJOMBE
  vi. Makete: Dr. Binilith MAHENGE
  vii. Mufindi North: Mohamed MGIMWA
  viii. Mufindi South: Menrad KIGOLA
  ix. Njombe North: Deo SANGA (Jah People)
  x. Njombe South: Anne MAKINDA
  xi. Njombe West: Gerson LWENGE

  KAGERA

  i. Nkenge: Assumpter MSHAMA
  ii. Bukoba Urban: Khamis KAGASHEKI

  iii. Bukoba Rural: Jasson RWEIKIZA
  iv. Muleba North: Charles MWIJAGE
  v. Muleba South: Anna TIBAIJUKA
  vi. Chato: John MAGUFULI
  vii. Kyerwa: Eustace KATAGIRA
  viii. Karagwe: Gosbert BLANDES
  ix. Biharamulo: Oscar MUKASA
  x. Ngara: Deogratias NTUKAMAZINA

  KIGOMA

  i. Kigoma Urban: Peter SERUKAMBA
  ii. Kigoma South: Gulam KIFU
  iii. Kasulu Urban: Neka NEKA
  iv. Kasulu Rural: Daniel NSANZUGWANKO
  v. Manyovu: Albert NTABALIBA
  vi. Buyungu: Christopher CHIZA
  vii. Muhambwe: Jamal TAMIMU
  viii. Kigoma North: Rabinson LEMBO

  KILIMANJARO

  i. Moshi Urban: Justin SALAKANA
  ii. Moshi Rural: Dr. Cyril CHAMI
  iii. Rombo: Basil MRAMBA
  iv. Same East: Anne MALECELA
  v. Same West: David DAVID
  vi. Hai: Fuya KIMBITA
  vii. Vunjo: Chrispin MEELA
  viii. Mwanga: Prof. Jumanne MAGHEMBE
  ix. Siha: Aggrey MWANRI

  MANYARA

  i. Babati Urban: Kisyeri CHAMBIRI
  ii. Babati Rural: Jitu SONI
  iii. Hanang: Dr. Mary NAGU
  iv. Kiteto: Benedict Ole NANGORO
  v. Mbulu: Philip MARMO
  vi. Simanjiro: Christopher Ole SENDEKA

  MARA

  i. Musoma Urban: Vedasto MATHAYO Manyinyi
  ii. Musoma Rural: Nimrod MKONO
  iii. Mwibara: Alphaxard LUGOLA
  iv. Bunda: Stephene WASSIRA
  v. Rorya: Lameck AIRO
  vi. Tarime: Nyambari NYANGWINE
  vii. Serengeti: Dr. Stephene KEBWE

  MBEYA

  i. Mbeya Urban: Benson MPESYA
  ii. Mbeya Rural: Luckson MWANJALA
  iii. Kyela: Dr. Harrison MWAKYEMBE
  iv. Mbarali: Dickson KILUFI
  v. Lupa: Victor MWAMBALASWA
  vi. Songwe: Philipo MULUGO
  vii. Rungwe East: Prof. Mark MWANDOSYA
  viii. Rungwe West Prof. David MWAKYUSA
  ix. Ileje: Aliko KIBONA
  x. Mbozi Mashariki: Godfrey ZAMBI
  xi. Mbozi West: Dr. Luka SIAME

  MOROGORO

  i. Morogoro Urban: Aziz ABOOD
  ii. Morogoro South East: Dr. Lucy NKYA
  iii. Morogoro South: Innocent KALOGERIS
  iv. Mvomero: Amos MAKALA
  v. Ulanga East: Celina KOMBANI
  vi. Ulanga West: Haji MPONDA
  vii. Gairo: Ahmed SHABIBY
  viii. Kilosa: Mustafa MKULO
  ix. Mikumi: Abdulsalaam SULEIMAN
  x. Kilombero: Abdul MTEKETA

  MTWARA

  i. Mtwara Urban: Murji MOHAMED
  ii. Mtwara Rural: Hawa GHASIA
  iii. Masasi: Mariam KASEMBE
  iv. Lulindi: Jerome BWANAUSI
  v. Tandahimba: Juma NJWAYO
  vi. Newala: George MKUCHIKA
  vii. Nanyumbu: Dunstan MKAPA

  MWANZA

  i. Ilemela: Anthony DIALLO
  ii. Nyamagana: Laurence MASHA
  iii. Busega: Dr. Kamani MLENGENYA
  iv. Magu: Dr. Festus Limba
  v. Kwimba: Sharif MANSOOR
  vi. Sumve: Richard NDASA
  vii. Geita: Donald MAX
  viii. Nyang’wale: Hussein AMAR
  ix. Sengerema: William NGELEJA
  x. Buchosa: Charles TIZEBA
  xi. Misungwi: Charles KITWANGA
  xii. Ukerewe: Getrude MONGELA.

  RUVUMA

  i. Songea Urban: Emmanuel NCHIMBI
  ii. Peramiho: Jenister MHAGAMA
  iii. Namtumbo: Vita KAWAWA
  iv. Tunduru South: Mtutura MTUTURA
  v. Tunduru North: Ramo MAKANI
  vi. Mbinga West: Capt. John KOMBA
  vii. Mbinga East: Gaudence KAYOMBO

  TABORA

  i. Tabora Urban: Ismail RAGE
  ii. Tabora North: Sumar MAMLO
  iii. Urambo East: Samuel SITTA
  iv. Urambo West: Prof. Juma KAPUYA
  v. Igunga: Rostam AZIZ
  vi. Sikonge: Said NKUMBA
  vii. Igalula: Athuman MFUTAKAMBA
  viii. Bukene: Seleman ZEDI
  ix. Nzega: Hamis KIGWANGALA (Hussein Bashe - NJE)

  Matokeo ya Mikoa mingine bado.
   
 5. K

  Kanyafu Nkanwa JF-Expert Member

  #5
  Aug 14, 2010
  Joined: Jul 8, 2010
  Messages: 812
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  List of the endorsed candidates

  [​IMG] The list of the names of parliamentary aspirants endorsed by the CCM National Executive Committee:

  ARUSHA

  i. Arusha: Dr. Batilda BURIANI
  ii. Arumeru East: Jeremiah SUMARI
  iii. Arumeru West: Goodluck Ole MEDEYE
  iv. Karatu: Dr. Wilbald LORRI
  v. Longido: Michael LAIZER
  vi. Monduli: Edward LOWASSA
  vii. Ngorongoro: Saning’o Ole TELELE

  IRINGA

  i. Iringa Urban Monica MBEGA
  ii. Isimani: William LUKUVI
  iii. Kalenga: William MGIMWA
  iv. Kilolo: Prof. Peter MSOLLA
  v. Ludewa: Deo FILIKUNJOMBE
  vi. Makete: Dr. Binilith MAHENGE
  vii. Mufindi North: Mohamed MGIMWA
  viii. Mufindi South: Menrad KIGOLA
  ix. Njombe North: Deo SANGA (Jah People)
  x. Njombe South: Anne MAKINDA
  xi. Njombe West: Gerson LWENGE

  KAGERA

  i. Nkenge: Assumpter MSHAMA
  ii. Bukoba Urban: Khamis KAGASHEKI

  iii. Bukoba Rural: Jasson RWEIKIZA
  iv. Muleba North: Charles MWIJAGE
  v. Muleba South: Anna TIBAIJUKA
  vi. Chato: John MAGUFULI
  vii. Kyerwa: Eustace KATAGIRA
  viii. Karagwe: Gosbert BLANDES
  ix. Biharamulo: Oscar MUKASA
  x. Ngara: Deogratias NTUKAMAZINA

  KIGOMA

  i. Kigoma Urban: Peter SERUKAMBA
  ii. Kigoma South: Gulam KIFU
  iii. Kasulu Urban: Neka NEKA
  iv. Kasulu Rural: Daniel NSANZUGWANKO
  v. Manyovu: Albert NTABALIBA
  vi. Buyungu: Christopher CHIZA
  vii. Muhambwe: Jamal TAMIMU
  viii. Kigoma North: Rabinson LEMBO

  KILIMANJARO

  i. Moshi Urban: Justin SALAKANA
  ii. Moshi Rural: Dr. Cyril CHAMI
  iii. Rombo: Basil MRAMBA
  iv. Same East: Anne MALECELA
  v. Same West: David DAVID
  vi. Hai: Fuya KIMBITA
  vii. Vunjo: Chrispin MEELA
  viii. Mwanga: Prof. Jumanne MAGHEMBE
  ix. Siha: Aggrey MWANRI

  MANYARA

  i. Babati Urban: Kisyeri CHAMBIRI
  ii. Babati Rural: Jitu SONI
  iii. Hanang: Dr. Mary NAGU
  iv. Kiteto: Benedict Ole NANGORO
  v. Mbulu: Philip MARMO
  vi. Simanjiro: Christopher Ole SENDEKA

  MARA

  i. Musoma Urban: Vedasto MATHAYO Manyinyi
  ii. Musoma Rural: Nimrod MKONO
  iii. Mwibara: Alphaxard LUGOLA
  iv. Bunda: Stephene WASSIRA
  v. Rorya: Lameck AIRO
  vi. Tarime: Nyambari NYANGWINE
  vii. Serengeti: Dr. Stephene KEBWE

  MBEYA

  i. Mbeya Urban: Benson MPESYA
  ii. Mbeya Rural: Luckson MWANJALA
  iii. Kyela: Dr. Harrison MWAKYEMBE
  iv. Mbarali: Dickson KILUFI
  v. Lupa: Victor MWAMBALASWA
  vi. Songwe: Philipo MULUGO
  vii. Rungwe East: Prof. Mark MWANDOSYA
  viii. Rungwe West Prof. David MWAKYUSA
  ix. Ileje: Aliko KIBONA
  x. Mbozi Mashariki: Godfrey ZAMBI
  xi. Mbozi West: Dr. Luka SIAME

  MOROGORO

  i. Morogoro Urban: Aziz ABOOD
  ii. Morogoro South East: Dr. Lucy NKYA
  iii. Morogoro South: Innocent KALOGERIS
  iv. Mvomero: Amos MAKALA
  v. Ulanga East: Celina KOMBANI
  vi. Ulanga West: Haji MPONDA
  vii. Gairo: Ahmed SHABIBY
  viii. Kilosa: Mustafa MKULO
  ix. Mikumi: Abdulsalaam SULEIMAN
  x. Kilombero: Abdul MTEKETA

  MTWARA

  i. Mtwara Urban: Murji MOHAMED
  ii. Mtwara Rural: Hawa GHASIA
  iii. Masasi: Mariam KASEMBE
  iv. Lulindi: Jerome BWANAUSI
  v. Tandahimba: Juma NJWAYO
  vi. Newala: George MKUCHIKA
  vii. Nanyumbu: Dunstan MKAPA

  MWANZA

  i. Ilemela: Anthony DIALLO
  ii. Nyamagana: Laurence MASHA
  iii. Busega: Dr. Kamani MLENGENYA
  iv. Magu: Dr. Festus Limba
  v. Kwimba: Sharif MANSOOR
  vi. Sumve: Richard NDASA
  vii. Geita: Donald MAX
  viii. Nyang’wale: Hussein AMAR
  ix. Sengerema: William NGELEJA
  x. Buchosa: Charles TIZEBA
  xi. Misungwi: Charles KITWANGA
  xii. Ukerewe: Getrude MONGELA.

  RUVUMA

  i. Songea Urban: Emmanuel NCHIMBI
  ii. Peramiho: Jenister MHAGAMA
  iii. Namtumbo: Vita KAWAWA
  iv. Tunduru South: Mtutura MTUTURA
  v. Tunduru North: Ramo MAKANI
  vi. Mbinga West: Capt. John KOMBA
  vii. Mbinga East: Gaudence KAYOMBO

  TABORA

  i. Tabora Urban: Ismail RAGE
  ii. Tabora North: Sumar MAMLO
  iii. Urambo East: Samuel SITTA
  iv. Urambo West: Prof. Juma KAPUYA
  v. Igunga: Rostam AZIZ
  vi. Sikonge: Said NKUMBA
  vii. Igalula: Athuman MFUTAKAMBA
  viii. Bukene: Seleman ZEDI
  ix. Nzega: Hamis KIGWANGALA
   
 6. V

  Vakwavwe JF-Expert Member

  #6
  Aug 15, 2010
  Joined: May 16, 2009
  Messages: 507
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Big UP Mhandisi Ramo Makani wherever you are....you are one of the most effective people i have ever met...
   
 7. Malafyale

  Malafyale JF-Expert Member

  #7
  Aug 15, 2010
  Joined: Aug 11, 2008
  Messages: 11,214
  Likes Received: 3,626
  Trophy Points: 280
  CCM ni muflisi kisiasa;Mramba na Chenge hawakustahili hata kugombea;hawa wana kashfa za wazi kabisa na ni doa lingine kwa wana CCM hilo,anyway nakupongeza Dr Kigwangala kwa kupata nafasi hiyo Nzega ingawaje umeipata kwa kutumia demokasia-tata!

  Ndugu yangu Sikonge nahisi hapo ulipo ni maumivu tu,Said Nkumba karudi tena eheheheheheh!
   
 8. Mwawado

  Mwawado JF-Expert Member

  #8
  Aug 15, 2010
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 998
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 35
  CC/NEC wametengua ushindi wa Fredrick Mwakalebela aliyekuwa mshindi wa kura za Maoni Iringa Mjini,Ni wazi kuwa Ushindi wa Waziri Margreth Sitta (Viti maalumu Jumuiya ya wanawake - Tabora),Fadhili Ngajilo (UVCCM - Iringa) na Easter Mambali (UVCCM - Tanga) utatenguliwa kwa sababu wote wameshitakiwa na Takukuru kwa madai ya kukiuka sheria ya Gharama za Uchaguzi.
   
 9. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #9
  Aug 15, 2010
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  Hiki chama cha mafisadi ama kweli hakina mwelekeo, itakuaje umuengue Mwakalebele kwa shutuma za kutoa rushwa na hata bado hajafikishwa mahakamani halafu in the same breath ukawapitisha [Mramba na Chenge] watu waliofikishwa mahakamani kwa shutuma za rushwa babu kubwa[ MEGA_ CORRUPTION]!! Double standard ya namna hii haijawahi kutokea.Hii lack of consistency itakiyumbisha sana hiki chama.
   
 10. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #10
  Aug 15, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Huyu si alikuja hapa kusema amegaragazwa? Wapi Selelii waliyesema alikuwa #2?
   
 11. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #11
  Aug 15, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,607
  Likes Received: 6,197
  Trophy Points: 280

  Mazee kama wabunge wenyewe ndio type hizi tunazoziona hapa (CHADEMA Regia Mtema, CCM Hamis Kigwangala ) basi tumekwisha.

  Hamna CHADEMA wala CCM, kwa mtaji huu wote waganga njaa tu.
   
 12. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #12
  Aug 15, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Of course mimi nafanya u-bandwagon tu hapa, as i know 4 sure nothing serious or good can come out of politix. Unahitaji architecture kudesign jumba kama la Sydney Oprah House, unahitaji mwandishi mjuvi kutunga vitabu vyenye uoni kama akina Jules Verne, unahitaji mhandisi kujenga barabara zilizoiviriga kama nyoka wanaofanya mating, and the list goes on..sasa swali la kujiuliza mwasiasa anawezaje kuwa bosi wa hawa wote while s/he knows NOTHING??

  Jibu ni rahisi tu, huezi kuvuna madafu kwa kupanda chelewa.
   
 13. Malafyale

  Malafyale JF-Expert Member

  #13
  Aug 15, 2010
  Joined: Aug 11, 2008
  Messages: 11,214
  Likes Received: 3,626
  Trophy Points: 280
  Sahihisho kwa Bulesi;

  Mheshimiwa Andrew Chenge HAJAWAHI kufikishwa mahakamani kwa kosa lolote linalohusiana na rushwa;kesi yake iliyopo kwenye mahakama moja ya Jijini Dar inahusiana kuendesha gari vibaya na hivyo kusababisha vifo,anashtakiwa pia kwa kosa la kuendesha gari bila kuwa na BIMA!

  Ni kawaida kwa binadamu kusahahu!
   
 14. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #14
  Aug 15, 2010
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,366
  Likes Received: 7,008
  Trophy Points: 280
  Malafyale Heshima Mkuu
  Ni kweli Mr Chenge hajaenda mahakamani bado, lakini anatuhuma na amekili ana pesa kwenye kisiwa cha jersey (Billions) ambazo anaziita Visenti na ambazo kwa Mashahara wake na marupurupu hata akefanya serving nzuri hasingeweza kuzifikisha hizo fedha, swali linakuja amezipata wapi hizo pesa? mojamoja kwa moja hiyo ilikuwa ni "disco"
  Chenge anaungana na hawa Mramba, Rage ambaye alishafungwa kwa wizi za fedha za by then FAT, R Azizi, E Lowasa,
   
 15. e

  echonza Senior Member

  #15
  Aug 15, 2010
  Joined: Jun 25, 2009
  Messages: 163
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Acha mafisadi waangushane wao kwa wao! Sisi ni watazamaji tu, na mwisho wa siku tutabaki tunadunda kwa ushindi wetu wa kulikomboa taifa kutoka katika kunyonywa kwa muda mrefu. Nawasihi waliojiandikisha kupiga kura wajitokeze kwa wingi siku ya Oktoba 31 ili kutimiza haki yao ya msingi.
   
 16. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #16
  Aug 15, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Penye red: Nilikuwa naamini tangu mwanzo kwamba TAKUKURU hufanya kazi yake kutokana na maelekezo na msukumo kutoka viongozi wa CCM.
   
 17. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #17
  Aug 15, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Nauliza: Hivi Selelii alikamatwa kwa vitendo vya rushwa katika zoezi la kura ya maoni? Kama aliibuka No 2 kwa nini asipewe yeye badala ya Bashe? Mimi naona kwamba Seleli ni victim wa kwanza wa maamuzi ya CC/CCM-NEC kutokana na msimamo wake madhubuti wa kupinga ufisadi. Hii ndiyo CCM -- imejionyesha waziwazi kwamba haipendi viongozi wanaoutuhumu utawala kuhusu ufisadi.
   
 18. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #18
  Aug 15, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Huyu Rage hivi imekuwaje? alishafungwa huyu sio? Sasa imepigwa pasi ya kisigino au imekueje?
   
 19. Butola

  Butola JF-Expert Member

  #19
  Aug 15, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 2,222
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Ni kwa ajili ya kujenga tu umoja ndani ya chama, na kisiasa wameifanya homwework yao vizuri sana,wamempa furaha Mpiganaji Seleli na wafuasi wake kwa kumuondoa mbaya wake aliyemsumbua kwa muda mrefu na kumwangusha katika kura za maoni lakini pia wamempooza Bashe na wafuasi wake kwa kutomteua adui yake.

  Mwisho wa siku wote watafarijika na kumpigia kampeni Dr Hamisi Kigwangala.
   
 20. senator

  senator JF-Expert Member

  #20
  Aug 15, 2010
  Joined: Aug 9, 2007
  Messages: 1,927
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 133
  Ila hii ya Dr HAMIS NAONA MBELEKO YA WAZI KABISA!! Kweli NEC kuna maamuzi ya Ajabu..
   
Loading...